Naomba ushauri: Miaka 18 iliyopita niliingia kwenye uhusiano na ‘Bi Mdogo’ na kuzaa naye watoto 2

Naomba ushauri: Miaka 18 iliyopita niliingia kwenye uhusiano na ‘Bi Mdogo’ na kuzaa naye watoto 2

OMBI WAKUU NA USHAURI

hii nyumba niifanye nini, ni nyumba kubwa,
Ipo kwenye kiwanja cha eka moja,

Eneo ni ni zuri sana, sasa hivi nyumba ni nyingi, lakini ya kwangu kila mtu anaitamani,

Ila bado haijaisha,

Madilirisha nilishaweka ya aluminium bado matatu tu ya dining room
Uza nyumba chukua watoto uishi nao kwa bi mkubwa
 
Nilisubscribe huu uzi ukiwa na post 10,saivi naona 1.6k..wtf is going on here?..Ngoja nikae chini niupitie.
 
Michepuko ni muhimu kwenye maisha yetu,tutapambana nayo tu,kwani nasema uwongo ndgu zangu
Nimesoma hadi sehemu ya 21
Itoshe kusema utavuna ulichopanda.
Mnatega wenyewe mabomu yakianza kuwalipukia mnalia.
Hii iwe fundisho na kwa wanaume wengine wenye macho juujuu na tamaa za kijinga..badala kukaa na familia zao wanaenda hangaika nje..na mtakufa siku si zenu.
 
Yaani hapa natoka church, nishaanza kupata upako! Yaani mtu anasema "amepata viwili" shetani ananishawishi vinginevyo wakati ni viwanja viwili; Eh Bwana Mwokozi!!!
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
 
Huyo mwanasheria aseme nini hujui kwani, umekaa na mwanamke miaka mingi, umeamua kumuacha mlichochuma mnagawana nusu kwa nusu.

Hizo room 30 heri ukajenge sehemu nyingine. Hapo gawaneni uende kwako japo unaonekana king'ang'anizi.
Hakuna sheria ya kugawana nusu kwa nusu Madam, hata kama mmeishi wote miaka mia, kuna mambo mengi sana yanaangaliwa,
Kwa ufahamu wangu mdogo baada ya kupelekana ofisi ya kata, nilikuwa tayari nafahamu nini nitapata, nilikuwa nimepitia juu juu sheria za ndoa kwenye kitabu fulani hivi,

Yule afisa kata anayeshughulika na jamii, moja ya kitu alichosema ndio hicho unachosema wewe, nusu kwa nusu, na alikuwa anasoma kwenye kakitabu Hako hako,
Lakini hakumaliza sentensi yote, nikamwambia endelea kusoma, akakataa akanniambia nisimfundishe kazi,

Lakini mojawapo ya vitu wanavyoangalia ni nani Macha giant zaidi katika ujenzi nani amechangia sana malezi na masomo ya watoto, nani anayesababisha ndoa ivunjike na aina ya makosa vile vile,

Basi alipokataa kumalizia kusoma, nikakasilika na kikao kikavunjika, ndio nikaenda mahakamani

Ingekuwa ni hivyo unavyowaza, mbona watu wangekuwa wanavunja ndoa makusudi ili wagawane kila mmoja aende zake

Hivi unajua kuna ndoa nyingine mtu anaomba mwenzie afe ili aachiwe mali, na kila unaporudi anachukia kukuona bado unadunda,

Sasa kama ni nusu kwa nusu ana haja gani ya kusubiri mpaka ufe,

Na yeye amesubiria miaka 30 ufe lakini hufi,

DUNIA HII MAMA MDOGO IONE HIVYO HIVYO
 
Kaka mwitore,uza nyumba ila Mnunuaji uwe we we umzunguuke iwe yako shem yeye umlipe aondoke.
Hiyo poa kabisa, nimeliweka kichwani ni wazo zuri kabisa,
Ahsante sana sana sana
Hilo ni neno.
Ila naona kuna ishu moja hapa kidogo ni ngumu,
Inabidi niingie gharama ya kununua kiwanja tena kwa ajili ya watoto,
Halafu nianze ujenzi, na kipindi hicho wale watoto sijui wataishi wapi,
Maana nyumba lazima aingie mtu ( aliyenunua)
Lakini hilo halinipi shida ngoja nianze kulifanyia wazo hili kazi
 
Binafsi naamini huyu bi mdogo alikuwa na mapenzi na wewe. Mwanamke mpaka kufikia hatua ya kuzaa na wewe kuna sehemu ndani ya moyo wake unakupenda. Kumbuka pia una mke mkuu, upendo wake kwako ulikuwa unakutana na kizingiti cha wewe kuwa na mke, so inabidi pia uvae viatu vyake. Pia duniani hakuna upendo unaokuja bila ya "kisababishi". Kila mtu anampenda mtu flani kwa sababu ya kitu flani. Huo ndio uhalisia. Unaweza kupendwa kwa sababu ya uhandsome wako. Unaweza kupendwa kwa sababu ya urembo wako, usingekuwa mrembo usingependwa. Unaweza kupendwa kwa fedha zako. Hakuna kupendwa bila kisababishi. Kisababishi kikitoweka either utaachwa au utavumiliwa.
Kama wewe KHUMBU alivyokuwa anakipenda mwanzoni, ila baadae akabadilika mno.. (joke)
Ndo kama ilivyomtokea Mzee Baba, mwanzoni mapenzi yalikuwepo as the days going on kila kitu kikabadilika
 
Hii stori kuna mambo yamefichwa, kwanza upande wa bi mkubwa hatujaambiwa ukweli
Pili yawezekana huyo sio mchepuko
Angekuwa mchepuko wachungaji wangefuata nini kusuluhisha?
Kama ni mchepuko mama mzazi wa mleta mada angefikaje kwa uhuru nyumbani hapo?

Unapotaka ushauri eleza jambo kwa uhalisia wake maana watu watakushauri kwa kile ulichoeleza, ukidanganya utashauriwa kwa kitu ambacho hakipo na ushauri hautasaidia
Hivi hili swali nimeshalijibu sana, hata kabla hujauliza, labda mimi sijui niki reply kama hivi, nikiwa kwenye comment ya 1400 na uzi upo mbele sana, maana naona tayari imefika 1700 huko, je hili jibu litaonekana wapi ni mbele ya 1700 au hapa nilipo kwenye 1400,
Halafu mtu akianzia au akiingia sasa hivi hawezi kuona tena

Ushauri tafadhali

Maana naona narudia kujibu kitu ambacho nilishakijibu,
 
Kweli mie nimekuelewa na nikweli unavyo simulia, ila madhaifu yako yafanyie kazi:

1.Usipende mwana mke kupitiliza hatakama umezaa nae

2.Never ever trust a woman hata kama umekanae miaka 20.

3.Umezidisha kutumia logic na common sense kwa mkeo some Time ujinga na ubabe ni suluhisho kwa wana wake.

Usimuachie nyumba wala usiiuze acha tu hiyo ni mali yako labda akuue.
4. Anza maisha mengine (move on) upya wewe bado mdogo at 50yrs tafuta mke mgine ila usimjengea wala usimuonyeshe mali zako panga umueleza una mke lazima alijue hilo.
5. Watoto wako wasimamie wakileta dharau achana nao watajirudi wenyewe
6. Acha kusimulia watu wanao kujua visa vyako wanakuenjoye tu. Pambana kama mwana umme we only live once here usiogope mahakama au usitawi it will buy time for you to settle huwezi kufungwa kwa civil suite
Da point, big up,
Namba 1, 2 3,4,5, ✅✅✅✅✅
 
Najiuliza mchepuko anawezaje kupata nguvu ya kumpeleka polisi na uku hifadhi kapewa?? Jamaa zuzu
Mbona, umezidisha kutukana,?
Be gentleman,
Tayari nimeshajua udhaifu wangu ndo maana nikatupia huku, najua wengi sana imewaumiza,
Na mpaka hapa sijaona yeyote aliyekuwa upande wa huyo mwanamama,
Hapo ndio nimeelewa kweli sikuwa mimi,

Lakini sasa nimekuwa mimi,

Na ni kweli wakati mwingine masaibu kama haya ukimsimulia mtu unayemfahamu uso kwa uso anaweza kukupa jibu ambalo sio sahihi, akiogopa unaweza kwenda kumsimulia mwenza wako baada ya kuelewana,
Lakini hapa ni makavu tu, hakuna kuremba,
Kwa sababu hakuna cha kupoteza
Nawashukuruni sana
 
Huyu mzee hana akili, ndio wale wahuni waliozeeka na hawana busara wala akili... ajielewi, apambane na maisha yake, awezi kutumia bundle zetu kumbe story ya kitoto hivi? Na yeye anaona kaandika vya msingiii na uzee wake, daaaah kumbe unaweza zeeka na akili hazimo kichwani, sad..
Yaani kwa hili tu, ndio sina akili? Vipi mengine niliyofanya, yote ni ya kipumbavu sio?
Sawa bwana lakini ujue mimi sio malaika!!
 
Mkuu ulikuwa umeinamishwa sio bure..ndele zipo jamani..picha clear ilishaanza kuonekana ikawaje umuongezee pesa tena? Isije ikawa unahitaji msaada wa kiroho pia kuharib hizo ndele..
 
Back
Top Bottom