Huyo mwanasheria aseme nini hujui kwani, umekaa na mwanamke miaka mingi, umeamua kumuacha mlichochuma mnagawana nusu kwa nusu.
Hizo room 30 heri ukajenge sehemu nyingine. Hapo gawaneni uende kwako japo unaonekana king'ang'anizi.
Hakuna sheria ya kugawana nusu kwa nusu Madam, hata kama mmeishi wote miaka mia, kuna mambo mengi sana yanaangaliwa,
Kwa ufahamu wangu mdogo baada ya kupelekana ofisi ya kata, nilikuwa tayari nafahamu nini nitapata, nilikuwa nimepitia juu juu sheria za ndoa kwenye kitabu fulani hivi,
Yule afisa kata anayeshughulika na jamii, moja ya kitu alichosema ndio hicho unachosema wewe, nusu kwa nusu, na alikuwa anasoma kwenye kakitabu Hako hako,
Lakini hakumaliza sentensi yote, nikamwambia endelea kusoma, akakataa akanniambia nisimfundishe kazi,
Lakini mojawapo ya vitu wanavyoangalia ni nani Macha giant zaidi katika ujenzi nani amechangia sana malezi na masomo ya watoto, nani anayesababisha ndoa ivunjike na aina ya makosa vile vile,
Basi alipokataa kumalizia kusoma, nikakasilika na kikao kikavunjika, ndio nikaenda mahakamani
Ingekuwa ni hivyo unavyowaza, mbona watu wangekuwa wanavunja ndoa makusudi ili wagawane kila mmoja aende zake
Hivi unajua kuna ndoa nyingine mtu anaomba mwenzie afe ili aachiwe mali, na kila unaporudi anachukia kukuona bado unadunda,
Sasa kama ni nusu kwa nusu ana haja gani ya kusubiri mpaka ufe,
Na yeye amesubiria miaka 30 ufe lakini hufi,
DUNIA HII MAMA MDOGO IONE HIVYO HIVYO