Naomba Ushauri, Mpangaji wangu 'kaniblock'

Naomba Ushauri, Mpangaji wangu 'kaniblock'

Wengi hua tunajua kodi inaisha mwezi E. Kwa hali yangu ilivyo nitaanza kutafuta kodi mwezi C na D aggressively halafu mwezi E natafuta with luxury ili kulipa mwezi F. Nikiteleza mwezi C basi taarifa nampa mwenye nyumba mwezi huo huo C ili ajue kuna kuchelewa kutakuja.

Ndiyo sababu hua naprefer kupanga nyumba ambayo mshahara wangu mmoja unaweza kucover kodi nzima au angalau robo tatu ya kodi nzima ya miezi 6. Mwendo unakua ni hata majani yataliwa humu ndani ila aibu ya kudaiwa na mwenye nyumba isiifikie familia.
 
Wengi hua tunajua kodi inaisha mwezi E. Kwa hali yangu ilivyo nitaanza kutafuta kodi mwezi C na D aggressively halafu mwezi E natafuta with luxury ili kulipa mwezi F. Nikiteleza mwezi C basi taarifa nampa mwenye nyumba mwezi huo huo C ili ajue kuna kuchelewa kutakuja.

Ndiyo sababu hua naprefer kupanga nyumba ambayo mshahara wangu mmoja unaweza kucover kodi nzima au angalau robo tatu ya kodi nzima ya miezi 6. Mwendo unakua ni hata majani yataliwa humu ndani ila aibu ya kudaiwa na mwenye nyumba isiifikie familia.
MImi nwenye nyumba hata akinikumbusha ile kawaida naonaga soo sana.
Natami asiniambie kabisa kuhusu kodi.
Maana mimi najua na ninakumbuka.
 
Kuna mapungufu kwenye mkataba wako.

Weka/ongeza terms za kuvunja mkataba kwa lazima, moja wapo iwe: mpangaji asipolifa kodi ndani ya mwezi mmoja tokea iishe bila taarifa/ruhusa ya maandishi, mkataba umevunjika.

Pia ni jukumu la mpangaji kukumbuka tarehe za kulipa kodi
 
Wakuu,

Kama Kuna sehemu nmekosea labda mnambie ninyi.

Kuna sehemu nna kibanda Cha wapangaji wanne huwa nakipangisha, Sasa Kutokana na mkataba.

Kila mpangaji ananilipa Kodi yake kutokana na tarehe aliyoingia kwangu, na Kodi huwa napokea kuanzia miezi 6.

Huyu mpangaji alihamia kwangu mwaka JANA mwezi Novemba mwanzoni, Hivyo Kodi yake Kwa miezi 6 ikaisha mwezi APRIL mwanzoni. Hivyo mwezi MEI mwanzoni alipaswa kunilipa tena Kodi Inayofuata. Na nilimtumia sms ya kumkubushia.

Tatizo la huyu mpangaji,
sms yangu ya kumkubushia aliiona Ila akanyamaza kimya, na mwezi MEI Ukaisha bila kupokea hata Senti Moja Wala taarifa yoyote ya dharula toka kwake. Nikanyamaza Kimya.

Ukaanza mwezi JUNI, nikampigia simu, akajifanya kasahau Kama Kodi imeisha na sms zangu hakuziona, Ila akaahidi kua atanilipa mwisho wa mwezi juni.
Nikasema sawa, nisubiri Kodi Yake mwisho WA mwezi juni

Mwisho WA mwezi JUNI ukaisha wote, jamaa Yuko kimya, nikampigia simu zangu hapokei, nilipobadili namba akapokea na akadai shule zimefunga, kwaiyo kwa Sasa amesafiri mkoani ila atanilipa akisharudi JULAI, nikasema sawa.

Jamaa amekuja kurudi mwezi JULAI mwishoni na Kodi yangu akanilipa mwezi AGOSTI mwanzoni. Nami nikienda kwenye daftari langu, nikaandika kua "Leo tarehe 03 AGOSTI, nmepokea Kodi ya mwezi MEI-OKTOBA"

Sasa Baada ya miezi 2 (yaani mwezi OKTOBA) nikamdai tena Kodi ya miezi 6, jamaa akalalamika mbona mapema Sana, mbona katoka kulipia juzi TU Kodi yake ya miezi 6. Namkumbusha kua ile Kodi yake ilipaswa kulipwa mwezi MEI, yeye kaivuta na kuja kuilipa mwezi AGOSTI, ndo maana imekua hivyo.

Basi Jamaa Akadai amenielewa, akasema atanilipa Kodi yangu mwisho WA mwezi oktoba akishapokea mshahara , nikasema sawa. Nikaenda zangu.

Mwisho WA mwezi umefika, jamaa Kimya.Nikajua labda katingwa, na kumkubushia ovyo kodi sio vizuri, nikakaa Kimya mpk mwezi NOVEMBA.

Katikati ya mwezi Novemba ikabidi nimpigie, akawa hapokei simu zangu, nilipobadili namba akapokea na kudai anaelewa, Ila Atalipa mwisho WA mwezi huu huu, zimebaki wiki 2 anaomba nimvumilie. Nikasema sawa.

Mpaka mwezi Novemba umeisha, sijapokea pesa Wala simu yoyote ya jamaa. Ulipoanza mwezi DISEMBA ikabidi nimpigie, Kama kawaida yake hakupokea simu zangu. Ila nilipobadili laini, akapokea na kudai amesafiri mkoani kula sikukuu,kurudi dar Ni Hadi January.

Nikaulizia khs Kodi yangu,akadai ataituma tar. 15 kwenye account yangu ya benki. Nikasema sawa,jitahidi.

Tar 15 imefika, Kimya.
Nikavumilia Hadi tar 20 Nako Kimya. Nimempigia simu zangu hapokei, nilipobadili laini akapokea na kudai tar 22 jioni anaituma, uhakika 100%. Nikasema sawa.

Tar 22 ikapita Kimya, mpaka Jana tar 24 ikabidi nimpigie, nikastuka Kila mara simu yake inadai inatumika Kisha inajikata. Nilipobadili laini, ikaita vizuri TU.Nikagundua kaniblock.

Nilivojitambulisha kua Ni Mimi mwenye nyumba wake, akakata simu ghafla na nilipojaribu kumpigia Tena, ikawa inadai anatumika Kisha inajikata. Nikagundua Hii namba nayo jamaa kaamua kuiblock.

HAPA KIUKWELI WAKUU NMEGHAFIRIKA SANA,

NAWAZA HUYU MPANGAJI SIJAJUA ANANICHUKULIAJE YAANI.

KAMA HAYUKO VZUR NI BORA ASEME MAPEMA AELEWEKE NA SIO KULETA UBABAISHAJI USIO NA KICHWA WALA MIGUU.

KUNIBLOCK NI UTOTO,UJEURI NA UPUUZI ULIOPITILIZA, PIA NI KUNIVUNJIA HESHIMA ILHALI KESHAVUNJA MASHARTI YA MKATABA.

Hapa nafikiria kumuandalia NOTISI Yake, ili January akirudi akatafute pa kuishi. Ila mama watoto kanishauri nisifanye hivo maana huenda Kuna magumu anapitia.

Wazo lake linanipa ukakasi sn maana Kama anapitia magumu, Kuna Sababu gani mpk aniblock zaidi ya kuhisi ananifanyia UJEURI TU.

Plz MNISHAURI pia wakuu🙏.
Wewe jamaa ni mvumilivu sana.
 
Kaka unatafuta pepo? Mtimue nenda mlangoni kwake weka kufuli akija atakutafuta akifika unamtolea vitu njee
 
Ubaya ubaya,tatizo mbongo ukimlegezea kamba anaona tayari anakumudu
Nipe hiyo nyumba niisimamie mimi uone kama hutalipwa kodi kwa wakati
Mda mwingine mwenye nyumba uwe na uso mkavu kama al shaabab
 
Back
Top Bottom