Naomba Ushauri, Mpangaji wangu 'kaniblock'

Wengi hua tunajua kodi inaisha mwezi E. Kwa hali yangu ilivyo nitaanza kutafuta kodi mwezi C na D aggressively halafu mwezi E natafuta with luxury ili kulipa mwezi F. Nikiteleza mwezi C basi taarifa nampa mwenye nyumba mwezi huo huo C ili ajue kuna kuchelewa kutakuja.

Ndiyo sababu hua naprefer kupanga nyumba ambayo mshahara wangu mmoja unaweza kucover kodi nzima au angalau robo tatu ya kodi nzima ya miezi 6. Mwendo unakua ni hata majani yataliwa humu ndani ila aibu ya kudaiwa na mwenye nyumba isiifikie familia.
 
MImi nwenye nyumba hata akinikumbusha ile kawaida naonaga soo sana.
Natami asiniambie kabisa kuhusu kodi.
Maana mimi najua na ninakumbuka.
 
Kuna mapungufu kwenye mkataba wako.

Weka/ongeza terms za kuvunja mkataba kwa lazima, moja wapo iwe: mpangaji asipolifa kodi ndani ya mwezi mmoja tokea iishe bila taarifa/ruhusa ya maandishi, mkataba umevunjika.

Pia ni jukumu la mpangaji kukumbuka tarehe za kulipa kodi
 
Wewe jamaa ni mvumilivu sana.
 
Kaka unatafuta pepo? Mtimue nenda mlangoni kwake weka kufuli akija atakutafuta akifika unamtolea vitu njee
 
Duh mkuu wewe ni mstaarabu sijawah kuona..
 
Ubaya ubaya,tatizo mbongo ukimlegezea kamba anaona tayari anakumudu
Nipe hiyo nyumba niisimamie mimi uone kama hutalipwa kodi kwa wakati
Mda mwingine mwenye nyumba uwe na uso mkavu kama al shaabab
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…