Naomba Ushauri, Mpangaji wangu 'kaniblock'

Plz MNISHAURI pia wakuu🙏.
Wahi kwa mjumbe wa nyumba 10 hao pasua kichwa wapo kila sehemu huku tulimweka mmoja mdangaji mmoja hivi kagoma kulipa mpaka kaja kutolewa na mwenyekiti wa serikali ya mtaa ndio akaondoka kakaa miezi 3 bila kulipa hata 100 umeme anatumia bure maji bure kunya bure kukojoa bure miezi 3 mjumbe alishindwa kesi ikaenda kwa mwenyekiti
 
Ubaya ubaya,tatizo mbongo ukimlegezea kamba anaona tayari anakumudu
Nipe hiyo nyumba niisimamie mimi uone kama hutalipwa kodi kwa wakati
Mda mwingine mwenye nyumba uwe na uso mkavu kama al shaabab
Tatizo la wapangaji ukiwafanyia fujo kesi inahamia kwako unaweza ukaambiwa fidia akae kwako mwaka bila kulipa kodi na kodi zingine zote awe anachukua yeye mwaka mzima km faini, usijaribu kugombana na hao pasua kichwa wana hesabu zao kichwani ukibugi tu unamlipa
 
Unampeleka kisheria,yaani kama inatakiwa alipe kodi tarehe 5 na ww unakaza hapo hapo
 
Mpe notes kwanza ,baada ya miezi mitatu umuondoe
 
Kudeal na hii kitu ni very simple.
Fanya haya.

Kata huduma zote muhimu katika nyumba (mfano Maji, umeme, usalama), nenda na fundi ondoa switch zote, koki zote na vitasa vyote, sema unafanya marekebisho ni vibovu.....

Pili mwambie akulipe pesa zako ndani ya wiki moja na kisha ahame. Baada ya wiki piga kufuli nyumba yako kama hajakulipa.
 
Achana na mambo ya mama watoto mpe notisi aondoke,usipende kumpangisha mpangaji msumbufu hawezi kubadilika hata siku moja,kama hawezi kuishi mjini arudi kijijini kwao.
 
Mkuu huyo jamaa namtamaani 😬😬😬😬

Mimi huwa naVIBE na BEAT unalokuja nalo yaani ukinileta usela mavi mimi unakuwa umewachokoza WADUDU KWENYE HILI FUVU langu lazima nikushughulikie kiulalo ulalo, bastardo gardembich bladiful😎

Huyo ashakuzarau cha kufanya acha kujifanya wewe ni yesu au upo hapo duniani uungue kama mshumaa ili wengine wapate mwanga.Hii dunia ni katili sana hasa kwenye hiki kipindi cha KIBEPARI.

Yaani huyo akikulipa baada ya siku tatu mpe notice atoke unaka kurekebisha nyumba. Acha kulea ujinga, biashara ya nyumba inareturn ndogo sana alafu bado mtu anakuletea utoto😬😬😬😬

Mimi ningemfanyia ukatili asingesahau nyambafu!!!Huo muda wa kubembelezana unautoa wapi huyo mpuuzi mmoja anakupotezea muda mpe notice achape lapa!!!!

Rekebisha mkataba, weka kipengele cha kodi ikizidi wiki mbili baada ya kuisha uwe unahaki ya kufukuza!
 
Wewe hao hoehae hawana hata pesa ya wakili wala wasikuumize kichwa.
 
Sijakublock baba mwenye nyumba, we nisubiri January nikirudi. siyo mpaka tuanikane humu. Sahv sikukuu mambo mengi, ikishindikana basi toa nyumba yako kwenye vitu vyangu
 
Bila shaka wewe ndiye mpangaji tajwa. Unaonekana una jeuri sana kwa mwenye nyumba wako😀😀😀
Acha usumbufu, kwanini umtafute siku za siku kuu? Subiri atapatikana baadaye tu.
 
mvumilie tu pengine kuna magumu anapitia kweli kama mke wako alivokushauri.
Angekua wa kuhama huyo angehama hata usiku kwa usiku. Vumilia tu atakupa pesa yako
 
Naomba nije kupanga kwako,ulikuwa unamdai kistaarabi sana ndomaana amekuchezea
 
Andaa notisi ,timua hilo jing.
Hiyo ni dharau ,kibri na anajihisi anakuweza ,embu fukuza Mara moja huyo mtu
 
Mzee umemlea sana aisee. Cku hiz sio kama zaman mzee, huyo kuna namna ya kumtoa kwa kustukiza, kuna mturuki mmoja alikuwaga kwenye apartment yangu akaniletea huo mchezo. Alikula jeuri yake. Nilimchomoa usiku akiwa amelala. Hela hazitafutwi kilekole mzee pinduka kama walivyopinduka watawala wako utakula mema ya nchi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…