Naomba Ushauri, Mpangaji wangu 'kaniblock'

Kama kuna jambo sipendi na anogopa ni kudaiwa kodi. Mimi huwa nina tabia ya kulipa kodi mwezi mmoja kabla ya kuisha. Napoishi kodi hulipwa january tarehe 1 na july tarehe moja kwa wapangaji wote.
Hapa kabla ya christmas nishamalizana na mwenye nyumba tutakutana tena july napo nitajitahidi nimalizane naye mapema.
Ukiwa waishi kwenye nyumba ya mtu kuwa mstaarabu kama kujenga ni rahisi mtu angejenga yake.
 
Nikweli mkuu
 
Notice ya pango ni miezi mitatu (3) tu yaani mpangaji kukaa bure akijiandaa kuhama, kwa hiyo huyo tayari keshajipa notice.

Akirudi mburuze kwa mwenyekiti S/M kudai haki yako aliyokaa ziada ya miezi mitatu ya notice na kumtaka ahame bila wewe kutoa visingizio.

Hapo kubali hasara ndogo kuliko kuendelea kufuga hicho kirusi.

Mpangaji yeyote mwenye mkwamo, hufunguka mwenyewe mapema kwa mwenye nyumba akiwa tayari kapiga hesabu zake ni mwezi gani atakuwa tayari kulipa na ukifika mwezi huo lazima alipe na siyo kusongesha blah blah zake tena.

Wapangaji aina hiyo siyo wazuri, umesoma kwenye mitandao issue ya Kawe, hadi Mbunge Gwajima kulivalia njuga?

Nyumba ya mamillioni imeuzwa na mpangaji, kisa kilo 38 za nyama na mwenye nyumba kubaki analalamika asijue aanzie wapi.

Baadaye akiisha kukuzoea sawasawa, mtaingia naye kwenye migogoro ya kupotezeana muda mahakamani na ukimhurumia lazima itakula kwako tu, mimi nina uzoefu sana na mambo hayo, kubali hasara hiyo ya kodi ya miezi mitatu kisha fukuza.
 
Ukiwa na roho nzuri sana na huruma zikizidi binadamu watakupanda kichwani hatimae kukung'ofoa nywele mpaka ubaki kipara.

Timua huyo mpangaji mkuu, umeonesha uungwana wako na ustaarabu ila kwa bahati mbaya mtendewa yeye hahitaji kufanyiwa hizo taratibu ulizo jaribu kumfanyia kiubinadamu.

Huruma sio malezi kqbisa timua huyo tapeli hapo kwako aisee! Haina haja ya kusubiri january mpigie simu aje atoe vitu vyake fasta usifanye makosa kabisa kumbakiza huyo mtu hapo kwako.

Hallelujah!!!
 
Na January inavyokuwa kavu, unasubirishwa mpaka mwisho wa February. Sasa hapo utajikuta mshavuruga mpangilio wa miezi ya kulipa. Kama vipi badili kitasa ila awepo Mwenyekiti wa Mtaa
Hapana asifanye hilo zoezi bila ya mwenye chumba kuwepo.

Amsubiri mpangaji wake arejee kisha ampeleke kwa mwenyekiti, kudai pesa ya pango iliyozidi miezi mitatu ya notice, kisha ampe masaa 24 kuondoka, kwa sababu alishajipa notice mwenyewe kwa kushindwa kulipa kodi zaidi ya miezi mitatu kwa makusudi.

Akishindwa kulipa hiyo hela pamoja na kuhama, ndiyo achukue hatua zaidi atakazoona zinafaa.
 
Ukiwa na huruma watakaa bure we siku waibukie ukiwa na watu wawil waambie nyumba ndo hii chumba kipo huyu anahama mwez ujao walipie kodi
 
Kuna mmoja kang’ang’ania nyumba ya upangaji kesharipotiwa lakin hatoki kuna watu wana roho ngumu
 
Kuna mmoja kang’ang’ania nyumba ya upangaji kesharipotiwa lakin hatoki kuna watu wana roho ngumu
Yaani mwenye nyumba anakosa mbinu za kumfukuza kisheria, hiii imekaaje hii!

Akishakaa bure miezi mitatu ni notice hiyo kajipa, anafukuzwa hata kwa fujo ya kutupiwa mizigo yake nje.

Kikubwa kila hatua ni lazima awepo kiongozi wa serikali ya mtaa.
 
Wapangaji ni changamoto jamaniii tena wengi wakorofi kulipa kodi huwa wanafanya makusudi wakitegemea Notisi,Hapo pesa ya kuhama kwako anayo si ya kukulipa deni.
Ww hujawahi kupanga au ndio maskin akipata
 
Vumilia yote lakini sio dharau. Huyo analeta dharau sasa. Wife anafanya maamuzi kwa hisia wee fanya kwa kutumia akili
 
Pole sana mkuu. Mimi wapangaji wangu wakizingua tu kulipa kodi nampa notice ya siku saba awe tayari amenikabidhi funguo za nyumba, na pia nyumba aiache ikiwa na hali ya usafi kama siku anaingia.

Pili bill ya maji ni shared kwa kila apartment block, hivyo ikitokea mpangaji anazingua tu kulipa bill ya maji na yeye notice inamhusu kwa sababu siwezi sababisha usumbufu kwa wapangaji wengine kwa ajili ya mzembe mmoja.

Kwa wapangaji huwa sitaki mzahaa na FEDHA yangu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…