Kwanza kabisa,inategemea na wewe unapenda gari aina gani. Af, kwa nini unanunua gari? Bro,usijichaanganye,gari ni kama malaya unayemhudumia wewe. Pesa unayotumia inaondoka hairudi. Kama huna vyanzo vingine vya kuihudumia,utalia.
Pili,uwezo wako unakuruhusu?
Tatu,kumbuka unachukua gari lililotumika. Ila kwa sababu unataka gari,ukiliona utanunua tu.
Nne, mafundi hawajakuibia. Nawatukana wanisamehe kama humu wamo. Ila wale ndo watoto wa mbwa halisi kama hujui
Tano, Je, bajeti yako inatosha kukava imajensi(ulaji wa mafuta,matengenezo,kuiweka katika hali unayotaka)? Kama unataka la M18, angalau tenga 10 nyingine.
Ni kweli maendeleo ni gharama. Mi nakushauri uanzie kigari cha bei ndogo,kikupe uzoefu,ukitunze,ukishajiweka sawa,utakiuza uongezee uchukue la ndoto yako.