Naomba ushauri na mapendekezo kuhusu Suzuki Escudo old

Naomba ushauri na mapendekezo kuhusu Suzuki Escudo old

Chukua escudo ,gari nzuri sn niliuza ya Kwanza nikanunua tena nyingine, Ila Kwa budget yako ni ndogo at least ungefika M 10 utapata nzuri
 
Wakuu habari ya muda huu,

Nimekuja mbele yenu nipate ushauri na mapendekezo zaidi kuhusiana na gari aina ya Suzuki Escudo old model.

Mimi napiga sana mihangaiko ya vijijini mashambani ambako ni 100% rough road. Kulingana na mazingira hayo nilitamani gari yenye spec zifuatazo;



Sasa kulingana na vigezo hivyo nikawaza Suzuki Escudo old model maana naskia zina ulaji mzuri wa mafuta naskia zinafika hadi 12km/l, pia nasikia 4WD yake ni balaa. Japo nasikia zina changamoto ya bodi kuingiza vumbi ndani. Nina mpango wa kuchukua mkononi na bajeti yangu ni 6m max.

Awali niliwaza kuhusu Rav4 old, changamoto ikawa ni ulaji wa mafuta maana naona nyingi zinaenda 7km/l sasa kwa mizunguko yangu nikaona haitanifaa japo sifa nyingine inazo.

Naombeni ushauri wenu kama nipo sahihi kwa chaguo hilo na kama kweli escudo old ina sifa hizo na pia kama kuna mbadala tofauti na hiyo escudo old kwa bajeti hiyo ya 6m mkononi. Asanteni.
Alokudanganya RAV4 inakula hivo ni nani? 12-14km/l inapiga mkuu. Ni uwezo wako ukiichukua uiweke sawa
 
Tubaki kwenye mada,
Chukua G16 hutojutia. Natamani niipost yangu ila wataijua maana nafikaga nayo hadi masaki na oysterbay.😂😂.
Chukua chuma hiyo. Ila acha nipost hata engine tu.. inatia nyege sana gari hii hata nikitaka kwenda mkoa.
 

Attachments

  • 7882E663-BA27-4486-9E59-2166F8B7AEB2.jpeg
    7882E663-BA27-4486-9E59-2166F8B7AEB2.jpeg
    50.5 KB · Views: 61
mkuu hongera naona umejitahidi kuitunza, vipi ulaji wake wa mafuta
 
Nifanye nini iweze kula wese hivyo mimi nina gari hiyo na namba ni D
Nifanye nini iweze kula wese hivyo mimi nina gari hiyo na namba ni D
Kwanza,haikisha unamtumia fundi mzoefu,ukiogopa gharama,utalia. Japo unatakiwa ujue kinatengenezwa kitu gani.
1. Fuel pump yako ina hali gani?
2. Kwa sasa,ulaji wake umekaaje?
3. Spark plugs unazotumia zikoje?! Unaweza itoa utuonyeshe!
4. Engine yako ina hali nzuri(kama ilibadilishwa)
5. Uliagiza,au ulichukua kwa mtu!
6. Unajua lakini pia kuwa fuel tank yake ina chamber? Kwa maana mafuta yakikata si kwamba yanakuwa yameishamo!
 
Halafu nissan patrol sio hevy duty kama hiyo escudo , ni kama landrover tu zinataka matengenezo sana hasa kama utazitumia kwenye rough road
Duh.yani uifananishe N.Patrol/N.Safari na LR kweli?
Kwa Nissan ataingia gharama sababu ya spea kua ghali na adimu kwa baadhi ya mikoa ila kwa wenzetu kenya wanazo zakutosha maana wanatumia sana nissan.
Offroad zinakata shimo haswa bila kuhitaji matengenezo ya kila mara kama LR yenye ma-leakages zikitokaga rough roads!

spea gharama ila ukifunga umefunga!
 
Back
Top Bottom