Naomba ushauri, nijenge au ninunue nyumba

Naomba ushauri, nijenge au ninunue nyumba

Faida za Kujenga nyumba mwenyewe;
•Unajenga nyumba ya ndoto yako, kuanzia design hadi mpangilio wa muonekano wa mwisho wa nyumba yako.

•Utakuwa mlipaji wa mwisho wa Kila kifaa utakachonunua kwaajili ya ujenzi, hivyo una nafasi ya ku-save kiasi Fulani cha fedha.
•Utakuwa na nafasi nzuri ya kujenga Kwa vifaa vya Kisasa zaidi kadri utakavyoona na kushauriana na Mafundi. Vifaa vya Umeme vilivyo tumika kwenye Ujenzi wa nyumba Mwaka 2000 haviwezi kuwa sawa na Vifaa vya Umeme utakavyonunua utakapojenga Mwaka 2024 interms of technology.

Faida za Kununua nyumba;
•Inaokoa muda, unalipia nyumba Leo, keshokutwa unaweza kuhamia

•Inapunguza gharama, nyumba unayoweza kujenga Kwa shilingi milioni 100, unaweza kununua Kwa milioni 75, kutegemeana na uwezo wa ushawishi. Zone of Possible Agreement (ZOPA) wale tulio na skills za Negotiations

Maamuzi ni yako Chifu, Wishing you best of luck
 
Unakisia sana, mkuu. Kuna wengine wanaweza kupata mali za urithi. Au akajizolea Tatu Mzuka ama Biko! Haiwezekani?

Ushauri wangu ni kwamba anunue nyumba wakati huohuo akijenga; vyote viende sambamba. Inawezekana kabisa.

Akimaliza kujenga, anaweza kuamua kuiuza hiyo nyingine.

Naona unajua mpaka ana shillings ngapi mkononi ili anunue na kujenga kwa wakati mmoja?!
 
Naona unajua mpaka ana shillings ngapi mkononi ili anunue na kujenga kwa wakati mmoja?!
Maadam kasema anataka kujenga, tayari huo ni mwanzo mzuri. Suala la kiwango cha fedha alicho nacho mkononi, hilo tumwachie yeye mwenyewe.

Lakini mtu anaweza kujenga nyumba yake, wakati huohuo amenunua nyumba bora ya kupitishia siku, miezi au miaka kadhaa wakati akingoja kukamilika kwa jengo lake.
 
Raha ya kujenga ni moja, unajenda dizaini uitakayo
 
Jenga yako mkuu,

Ukitaka design bora, usisite kupitia uzi huu mkuu

 
Ina tegemea zipo za kununua na zimenyooka sana ila bei cheap kutokana na gharama za uenzi za zamani kuwa ndongo kulinganisha na sasa. Mfuko wako tu unanunua nyumba unaiongezea udambwi inakua kali zaidi.

Kama unataka nyumba ya idea zako mwenyewe jenga yako isimamie mwenyewe usitake utitiri wa mafundi au kusimamiwa ujenzi wengi sio waaminifu.

Wananunua watu maghorofa kkoo sembuse kununua nyumba swekeni. Kikubwa know what you want and zingatia taratibu sahihi za manunuzi usije mwaga kilio. Jitahdi uwajue wamiliki first hand….ukishasikia nyumba ni ya urithi kaa attention ama kimbia meter 800.
Umenena vema kabisa chief.
 
Blaza nishaona watu wakiingia kwenye majanga kama hayo hata kwa kuangalia kikubwa ni kupotezewa muda na fedha kutokana na migogoro iwe ya muuzaji mwenyewe au migogoro ya warithi.

Inshort wauzaji anza kuwapekua kuanzia ngazi ya majirani, mjumbe wa nyumba 10, M/Kiti Serikali Ya Mtaa, Mtendaji Kata, Manispaa mpaka verification kutoka Ardhi na maelezo yote utapopita huko yawe sawa sawia (parallel). Kote huko unapopita omba historia ya eneo husika ukweli utaujua tu. Usipuuze hata doubt moja ya maneno mawili.

Mwisho weka legal papers za maana hakikisha wanaopokea hela yako hawachomoki wakizenugua una watia ndani.

Kikubwa Ni Kuepuka Kupotezewa Fedha Na Muda. All The Best [emoji817].
Mjombav wangu alinunua nyumba mwaka karibia wa 10 ni mogogoro tu mkuu anavyosema peleleza kwa kina.

Rafiki yangu aliuziwa kiwanja mil 9 kumbe yule mama sio msimamizi wa mirathi ya mume wake case ipo mahakamani ina inahitaji kuchunguza sana kuna utapeli mkubwa sana kwenye sector ya ardhi na nyumba
 
Back
Top Bottom