Naomba ushauri: Nimdhamini au niachane naye?

Naomba ushauri: Nimdhamini au niachane naye?

Ni mtu ambaye miaka 10 tulikutana katika harakati za utafutaji kazi. Tukapoteana tulionana mjini Dar mwaka jana.
Mwaka jana kibarua chake kiliota nyasi. Si unajua sekta binafsi mistake ndogo tu wanapita na wewe.

Familia ina hitaji kula, umri umeenda kahangahika kaamua aende kampuni ya Uzinzi Garda security. Huko kapata ila issue ni udhamini kawekewa vigezo vigumu.

Wanataka apeleke watumishi wa umma 2 wenye barua za mkono, picha, kopi ya NIDA, kopi ya kitambulisho cha kazi na barua zao za utambulisho kutoka serikali ya mtaa.

Kasema kupambana kutafuta wadhamini kachemka, anaomba msaada wangu hana namna. Sijui kama mdhamini mwingine kampata au ndo anataka aanze na Mimi.

Vipi wakuu nimdhamini, au nimwambie kuwa haiwezekani. Na kama namdhamini nimpe masharti yapi Ili kujihakikishia usalama wangu?

Thanks.
Hiyo kampuni ya uzinzi na mimi naitaka kama kazi, ni uzinzi tu nika chague pisi nijilie taratibu huku nalipwa na mshahara.
 
Back
Top Bottom