Cement 200 utauza vip upate faida wakat Kuna wenzio jiran wanaleta lori Zima la cement,hapo kwa hiyo Hela ajikite zaid kwenye vifaa vidogo vidogo vya ujenz na mifumo ya maji taka na safi
Kwa akili hizi umewahi kufanya biashara yoyote? Kwahiyo kisa jirani kaleta lori la cement yeye akianza na mifuko 200 itamzuia kupata faida? Ingekua ni hivyo hata hao wanaoleta tani nzima wasingeweza kufikia hiyo hatua ya kuleta gari nzima, au unafikiri walianzia hapo unapowaona?
Million 25 anaanzisha biashada nzuri ya hardware na anapiga pesa na faida anapata nzuri tu
Kwa kuanzia anaweza kuanza na Mifuko ya cement 100-200
Vifaa vingine kama Misumari, binding wires, Bomba na fittings za maji,
Nyundo, plaizi
Vifaa vya umeme auze hapohapo kama bulbs, Sockets, switches, rangi kidogo na brush.
Vifaa vya mafundi kama makoleo, pima maji, kamba vyote anaweza kuvitapa kwa mtaji huo wa 25M baada ya kutoa gharama za leseni ya biashara na kulipia kodi ilimradi tu biashara aifungue maeneo yanayoanza ujenzi
Ila kama una akili za kuwaza kubeti utaendelea kuuliza hayo maswali yako ya atapataje faida kwa kuuza mifuko 200 wakati wenzake wanaleta lori