Naomba ushauri: Rafiki yangu ana tabia ya kutongoza kila binti ninayekuwa naye kwenye mahusiano

Naomba ushauri: Rafiki yangu ana tabia ya kutongoza kila binti ninayekuwa naye kwenye mahusiano

Punguza ukaribu na huyo unayemuita rafiki yako. Hama kwenye nyumba za kampuni uende mbali na hapo ili uwe na privacy kwenye mambo yako. Si vema kila kitu unachofanya umshirikishe rafiki yako, vingine vibaki kuwa suprise, aone matokeo tu hata kama akilaumu kuwa haukumwambia.
 
Kamwe ni nadra wanaume kuwa na urafiki wa hivyo never never huyo si rafiki ni mjinga mjinga uliye kutana nae ukubwani
 
Ujue Kuna baadhi ya watu ukuaji wao ni wa kuongezeka idadi ya miaka tu lakini akili imeganda palepale
 
Habari mwanaJF,

Naomba ushauri rafiki yangu huwa na tabia ya kutongoza kila binti niliye naye kwenye mahusiano.

Ni rafiki ninayefanya naye kazi kituo kimoja pia tulikutana kazi japo pia tunakaa jirani kwenye nyumba za kampuni.

Kipindi cha nyuma nilikuwa na demu ambaye alimjua pia baadhi ya mambo alikuwa anajua coz ni rafiki yuko karibu na mimi ila nilipokuja kujua kuwa amemtongoza pia kala mzigo, nilijikuta hisia zinaisha kabisa na yule demu nilimpenda ila sijui kama na yeye alinipenda kwa mara ya mwisho alikuja gheto kwangu sikuweza kufanya chochote, niliachana naye pia sikumwambia kitu rafiki ila nilianza kuweka mipaka.

Niliingia tena na mahusiano binti mwingine, hali ilirudi ile ile ila cha ajabu huwa anajifanya kunipa ushauri na kuniambia usimuache huyu demu anakupenda sana ila nilijikuta namuacha kwani nilishindwa kufanya naye sex zaidi ya mara mbili.

Sasa juzi nikiwa na binti niliyenaye kwa sasa, rafiki yangu alinipigia simu akiniomba nimuazime pikipiki, nilimwambia nimeenda kijijini ila haikuwa ni kweli nilikuwa out na mpenzi wangu, sasa nilishangaa nilipooneshwa sms aliyomtumia mpenzi wangu wakati huo nikiwa naye ila kwa kipindi cha nyuma aliniambia kuwa jamaa anamsumbua.

Nilichati naye na nikamuomba 20,000/=, cha ajabu aliniomba nimuazime 30,000/= baada ya kumtumia alituma kwenye namba ya mpenzi wangu, nilijikuta naumia na kujaa hasira sana.

Naomba ushauri maana huyu binti nampenda sana pia nimeshafika kwao nahitaji kumuoa , nifanyeje ili yasinikute yaliyopita? Maana rafiki yangu najua tabia zake ana madem wengi pia huwa ananunua wale dada poa.

Naombeni ushauri maana kila nikikumbuka najaa na hasira.
Huna rafiki na pia huna wapenzi. Hao wote ni vichaa wanakufanya buzi lao
 
Back
Top Bottom