Naomba ushauri tafadhali

Nijuacho mimi hapo ni nguvu za giza na maagano ya ufalme wa giza,maisha yetu tunayo ishi huwa yana anzia rohoni.ninakushauri OKOKA mkuu,wokovu sio dini mpya ni kumkiri YESU kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yako.ww ndio unajua namna gani unaumia na hayo maumivu humu ndani hayupo wa kukusaidia kwa kiasi ambacho utapata raha nafsini mwako zaidi ya Damu ya Yesu inenayo mema na iliyo lipa gharama ya hayo yote.karibu kwenye ulimwengu wa nuru
 
Shekh, nimeangaika mnoo kwa maustadha bado shida inaendelea.
Nasikiza saaana Quran na kuswali pia.
Nimeenda miskiti kuomba dua, kilichotokea, narudi tu nalopokewa na mke kwamba namswalia kabla hajafa misikitini
Huko unateseka mwamini Yesu mwana wa Mungu ,utaokoka.
 
Shukran Sana umemuwaidhi ipasavyo ...
Asichanganye dua na shirki ...usiruke ruke ndugu tawakal kwa Allaah..
 
Kama ni muslim fanya dua sana either mwenyewe au kushirikisha watu wanaoweza kufanya dua...zoezi hili liendane sambamba na kutoa sadaka kwenye vituo vya watoto yatima au nyumba za ibada..

Kama ni christian, fanya maombi toa sadaka...jpili nenda kanisani...

Dunia ina mambo sana magumu na mepesi pia..chukulia huo ni mtihani kama wengine unavyowaona wana mitihani..

InshaAllah Mungu ni mwema atakufanyia wepesi..
 
Yesu ni njia na uzima.
Mimi naweza kukusaidia, lakini Nimeokoka
 
Mkuu pole Sana sana mpk nmeogopa sana. Na nmejaribu kuvaa viatu vyako hakika vmenipwaya Sana uwenda ningekimbia familia.
Sasa hapo kuna maagano ya kiukoo yanakufatilia paspo ww kujua kuna viapo viliapwa huko zamani na kafala kutolewa uwenda ww umekiuka baadhi ya Mambo
Utateseka Sana bro hayo maagano ya ukoo lazma ujitenge nayo haraka sana.
Raia humu huwa wanambeza Sana mwamposa bt hakika kuptia jina la Yesu amesaidia wengi Sana.
Ungekuwa upo kanda ya ziwa huku ningekuja huko na rafiki yangu tuchape maombi hapo tuvunje hayo maagano hakuna kingebaki kukusumbua usje sema twataka hela au sadaka hapana yaani ni nauli Tu basi. Tungekuonyesha uwezo WA Jina na Damu ya Yesu hayo madude yangesema yanatoka wapi Amini usiamini
 
Nashukuru saaana, nimezingatia
 
Pole sana mkuu,

Upo mkoa gani?
Wake zako wote wanaonyesha dalili za magonjwa ya akili, usipokuwa makini hata huyo wa sasa naye siku si nyingi atachizika,


Jaribu kwenda Muhimbili au Mirembe ukawaome wataalam.
 
Shekh, nimeangaika mnoo kwa maustadha bado shida inaendelea.
Nasikiza saaana Quran na kuswali pia.
Nimeenda miskiti kuomba dua, kilichotokea, narudi tu nalopokewa na mke kwamba namswalia kabla hajafa misikitini
tatizo unaswali kwasababu ya matatizo ndo shida..
 
1996+9=2005, wewe uliongeza mke 2003.

Pole sana, muombe Mungu atakusaidia hakika.
 
Pole sana mkuu ..matatizo ni mengi sana kwenye hii dunia. Muombe sana Mungu akuokoe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…