Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kuwa na Imani thabit na usiwe mtu wa kujaribu kila aina ya mambo
Mwamini Mungu wako sana na uswali na kumlilia sana Mungu
Kuna tatizo kwako ila hujasema upande wa familia yako wakoje
Je umeiliza nyumbani
Nimefika kwa kuchelewa kidogo my apology
Pole sana sana hii ina uhusiano mkubwa sana na ushirikina uliofanyiwa wewe kwa familia yako...Salaaam.
Nimekuwa na changamoto katika maisha yangu na familia yangu.
1. Nilikuwa nimeowa mke wa kwanza 1996 na kubahati kuishi kwa miaka 9 ivi na kupata watoto 3. Lakini, ikaja changamoto mke akawa ananishutumu kuwa nawatuma watu wamzalilishe, akawa anakosa amani aliamini kuwa nawatuma watu wamchungulie Hadi chooni/bafuni na hata tunapolala. Nikamuacha kwa kuamini alikuwa analengo lake. Lakini baada ya kuachiwa Hali yake ikawa mbaya zaidi na kuwa mtu aliechanganyikiwa.
2. Nikaowa Tena 2003, lakini baada ya miaka Kama Saba Hali ya yule mke wa kwanza ikajitokeza kwa huyu na kupelekea kukosa Furaha ya ndoa. Amekuwa anasikia na kusema Mambo ambayo wengine tunashangaa tu na ngumu kuamini. Anaweza kuwa ndani lakini akakuambia watu wanamzomea au wanamtuka nje bila wengine kusikia
Mbaya zaidi kunasiku akaamka na kuniambia kuwa ameota kuwa na jitu kubwa na lilimwambia yeye ni mkubwa na aniambie nimwaache. Baada ya mwezi, anadai kuachwa. Naogopa kumwacha kwakuhofia lile la mke wa awali.
3. Wakati napambana na Hilo, mwaka juzi mtotowangu alitoka nyumbani nilikozaliwa na kuanguka na pikipiki na lakini hakuumia sehemu yoyote ile lakini alisema alishangaaa tu ameanguka na hakuwa anajielewa na kujikuta tu anaburuza pikipiki kwa mda mrefu na baada ya kupata fahamu akawasha na kurudi nyumbani anakoishi. Toka siku hiyo akawa anaongea Mambo ambayo ni ngumu kuelewa, atoki ndani mchana na kuchukia kuwa karibu na watu.
Naomba Allah akuongoze kunishauri Hilo maana linanikosesha amani. Naomba saana kwa Allah Ila nakosa maarifa ya kutafakari ndoto zangu.
Bahati mbaya wazazi walishafariki kabla ya kumaliza shule ya msingi. Hata hivyo, nimewauliza Kaka na dada zangu, pia wajomba na mashangazi na wakubwa wa ukoo kupata histori yetu, bla kupata msingi wa matatizo yangu.Pole sana sana hii ina uhusiano mkubwa sana na ushirikina uliofanyiwa wewe kwa familia yako...
Je kuna mtu aliwahi kujiapiza kukufanyia mabaya?
Je kuna ndugu mlitofautiana mambo ya kifamilia?
Je kuna mwanamke ulishawahi kudate naye ukamuahidi ndoa na hukumuoa?
Tiba halisi ni pale utakapojua chanzo cha tatizo ama asili yake
Vipi kuhusu mahusiano yako ya nyuma? Hujawahi kuharibu mahali?Bahati mbaya wazazi walishafariki kabla ya kumaliza shule ya msingi. Hata hivyo, nimewauliza Kaka na dada zangu, pia wajomba na mashangazi na wakubwa wa ukoo kupata histori yetu, bla kupata msingi wa matatizo yangu.
Dada yetu aliniambia nimezaliwa baada ya watoto Kama watatu kufariki wachanga na kupelekea maneno mengi Kati ya baba, mama na wazee wao na nikapewa jina la utoto Maneno
Funguka kidogo mwisho ulikuwajeWakati nasoma chuo nilizaa na bint mmoja.
Nilikwenda likizo home kabisa, kijijini, katika kaa yangu huko, nikalala nae na kurudi shule bila kujuwa Kama Ana ujauzito. Nilikaa mda mwingi kurudi huko na sikupata taarifa yoyote kuhusu Hilo. Ndugu zangu pia hawakunipa taarifa hiyo. Lakini baada ya mtoto kuzaliwa na kuendelea kukuwa DNN Za kienyeji zilithibiti kuwa ni wangu. Nilipomuuliza binti Kama Jambo Hilo ni sahihi alisema ndio na alitoa taarifa kwa dada mkubwa lakini dada zangu walilikataa.Funguka kidogo mwisho ulikuwaje