Naomba ushauri wa biashara ya kuingiza 50,000 kwa siku

Naomba ushauri wa biashara ya kuingiza 50,000 kwa siku

Ama kweli mswahili ni mswahili tu!
Sasa kama unakunja 70,000/= kwa mtaji wako wa laki 3, si umpe mawazo mwenzako anahitaji msaada wa kimawazo kuhusu biashara ya million 3-4.
Au ndio unataka kusifiwa kwamba wewe una akili nyingi kuliko mwenzio.!?
Kuna mswahili mwengine huko juu kasema mtaji wa 50,000 anapata faida ya 150,000 kwa siku.

Yaani faida ni 3 times ya margin. Yaani ilimradi tu mtu akomment aonekane yeye kiboko kuliko wengine. [emoji23]
 
Bodaboda wa darisalama akiona hii comment ataona anapoteza muda huko alipo [emoji23][emoji23][emoji23]
wapi huko mbona hamna hela, kuna chimbo huku mkoani watu wanakunja hadi laki 3 kwa siku
 
Ni sawa mkuu, lakini eneo lililochangamka, bar iliyochangamka manake hata gharama za uendeshaji ziko juu.

Biashara ya kukupa 70k baada ya kuondoa gharama zote sio mchezo mkuu.
Sikia ndugu.
Jamaa alichoongea mimi nimemuelewa vizuri sana.
Kuna baadhi ya biashara ambazo ukiziangalia kwa juu juu unaweza ukazidharau ila zina faida kubwa sana.
Mimi kuna Sister wangu alikuwa anafanya hiyo biashara ya kukaanga kuku tu peke yake kwa mtaji wa Laki 1 tu na alikuwa anapata faida ya elfu 30 kila siku.
Sasa ukiweka mtaji wa laki 4 kwa nini elfu 70 isipatikane?
Sasa piga hesabu mtu anayeuza chipsi na kuku kwa pamoja inakuwaje.
Na anaposema kwenye eneo lililochangamka sio lazima bar ila kwenye eneo lolote lenye muingiliano wa watu wengi kama karibu na sokoni,stendi,eneo la viwandani,magereji,karibu na vyuo,shule unaweza kujenga banda lako ukawa unamlipa hela kidogo mwenye eneo au unakodi fremu ya elfu 50 hadi laki 1.
Na hata ukichukua jiko sehemu ya bar ukalipia laki 1 kwa mwezi haina hasara hiyo ni faida ya siku 1 tu.
 
Ni sawa mkuu, lakini eneo lililochangamka, bar iliyochangamka manake hata gharama za uendeshaji ziko juu.

Biashara ya kukupa 70k baada ya kuondoa gharama zote sio mchezo mkuu.
Zipo nyingi tu sema watu huwa wanakula pesa kimya kimya,watu wakiziona hizo biashara wanazidharau kumbe ndizo zenye hela.
 
samahan boss .. nulikua nahitaji kufahamu zaidi kuhusu biashara ya kuuza compyuta pamoja na simu katika duka moja. ila nahitaji kupewa ata mwanga kuhusu iyo biashara katika vipengele vifuatavyo
1. kiasi cha mtaji kinachofaa kuanzia biashara hiyo
2. mkoa au eneo linalofaa kwa hiyo biasahara
3. Eneo la kupata mzigo.
na vitu vingine naomba unielekeze tu nduguydngu kama utakua naufaham kuhusu ilo ndugu
 
1679648631864.png
 
Uza shorts utatumia mtaji wa milioni 1 tu ila utaweza kulaza 30-50 ila kwa kazi ngumu sana Mkuu na nongwa hazitakosekana ila ukikomaa utaweza.

Unauza kama wauza kahawa tu, ni wewe na machimbo unawapelekea wadau ulevi kijiweni tu. K Vant, Diamond, Konyagi, Hanson Choice, ba vidude vingine ilimradi ulevi tu.

Kwenye kila chupa kubwa ukosi 2500 ni wewe tu kuchangamka.

Ila ni kazi ngumu sio masihara.

Biashara ya kuingiza 50000 kwa siku kama ni biashara yenye ofisi juamtaji hapo sio chini ya milioni 5+. Ila biashara za kutembea ndio unaweza ingiza iyo faida au kuikaribia kwa mtaji mdogo wa milioni 1-3
0713491359
Naomba ufafanuzi wa hii
 
Asante kwa kuuliza. Kuna biashara nyingi unazoweza kuanza na mtaji wa kuanzia milioni 3-4 ambazo zinaweza kukuingizia kiasi cha kuanzia elfu 30 mpaka elfu 50 kwa siku. Hapa chini ni baadhi ya biashara ambazo unaweza kuzingatia:

1. Biashara ya chakula: Unaweza kuanzisha biashara ya kuuza chakula kama vile mboga, matunda, na vyakula vya kukaanga. Unaweza kuuza kwa njia ya mkononi au kuanzisha duka la kuuza vyakula. Kwa kuanza unaweza kutumia mtaji wako kwa kununua vifaa vya kupikia na usambazaji wa bidhaa.

2. Biashara ya kuuza nguo: Unaweza kuanzisha biashara ya kuuza nguo kwa njia ya mtandaoni au kuanzisha duka la kuuza nguo. Unaweza kuanza na nguo za bei rahisi na kuongeza kiasi na ubora wa nguo unavyoendelea kukua.

3. Biashara ya kusafirisha watu: Unaweza kuanzisha biashara ya usafiri wa watu kwa kutumia gari lako au kwa kukodi gari. Unaweza kutoa huduma za usafiri wa watu katika maeneo ya mijini au kusafirisha watu kutoka sehemu moja hadi nyingine. Unapaswa kuzingatia sheria za usafiri na usalama barabarani.

4. Biashara ya kusafisha: Unaweza kuanzisha biashara ya kusafisha ofisi, nyumba, na magari. Biashara hii inahitaji vifaa vya usafishaji kama vile dawa za kusafisha, vifaa vya kusafisha, na wafanyakazi wanaofanya kazi kwa bidii. Unaweza kutafuta wateja wako kwa kutangaza biashara yako na kutoa huduma bora kwa wateja wako.

5. Biashara ya huduma za teknolojia: Unaweza kuanzisha biashara ya huduma za teknolojia kama vile ufundi wa kompyuta au kutoa huduma za mtandao kwa wateja wako. Biashara hii inahitaji ujuzi wa kutosha na uzoefu katika teknolojia na inaweza kuwa na faida kubwa kutokana na uhitaji mkubwa wa huduma hizi.

6. Biashara ya kuuza vifaa vya ujenzi: Unaweza kuanzisha biashara ya kuuza vifaa vya ujenzi kama vile mabati, saruji, mbao, na vifaa vingine vya ujenzi. Unaweza kununua vifaa hivi kwa bei ya jumla na kuuza kwa bei ya rejareja ili kupata faida.

7. Biashara ya kusindika vyakula: Unaweza kuanzisha biashara ya kusindika vyakula kama vile juisi, jam, na chakula kingine kilichosindikwa. Biashara hii inahitaji ujuzi wa kupika na kusindika vyakula na vifaa vya kusindika vyakula kama vile mashine za kuchambua matunda na blender.

8. Biashara ya kuuza bidhaa za urembo: Unaweza kuanzisha biashara ya kuuza bidhaa za urembo kama vile vipodozi, lotions, na vifaa vya urembo. Unaweza kuanza kwa kununua bidhaa za bei rahisi na kuziuza kwa bei ya juu ili kupata faida.

Kumbuka, kabla ya kuanza biashara yoyote, ni muhimu kufanya utafiti wa kutosha ili kujua kama biashara hiyo ina soko na inaweza kukuingizia faida. Unapaswa pia kuzingatia sheria na kanuni za biashara nchini Tanzania na kuhakikisha kuwa unafuata taratibu zote za kisheria za kuanzisha na kuendesha biashara yako.

Natumai hii itakusaidia kufanya uamuzi sahihi kuhusu biashara ya kuanzisha ili kupata kiasi cha kuanzia elfu 30 mpaka elfu 50 kwa siku. Kila la kheri katika biashara yako!
 
ml 3-4 uingize 50000 per day unachezea hiyo hela Kuna watu tuna laki 3 mtaji tunakunja mpaka 70000 per day
Ni winga tuu ndo anaweza piga hyo hela Kwa mtaji huo au below tofauti na hapo labda ufanye issue illegal
 
Back
Top Bottom