Kama umenunua gari ya Lhd ,ambayo kwa sasa ni cheap kuliko Rhd , bora libaki hivyo hivyo.
Kama unapenda au ni muhimu kuwa na gari ya Rhd , kwa sababu kadha wa kadha kama madereva n.k, ni bora ununue original ikiwa Rhd.
Nitazungumzia Scania ,maana nimeishi nazo, by default Design ya Scania ni Lhd , Scania za uk, ireland ,n.k ambazo ni Rhd, zimefanyiwa add on. Ie kuna parts zinaongezewa kuja upande wa kulia , mf gear link , hii huwa inatoka hapo kushoto ambapo gearstick ya Lhd huwepo kuelekea kulia , kuna air pipes za brake valve , pia huwa llinked kutoka kushoto kwenda kulia , kwa sababu hii procedure inafanywa kiwandani huwa ni salama , maana wanatumia designed parts. Hata hivyo bado scania za Rhd zina gear stick nzito kuliko za Lhd .
Nyingi nilizoziona zimefanyiwa conversion ,zinasumbua sana gear , zinasumbua sana short circuit kwa sababu ya kuhamisha fuse box , na nyingi vitu vizuri kama retarder huwa hazirudi haya kama ilikuja nayo , maana wanaofanya ile wiring uswahilini hawana uwezo wa kuirudishia kila kitu,