Naomba ushauri wa biashara ya malori

Ahsante Mkuu kwa maneno ya kutia Moyo.
 
Mkuu hongera, nimeandika kiasi kuhusiana na haya maduala ila nikupe assignment maana najua huo utafiti ama uchunguzi wako umeufanya kwa mmmilikimsimamizi wa magari, hakikisha unawapata hata madereva wako watatu nao uwafanyie usaili wa uhalisia wa sekta halafu tukae sasa hapa tukushauri. Utanishukuru baadae
 
"Kila unachokiona mbele yako kilishawahi kuwa kwenye truck"

Umeamua vyema kuwaza biashara hii.

Niongeze kidogo

Kuliko kununua gari used budget yako inatosha kuwapa TATA wakakupa gari mpya kwa 35m na trailer ukiunga unga utapata kwa 30m double tyres.

Super single ina changamoto nyingi sana kuliko unavyoweza kudhan!
Transcargo, Dangote hawana trailer za super single.

Ukiamua kuchukua gari used jitahidi kuipitia kila sehemu ikiingia barabaran usipate changamoto. Maghari yanayotoka Poland usichukue mengi yametumika sana.

Gari kutoka South Africa ukipata muungwana akakurekebishia kabla ya kulisafirisha ni gari bora kuliko mtumba wa Uingereza.

Ukiamua kuchukua Uingereza hakikisha MOT iko active hii gar imejaribiwa kwao na inafanya kazi katika barabara za Uk.
Scani 124 420, kuwa makina kuanzia 2002 hadi 2004 nying ni HPI ama red dot zinasumbua sana katika mazingira yetu.
6x2 chagua tag axle yaan teriaz nyuma ili uweze kubeba mzigo mkubwa.

Biashara ni nzuri ngumu, jitahidi ujibanze kwenye kampuni yenye kazi za uhakika. Kazi za dalali zitakufanya uchukie kazi.

Usimamizi jitahid mda mwigini uone gari nanufanye service.

Hayo machache kwa nilivyojionea barabaran.
 
Chukua hio gari mkuu tela usichukue supersingle pia waweza kukodi kwa kuanza usiingie mazima Sana jaribu kuminimize initial costs..chonde chonde KUA KARIBU NA GARI NA UIFUATILIE HASWA NASEMA HASWA MPAKA DEREVA WAKUONE MNOKO FLANI Kama Hilo huwez achana na hio biznes maana hapo ndio uchawi wake ulipo,,, welcome to the industry
 
Kabla hajaingia huko hakikisha una njia zingine zinazo kuingizia mapato japo kima cha chini uingize laki5 kwa siku tofauti na hapo endelea kujiwekeza,sikukatishi tamaa ila naielewa vizuri hiyi biashara mwaka wa tano sasa ukiweza hilo karibu ni bonge la biashara
 
Ahsante kwa muongozo lakini huko nimepita na ninaendelea kupita. Kama nilivyoeleza awali nipo na connection fulani inayoniwezesha kuongea na madereva na wamiliki ama wasimamizi wa magari. hivyo hilo pia la kuongea na madereva nalifanya sana katika research yangu.
 

Mkuu ahsante sana kwa ushauri. Naomba niongezee hapo kwenye 124 420 nichukue ya mwaka gani hasa.. Naomba nishauri range ya miaka ambayo imeonekana ni bora zaidi. Pia hiyo ya TATA Naifanyia kazi Mkuu.
 
Ahsante sana Kamanda. Umenipa wazo zuri. Nikweli kabisa naweza kuanza kwa kuwa na horse yangu na nikatumia trailer ya kukodi. Nalifanyia kazi Kamanda. Ahsante
 
Mkuu ahsante sana kwa ushauri. Naomba niongezee hapo kwenye 124 420 nichukue ya mwaka gani hasa.. Naomba nishauri range ya miaka ambayo imeonekana ni bora zaidi. Pia hiyo ya TATA Naifanyia kazi Mkuu.
124 , 420 mwaka 1999 hadi 2001 cummis engine , utafurahi, unaweza jaribu na V8 164 ama R500 kwa kazi za kiume zina fanya vyema sana.
 
Mkuu biashara nyingine iniingizie faida ya laki tano kwa siku yaani 15mil kwa mwezi? hahahaa Acha utani
 
164 haina umeme mwingi, shida kubwa huwez para right hand , nyingi zinatoka ylaya ya kati wanatumia left hand.
Point taken for consideration, Vp hizi 114 kuna kadhaa nimekutana nazo za 1999-2001. Ama unaweza kunipa series zote za scania zenye kufanya vizuri katika barabara zetu
 
Mkuu nimedhamiria kuzikabiri changamoto ulizotaja. Ahsante kwa ushauri
So mkuu unataka kuanza biashara na semi1 umeweka add-ons maana naona unaelezea as if tayari una yard, mafundi ikizingua njiani, hela ya risk in case ikizingua kwa ajali kama unanunua na upo familia na hio biashara basi nunua semi1 halafu ji-attach na tajiri mmoja ili mwende sawa ukiongeza la2 unajiachia and fly solo
 
Hakuna haja ya kujiattach kwa mtu. Mm Sio mgeni kwenye biashara mzee, nafahamu risk zilizopo. Niko na biashara nyingine na kazi pia. Nina uhakika wa kipato hvyo sitegemei kutetereka sana kama unavyodhania.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…