Wakuu nawasalimu kwa Jina la JMT.
Kama kichwa cha Habari kinavyojieleza. Nimekuja humu ndani kupata ushauri wa Biashara ya Malori haya ya kubeba mizigo iwe ya Local ama Transit.
Kutokana na Connection nilizonazo nadhani suala zima la kupata Mizigo ya Kusafirisha halitokuwa la kuumiza kichwa.
Changamoto inayonikabili ni funding pamoja na aina ya truck ambayo inapaswa ni nunue.
Kabla ya kuja humu ndani nilishaomba ushauri kwa watu kadhaa ambao wapo kwenye hii industry na wamenijuza truck nzuri ya kununua ni Mtumba SCANIA 124 420 iliyotumika Europe. Hawakunishauri kabisa kununua Truck Mpya ama Refurbished za Mchina, DAF na Volvo wakaniambia zitanitesa maana ndio kwanza naingia kwenye game. Hata nilipouliza SCANIA zilizotumika south Africa wakaniambia ni bora nichukue za europe zinakuwa bado zipo Bora na hazijatembea sana kwenye rough road kwa hizo za SOUTH japo hizo za south walikiri kwa gharama ya manunuzi zipo chini kiasi.
FUNDING
Kama nilivyoeleza awali mimi ni new comer kwenye hii industry hivyo nategemea kujichanga kama 50-60Mil then the rest nichukue mkopo maana nakopesheka vizuri sana. Baada ya kufanya window shopping nimegundua horse scania mtumba inaweza kunicost kati ya 75Mil - 85Mil hapa nitapata gari nzuri tu, Trailer nimeshauri kununua ya Mkononi ambayo imetumika hapa nchini ambapo zina range 25Mil - 30Mil kutokana na hali yake. Nimejaribu kuulizia. Mpya lakini naona bei imechangamka sana USD 28,500.00 flatbed Double tire
TECHNICAL
Nimeshauriwa hapo kwenye trailer kununua super single kwa maana inabeba Mzigo Mkubwa kulinganisha na trailer yenye double tire.
Kwenye Horse kama nilivyoeleza awali nimeshauriwa SCANIA 6x2 124L 420 Mtumba kutoka EUROPE
BUDGET
Ukiangalia makisio ya gharama zote Horse na Trailer budget yake inacheka kati ya 100Mil - 115Mil. 60% Nategemea kuitoa Mfukoni na 40% nichukue Mkopo. Nategemea kulipa Mkopo kwa kutumia Mshahara wangu pamoja na Mapato yatakayokuwa yanapatikana baada ya Truck kuanza kuoperate. Nimekuja kuomba ushauri kwa yeyote mwenye kuielewa biashara hii kwa undani, nimeweka mchanganuo wote hapa ili niweze kupata ushauri mzuri kulingana na information nilizopokea pamoja na uwezo wangu wa kifedha. Nategemea kuna wajuzi wengi humu na nitambulia ushauri mzuri katika kukamilisha hili. Ahsanteni na niwakaribishe kwa Ushauri. Kejeli na dharau hapa si mahala pake.
"Kila unachokiona mbele yako kilishawahi kuwa kwenye truck"
Umeamua vyema kuwaza biashara hii.
Niongeze kidogo
Kuliko kununua gari used budget yako inatosha kuwapa TATA wakakupa gari mpya kwa 35m na trailer ukiunga unga utapata kwa 30m double tyres.
Super single ina changamoto nyingi sana kuliko unavyoweza kudhan!
Transcargo, Dangote hawana trailer za super single.
Ukiamua kuchukua gari used jitahidi kuipitia kila sehemu ikiingia barabaran usipate changamoto. Maghari yanayotoka Poland usichukue mengi yametumika sana.
Gari kutoka South Africa ukipata muungwana akakurekebishia kabla ya kulisafirisha ni gari bora kuliko mtumba wa Uingereza.
Ukiamua kuchukua Uingereza hakikisha MOT iko active hii gar imejaribiwa kwao na inafanya kazi katika barabara za Uk.
Scani 124 420, kuwa makina kuanzia 2002 hadi 2004 nying ni HPI ama red dot zinasumbua sana katika mazingira yetu.
6x2 chagua tag axle yaan teriaz nyuma ili uweze kubeba mzigo mkubwa.
Biashara ni nzuri ngumu, jitahidi ujibanze kwenye kampuni yenye kazi za uhakika. Kazi za dalali zitakufanya uchukie kazi.
Usimamizi jitahid mda mwigini uone gari nanufanye service.
Hayo machache kwa nilivyojionea barabaran.