Naomba ushauri wa fursa za biashara zinazopatikana Kahama

Naomba ushauri wa fursa za biashara zinazopatikana Kahama

Track47

Member
Joined
Dec 25, 2011
Posts
18
Reaction score
13
Habarini wana JF, nitangulize shukrani za dhati kwenu wote.

Nahitaji kuanza maisha yangu mjini Kahama. Natambua kuna wazoefu na wenyeji wanaoijua vizuri. Nina mtaji mdogo tu wa milioni moja.

Je, kitu gani naweza fanya hapo kwa huo mtaji hata kama ni kidogo japo nipate cha kufanya kuliko kusubiri hizi ajira na kuondokana na hii tabia ya vijana tulio wengi kukaa tu nyumbani kusubiri ajira na kuvizia chakula cha wazee.

Naomba kuwasilisha.
 
Kahama wazawa wanafanya biashara kwa mazoea sana wamelewa hela...!yaan mtu anabiashara nzuri sana lakini customer care hakuna...!ukiweza kumanage hizo ishu hela itakuja km ilipotea imerudi nyumbani!
vipi kwa mzunguko wa biashara nyingine kama nafaka na kadhalika?
 
Nisaidiwe aina za mabenk yaliyopo kahama wakuu.


Ukiachana na hizi crdb,nmb,Azania, access na Postal bank.

Natanguliza shukrani
 
Mpunga unalimwa sana.Unaweza anzisha duka la kawaida hapa mjini madam upate site nzuri.Lakini pia unaweza kuwa unaenda uganda kufunga mzigo mzuri( viatu na nguo mtumba) unaushusha kahama.
 
Ahsante swali la msingi sana..Chanzo cha Kuchagua Kahama ni Kwenye Pita Pita Pita zangu tu japo kwa Muda mfupi nikalinganisha na Sehemu chache Ambazo nimepita,ila jambo la kwanza kwa Upande wangu nilivutiwa nacho ilikuwa kwenye Hasa Garama za Maisha kwa ujumla kuanzia vyakula,Mahala pakuishi na Movement za Mjini Pia Sehemu nyingi hazihitaji kutumia Sana usafiri, ila Pia niliona ni moja ya Miji ambayo inakuwa na inazidi kukua kiuchumi na Pia mzunguko wa Biashara upo kwa Kiasi flani,Pia ni Center ya Kwenda Baadhi ya nchi za jirani kitu ambacho kilinivutia zaidi maana natamani pia siku moja kufanya biashara kwenye Hizo nchi kama Rwanda na Uganda hivyo nikaona kwa mtazamo wangu ninaweza nikaanzia hapo , hasa kwa mimi ambae naanza Maisha ya Kutafuta.
Kwa uchache ni Hayo sijui kama nitakuwa nimekujibu vya Kutoshaa.
Ahsante
Uko pande zipi kwa sasa na kwa nini umeichagua kahama
 
Nipo hapa Club Chillers nakata whatever-vant kubwa kwa kasi ya karasha......
Mkuu, kahama kina fursa nyingi kama ifuatavyo:-
Kilimo
Madini
Mazao
Nguo/Viatu

Kahama unaweza fanya biashara yeyote na ukapata faida ikiwa tu utakuwa na nidhamu kwenye pesa.
 
Back
Top Bottom