Naomba ushauri wa gari gani zuri la kutembelea lisilozidi Sh. milioni 10

Naomba ushauri wa gari gani zuri la kutembelea lisilozidi Sh. milioni 10

Prodigy Oligarchy,
Hata mimi naunga hii hoja, kina ist, raum na wenzake ziso gari za kujifunzia, kwanza zina ground clearance ndogo. Ni rahisi kuzifanya zichoke mapema
 
Automatic door ni moja tu.
Na kama haupo kwenye mazingira rafiki unaweza ukazima motor ukawa manual kama wa upande wa dereva
Najua ni mmoja mie nimeitumia hyo gari kwa miaka miwili nakuhakikishia ni gari ngumu sana ila changamoto ya mlango si kubwa sana ila shida inakuja mtu akipanda na kuanza kuusumbua utaharibika tu..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tafadhalii naomba unifafanulie hapaaa
Wanasema kuwa ukiendesha gari mjini (80000), vituo vinakua ni vingi mfano foleni, mataa n.k hivyo mara nyingi transmission inakua busy kupandisha na kushusha gia; brakes system pia sababu ya kusimama simama; pia cooling system inakuwa busy sababu pale gari linaposimama mafan lazima yawashe ilikupooza engine.
Ila ukiwa highway transmission inabaki kwenye gia muda mrefu, brake zinatulia na upepo unasaidia kupooza gari
 
Najua ni mmoja mie nimeitumia hyo gari kwa miaka miwili nakuhakikishia ni gari ngumu sana ila changamoto ya mlango si kubwa sana ila shida inakuja mtu akipanda na kuanza kuusumbua utaharibika tu..

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni kweli ni gari gumu, shida inayokuja ni kwenye ground clearance. Raum lipo chini na huyu ndugu yetu amesema hajui hata kuendesha gari.

Haya magari haya ukishaanza kuongeza mavitu ili kulifanya liwe juu huwa kuna percentage ya stability inapotea.

Angekua dereva wa muda nisingekuwa na wasiwasi ila ni dereva mpya na anataka kusafiri na familia nzima kwenye hilo gari
 
Mkuu usimfuate huyo mfanyabiashara Spacio huwezi ilinganisha na Raum na Ist hyo ni nyepesi mno

Sent using Jamii Forums mobile app
Kaka,
Kama kigezo ni 'ufanyabiashara"
Hata be forward, gari mlizopemdekeza zipo, tena nyingi sana.
Nilikua nauwezo wa kumwambia juu ya hizo pia.

Lakini nimeona, zitamtesa kwa kuchoka haraka. Ndio maana nikawaza juu ya Corolla spacio. Samahani kama kwa namna fulani ni,eingilia maslahi yenu, wala hata kamwene vanyalukolo asiagize kupitia Mimi, hata akinunua kwenu ni sawa tu, lakini tujitahidi kumpa kitu ambacho atakaa nacho muda mrefu. Bila kumpa shida yeyote.

Mkumbuke kwamba, utakapompa kitu kizuri ambacho kitadumu miaka 2 na kuendelea bila shida, basi hakika itawapa credit nzuri sana.

Lakini mkimpa kitu ambacho, atatumia mwaka kianze kumpa shida, hatoweza kurudi kwenu tena, na kibiashara itakua imewaangusha.

Narudia tena, tusichukulie advantage ya kwamba, yeye ni mgeni, basi tukampa tu gari ilimradi gari, bali tuitu,ie nafasi hii kumpa kitu ambacho atakaa nacho muda mrefu bila masumbufu.

Kama mnauhakika, raum inaweza kuingia njia mbovu kwa muda mrefu, kama mnauhakika raum inaweza kuingia hata njia za mashambani ., basi mpeni

#Nobeef
 
Ni kweli ni gari gumu, shida inayokuja ni kwenye ground clearance. Raum lipo chini na huyu ndugu yetu amesema hajui hata kuendesha gari.
Haya magari haya ukishaanza kuongeza mavitu ili kulifanya liwe juu huwa kuna percentage ya stability inapotea.
Angekua dereva wa muda nisingekuwa na wasiwasi ila ni dereva mpya na anataka kusafiri na familia nzima kwenye hilo gari
Ila boss ukiifunga Spensa kuipandisha kidogo itakuwa shida!!?

Gari nyingi hapa mjini kwa nature ya barabara zetu hasa hzi gari ndogo kuzipandisha hakuwezi kuepukika na madhara yake hayawezi kuwa makubwa.

Sawa labda tumshauri kuhusu Spacio ambayo ina cc karibia 1900 ila Raum ni 1490 cc na pia Spacio huwa naona kama luxury hazivumilii shida sijui wewe unalionaje hili..
Ndio mana bado nashauri abaki kwenye Raum na Ist mana kigezo cha spea almost Toyota spare zinapatikana nyingi tu mjini

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Prodigy Oligarchy, Samahani kwa lugha iliyokukwaza..

Narudi kwenye swali hvi kaka unaweza kusema Raum na Ist ni mbaya!??na hazivumilii shida!??

Mie nimetoa maoni yangu tu kutokana na budget yake ya 10 mil

Spacio sio mbaya ila kumbuka huwezi kuipata kwa budget yake ya 10mil na pia ulaji wake wa mafuta ni mkubwa ukilinganisha na Raum au Ist!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mnazareth,
Hapo kwenye spensa ngoja niwaachie wataalamu waje waelezee zaidi. Ila tu nikukumbushe kuwa spacio ni Corolla na kuna za 1.5l na zile za 1.8l
 
Mnazareth,
Bila samahani kaka, sisi ni binadamu, hakuna aliye mnyoofu, sote tuna madhaifu.
Sijasema yakwamba ni mbaya kaka, bali nimesema kwa hali ya mdau hapa, bado haja 'master' hata kuendesha. Kwa maana hiyo gari yake ndio itakua pia ni kama ya kujifunzia.

Pili, ameweka wazi kwamba, yeye ni mtu wa familia, sasa fikiria wameingia watu watano, wakianza kuweka na mizigo, unajua namna raum inavyokua inadidimia kwa nyuma .. lazma tu itakua inaburuza sehemu fulani.

Lakini spacio, ilivyoundwa, ina nafasi ya kuweka watu wengine nyuma kabisa, wawili. Kwa maana hiyo hata asipoweka watu kule nyuma , ila akaweka mizigo, still gari yake inakua iko freshy tu ukizingatia kama anasafiri.

Spacio, ina 1,490cc na ulaji wake wa mafuta sidhani kama ni m'baya hivyo. Maana inakwenda wastani wa 16km kwa Litre.
 
Hapa hujamshauri vizuri ila imekuwa ni fursa kwako na hapo wenzako kufanya biashara (riba ya mkopo).

Ahsante
Hili ni jukwaa huru,
Unao uhuru pia wakuweza kutoa ushauri wako mzuri.
Nikukumbushe, sisi binadamu, huwa tunajua kwa sehemu tu, hakuna anaejua kila kitu.

So, huwenda unacho, ambacho unajua zaidi ya tujuavyo. Karibu tujifunze.

#KwaamaniKabisa
 
Back
Top Bottom