kwanza hakuna aliyesema kwamba aende kukopa fedha ,ushuri upo mwingi kwenye kuongeza mtaji kwa mtu aliyekwama, Mimi nilichosema ni kuwa anachopaswa kufanya ni kuanza kidogo kidogo tena kwakua biashara hii ameifanya kwa muda mrefu na anasema kuna jambo liliingilia likamtatiza kwenye biashara yake, pili nikamshauri aanze tabia ya kuweka akiba ya kile kidogo anachopata kwakua kanuni ya mikopo siku zote ni kuwa unakopa ili kuongezea kwenye mtaji wako yaani 75% ni fedha zako na 25% ni fedha za mikopo. Sasa unapokuja ushauri wa kuuza makazi yake aongeze kwenye mtaji hili nasema si wazo jema kwakua linamuweka mhusika kwenye risk kubwa kwakua hakuna anayefahamu nini kilicho mkwamisha kwenye biashara yake awali , halafu kingine ni kuwa hakutakuwa na nidhamu kubwa kwenye fedha ya kuuza mali yako na ile ya kukopa. Kaka nikuombe ufikiri tu maana kanuni yangu ni "kuwa usipo fikiri utanuka"