Naomba ushauri wa kununua gari used ndani ya nchi

Naomba ushauri wa kununua gari used ndani ya nchi

Saidama

JF-Expert Member
Joined
Jun 10, 2022
Posts
598
Reaction score
1,151
Habarini wana jukwaa.
Kama kichwa cha habari kinavyoeleza.

Nimejichanga changa, mungu kasaidia nimepata kitu kidogo, nimeamua ninunue usafiri kurahisisha shughuli zangu.

Natamani nipate gari kama Spacio au Raum ila sina uzoefu kabisa na magari.

Hivyo nimekuja kwenu kuomba ushauri wa ni vitu gani vya kuzingatia katika kununua gari used iliyotumia nchini. Nahofia kuuziwa kitu kibovu chenye muonekano mzuri kwa nje

Naomba kwa anaefahamu pia, hizi gari zikiwa used zenye hali nzuri zinauzwa bei gani? Toyota Spacio na Toyota Raum.

NATANGULIZA SHUKRANI
 
Sio kweli,Unaweza ukanunua gari used na ukapata nzuri tu!
usiangalie namba,tafuta mtu unayemwamini anayejua magari atakayekushauri.
Gari ya kwanza sio lazima ununue mpya--pia itakupa uzoefu wa magari
Kila la kheri
 
Habarini wana jukwaa.
Kama kichwa cha habari kinavyoeleza.

Nimejichanga changa, mungu kasaidia nimepata kitu kidogo, nimeamua ninunue usafiri kurahisisha shughuli zangu.

Natamani nipate gari kama Spacio au Raum ila sina uzoefu kabisa na magari.

Hivyo nimekuja kwenu kuomba ushauri wa ni vitu gani vya kuzingatia katika kununua gari used iliyotumia nchini. Nahofia kuuziwa kitu kibovu chenye muonekano mzuri kwa nje

Naomba kwa anaefahamu pia, hizi gari zikiwa used zenye hali nzuri zinauzwa bei gani? Toyota Spacio na Toyota Raum.

NATANGULIZA SHUKRANI
Wanawake wagumu kutoa hela na kufanya service magari. Kama hana mwanaume wa kumfanyia service zinakufa vibaya.
Ukisikia alikuwa añàtumia mwanamke kimbia usinunue.
 
Yupo mkoa gani? Mi sipo Dar
Yuko Dar.
Nilitaka kukushauri nenda Facebook magari kama takataka yanauzwa. Then fundi ndiye akalikague. Fundi wa mwenye gari atakuvisha kwa kupewa kahongo kidogo. Ungekuwa dar nina mafundi wa uhakika government certified wangekukagulia kwa fedha ndogo.
Gari ya kuuziwa na Mtanzania si ya kuamini kwa macho
 
Back
Top Bottom