Naomba ushauri wa kupata simu ya nzuri za iPhone

Kama ulikuwa unatumia iTel mkuu nakubaliana na wewe. Shida betry za hizo simu hazifiki hata 2000 mah wakati kuna simu za android nying sasa ni 3000 Mah na kuendela mpaka 5000.
Pia kama umetumia kuanzia iPhone X utajua kwanini nasema kuna kitu flani utakikosa kwenye hizo simu. Sema ni nzuri huwezi kumiss kitu ambacho hujawahi kukiexperience kama ndipo ulikoanzia. Haikai na charge kisa ina mah ndogo. Na iOS ni OS moja iliyo tengenezwa kulinda charge ingekuwa ni android ungekoma zaidi.
 
Nilishatumia androids nyingi tu za kueleweka ikiwemo Sony Xperia Series! Wao walikuwa na 2500mAh ila zina last longer sana!
Hapo itel nilikuwa nazugia tu wakati nasubiri iPhone
 
kuna mdada nmepanga nae ana iphone akiwa anawasiliana anahakikisha vidole havizibi lile tunda[emoji1].nikiwa napiga nae story ananiambia iphone n ya kutoka nayo tuu out akirud geto anachukua infinix .anakwambia tangu amiliki iphone hajawah weka wimbo wwte et inamchanganya upande wa kudownload na mambo mengi yapo complicated[emoji1][emoji1][emoji1][emoji1]
 
Nilishatumia androids nyingi tu za kueleweka ikiwemo Sony Xperia Series! Wao walikuwa na 2500mAh ila zina last longer sana!
Hapo itel nilikuwa nazugia tu wakati nasubiri iPhone
Nipe maelekezo ya kununua iphone used canada sitak masoko ya aliexpress na the like
 
Asante sana mkuu.Hakika nmepata kitu
 
Hahahaa labda mshamba.Mbna wengne wanapeta tu
 
Ni Simu Iliyotumika Huko Ughaibuni Kwanza Halafu Ndiyo Inaletwa Hapa Tanzania Ikiwa Wakati Mwingine Na Kila Kitu Chake!!!


Sasa Inategemea Unaweza Kuipata Ikiwa Na Hali Nzuri Kila Idara Ama Kinyume Chake.
Chukua Ushauri Wa Wataalam Wa Hapo Juu
Asante mkuu
 
Duuuh mkuu asante kwa ushauri.Samsung gani current nzuri?Na yenyewe ina refurbished?
 
Asante mkuu kwa ushauri
 

Nipe namba nimsaidie ni simple tu..
 

Mkuu chukua iPhone 7 Gb 128 ni simu nzuri sana unapata IOS updates zote hadi latest 14.5 pia ina high processing speed na 2gb Ram.
Charge inakaa kutwa nzima ukiwa online Mda wote with 4G network.

Kinging apple wana real phone specification.
Eg.
retina camera, jinsi macho yako yanvyoona kitu ndio picha ya iPhone ikionyesha

Real Ram, iPhone huwezi kuta ina stack au ku load kitu kwa muda mrefu kama android

Lakini Android huwa simu zao wana label specifications yaan unakuta simu specification kubwa lakini uwezo au uharisia zero kabisa.

Mimi natumia iPhone 7 gb 128 na jamaa yangu anatumia sumsung kubwa tu kam A10 au A20 tulizilinganisha uwezo wa processing power ya internet

Tukachukua laptop yenye Ram 8gb na processor core i3 Tuka connect WIFI kwa kutumia simu yake ya Samsung aisee pc iko slow kwenye internet Kama kobe

Then tuka disconnect na ku connect iPhone 7 yangu 4G network aisee yaani ukigusa link faster pc ina open.
Na wote tulitumia chip ya Vodacome 4G

Baada ya hapo jamaa akaamini iPhone wapo realistic kuliko android wao wana label specification lakini uwezo halisi wa simu zero.
Kwa hiyo achane kuofananisha iPhone na simu za kijinga.
 
Hahaaa mkuu tatzo lingne ni kwenye kugundua simu ambazo zpo refurbished.
 
Bro ulikua unatumia Bajaji alaf unanunua V8 unashangaa liko faster? Nunua Android ya bei kubwa uone kma iko slow kma hzo itel
 
wazo zuri, mi mwenyewe naelemika kwenye hili
 
Yaani A20 unalinganisha na iPhone 7 [emoji23][emoji23] nyie watu nyie. iPhone 7 ni flagship na A20 ni low budget phone. Ilinganishe na akina S8 huko. Size ya kioo isikuchanganye. Ingekuwa hvyo basi Infinix ndio zingekua simu zenye uwezo kuliko zote
 
a10 unalinganisha na 7 kweli!!!!

halafu hakuna iphone 7 inakaa masaa 12 na charge usimuinhinze mwenzako mkenge akaanza kujuta.

iphone 7 ni simu yenye nguvu safi tu ila betri ni kimeo,zimeshachoka.kwa hiyo a10 nadhani ulikiwa unarudia kucharge mara 4 ndio mwenzako wa a10 anacharge tena.

halafu hakuna android inayoweka specs za uongo,unachoona ni utogauti wa OS tu,labda kama unazungumzia zile 64gb halafu ikiweka whatsapp inakwambia storage full(manganya).
kama unataka uelewe chukua simu ya window hapo,ndio utajua tatizo sio simu ila ni OS husika ndio ina wenge.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…