Habari wana JF, mimi ni kijana umri miaka 30. nina familia mtoto mmoja na nimeajiriwa kazi nzuri tu. Kwa haraka haraka naweza kusema maisha yangu ni mazuri kwa hilo nashukuru Mungu. Kilichonifanya kuandika uzi huu ni tatizo langu ambalo nimekua nalo muda mrefu naweza kusema toka nimezaliwa, tatizo la kushindwa kujiamini (wazungu wanasema social anxiety).
Labada nielezee historia yangu kwa kifupi inaweza kusaidia. Mimi nilizaliwa kwenye familia ya kawaida tu na nimelelewa tu vizuri. ilitokea nlikua namuogopa sana mzee wangu sijui kwanini. nilikua nashindwa kuongea nae freely na nikisikia amerudi kutoka kazini nilikua naingia hofu kwelikweli. Shuleni pia pamoja kua nilikua mwanafunzi bora, nilikua siwezi kusimama kuuliza maswali au kuchangia kitu chochote darasani kutokana na hofu. kipindi cha presentations nlikua natetemeka sana na kutoka jasho hali ambayo ilinifanya kuchekwa na kutaniwa na wenzangu.
Mpaka leo nimeajiriwa nina miaka sita kazini bado hali hii ipo. Naona aibu sana kuongea na watu wapya, siwezi kuangalia mtu machoni, ikitokea mabishano mimi hua ni mtu tu wakukubali hata kama naona si sawa, kwenye social events naogopa kuudhuria nahisi naweza itwa mbele labda kutoa speech kidogo.
Kazini nadhani walishaona mapungufu yangu haya. Mara nyingi wakihitaji mawazo kutoka kwangu hua hawaniulizi tukiwa wengi manake wanajua ntaogopa kuongea, badala yake hua wananiambia niwapatie riport iliyoandikwa nikishauri nini cha kufanyika.
Japokua naonekana kama mfanyakazi bora na anayejituma, nakiri kua hali hii imeniruidisha sana nyuma katika carrier growth. uwezo wangu mdogo wa kushawishi mambo kufanyika, kuongoza wenzangu na kujiamini umesababisha viongozi wangu kutonipatia majukumu makubwa zaidi japokua wanafahamu wazi kua nayaweza ila ndo ivo yanaitaji social skills ya hali ya juu.
Mimi ni mzuri sana nikipewa kalamu na karatasi, lakini likija swala la kuongea siwezi kabisa. kuna baadhi ya wenzangu ambao nilikua nao nafasi moja, walizitumia kazi zangu kwa sababu mimi sikuweza kuzipresent kwenye vikao vikubwa na ziliwawezesha wao kupandishwa vyeo na mishahara.
Hili kwakweli liliniumiza sana na sasa nimeona nitoke out of my comfort zone na kujaribu kukabiliana na tatizo hili. kwa utafiti niliofanya mtandaoni wanasema suala hili linatibika kwa dawa pamoja na ushauri na saha. Kwa hapa Tanzania kwa sijajua kama kuna taasisi ambazo zinahusika na masuala haya. Kama ipo tafadhali naomba lkufahamishwa. Kama kuna mtu ana ushauri wowote naupokea pia. Asante
Yaani kama vile umetoa historia yangu kabisa.
Hata mimi nilikua hivyo. Nakumbuka niliwahi kusanabisha darasa nzima likachapwa viboko kwa kutoweza kujibu swali moja. Swali ambalo nilikua najua jibu lake lakini kwa vile nilikua siwezi kuongea mbele za watu sikujibu.
Mimi pia ni mzuri wa kuandika, ninaweza kuandika mada hadi watu wakiisoma hawaamini imetoka kwangu, aibu ukimia na upweke ndio shida yangu.
Yaani hukuacha kitu vyote ulivyosema labda ninaweza kukuzidi maana pia nilikua napenda kukaa peke yangu zaidi na si rahisi kuzoeana na watu.
Ila sasa hivi nimebadilika sana.
1. Naweza kuanzisha story na kuisimamia kijiweni
2. Naweza kuongoza watu na nimekua kuongozi
3. Siogopi tena kuhojiwa kwwnye T.V au public ila inabidi nijikamue kisawasawa
4 Aibu haijaisha lakini imepungua sana
5 Nimekuwa mhubiri wa injili kanisani jambo ambalo sikutarania
6 Eti kuna wakati hata mimi ninakuwa mchekeshaji na watu wakacheka.
7. Jambo ambalo bado najitahid ni kuongea mbele za watu haswa nikishtukizwa, wakati mwungine tunakua kwenye semina za kikazi sasa kutoa point inakua mbinde japo nikijikakamua nawezaga.
Sasa nilifanyaje?
1. Nilimuomba Mungu
2. Niliikataa ile hali hapo najua nilirithi kwa mzazi
3 Elimu ilinisaidia maana nilikutana na watu wengi
4. Nilifanya practise sana. Wakari mwingine nilikua najifungua ndani naongea na kalamu makaratasi najihubiria kana kwamba niko na watu.
5 ambayo ni muhimu sana nilisoma vitabu, kuna vitabu vingi sana vinafundisha namna ya kuongea.
6 Nilijikubali na nilijua hatuwezi kufanana na wote.
Hakuna dawa, usijaribu kulewa wala kwwnda kwa waganga watakuharibia. Kama lazma upate tiba basi soma neno kama ww ni mkrsto kama sio mkrsro piga dua zako za kutosha