Naomba ushauri wakulungwa. Toto kiburi nataka kumpeleka Kizuka shule ya TPDF

Naomba ushauri wakulungwa. Toto kiburi nataka kumpeleka Kizuka shule ya TPDF

From Meru

JF-Expert Member
Joined
May 19, 2023
Posts
3,931
Reaction score
9,376
Kuna mtoto wa ndugu yangu
ninamsomesha. Huyu dogo kafaulu
Kidato cha 4. Kapangiwa college,
kwa akili za huyu mtoto naona bado hawezi kusoma college.
Ni kijana wa kiume, mvivu, bonge, hana adabu, jeuri. Kwa ujumla alilelewa kishenzi.
Mimi niko mbali na anakoishi.
Nimewaza aende Form 5 shule za kijeshi. Kuna jamaa amenishauri Kizuka iko Ngerengere Morogoro.

Kwa anayeijua zaidi Kizuka naomba maelezo. Na kama kweli itafaa kwa toto aina hii
 
Kimsingi naye pia awe na nia ya kusoma ila kwa kunyooka atanyooshwa. Mpeleke utakuja kuniambia huko ndiyo kuna watu wamevurugwa hasa.
 
Kimsingi naye pia awe na nia ya kusoma ila kwa kunyooka atanyooshwa. Mpeleke utakuja kuniambia huko ndiyo kuna watu wamevurugwa hasa.
Ahsante sana mkuu.
Hakua anataka kusoma Advanced ila natumia ubabe na lazima. Mtoto ni mshenzi sana.
Nadhani kama wako vizuri kuwa discipline naamini hata kusoma hatakua na namna zaidi ya kusoma ama kwa kupenda au bila kupenda
 
Uzuri ni kwamba nina paelewa na siyo kupewa masimulizi, kwa ishu za nidhamu,kuuondoa huo uvivu linawezekana tena anaweza jikuta anavutiwa mno kuja nae kupiga kitenge hapo baadae.
 
WALIWENGU SIKU ZOTE HUFUNZA WALE WASIO SIKIA, LAKINI JITAHIDI KUMWELESHA PASIPO KUTUMIA NGUVU.

#ROCA FELLA
 
Back
Top Bottom