Esperance
JF-Expert Member
- Jan 27, 2011
- 364
- 84
Nashukuru sana wote kwa ushauri wenu, ila mimi wasiwasi wangu ni kuwa je ni kweli anamaanisha anachokisema?
Maana kwa jinsi ninavyomuelewa anaweza kusema hivyo lakini bado hajawa na maamuzi kamili. Na wasiwasi wangu umenidhihirishia baada ya sasa kuanza vituko,
Mfano jumamosi nilimuuliza kama ataenda na watoto kumuona babu yao anaeumwa akasema hajajua, baada ya mimi kuondoka kwenda kazini alikwenda nao na akawaacha walale huko bila kunitaarifu, na hapo yule mtoto wa kwetu wote naumwa na kuna dawa anatumia na ameziacha nyumbani, baada ya mimi kurudi nyumbani na kugundua kuwa mtoto hatarudi na dawa ameziacha nikampigia kumuuliza sasa tunafanyaje maana dose itaharibika, akasema subiri nakuja tena kwa hasira, na aliporudi alikuwa kimya wala hakulizungumzia na likuwa amelewa, asubuhi pia akawa kimya, sasa ni visa tu na juzi amempeleka mtoto kwa aunt yake bila mimi kujua pia mpaka leo hajarudi, yaani kama mtu mwenye bifu fulani hivi na maelewano hakuna, na jana amelala kwenye chumba cha watoto.
Hio ndioo hali halisi ndugu zangu haya naendelea kusikiliza ushauri wenu.
Mpendwa baraka , kama wadau walivyoshauri jana , mwende mkapime wote mjue status zenu mpokee majibu kwa pamoja.Kutoka hapo mnaweza kufanya maamuzi.Kama ameshaanza kukunyanyasa mapema hivyo sijui huko mbeleni itakuwaje .Naamini hamaanishi anachokisema muendelee kuishi.Baraka unahitaji upendo na faraja sio hayo anayoyafanya hata kama ni kweli yu negative. Pole sana mlilie Mungu atakusaidia.