Naomba ushauri wenu wana JF


Naona sijaeleweka mie nimesema swala la mwanaume kukubali kiulani bila kuhoji ndo issue iliyonichanganya.

Hizo ndoa za positive na negative mbona nyingi tu na tunawapa ushauri jinsi ya kuishi bila kuambukizana???

VCT au CTC???
 
Kuachana si suluhisho,suluhisho ni kuikubali hali na kuvumiliana.
 
Habari ya muda wana JF
Kama nilivyowaambia kabla kuwa huyu mume wangu ana kigeugeu sasa hivi kaja na mpya tena anasema hana tena imani na mimi kama naweza kumlinda hivyo ni bora tuachane. Ila alichonichanganya zaidi anasema nyumba inabidi iuzwe. hayao aaliyasema jana, leo asubuhi kabadilisha tena anasema hapana tusiachane tutengane tu. Mpaka naondoka sikupata kujua ni nini anataka kuachana au kutengana? Habari ndo hiyo ndugu zangu
 
Pole sana dada,just kno that God loves u, he listen talk to him, ur his child anointed empowered and eqqiped. Simply be incouraged.wengi wamekushauri vizuri ila mimi nakukumbusha tu kuwa nothing is impossible to God,unaweza kupona kabisa. Faith moves mt. I love u sister.
 


Pole sana barak, kwa fikra zangu mimi, nahisi kabisa mumeo pia ni muathirika pia ukute ndo alie kuambukiza.

Pili yawezakua analijua hilo tokea zamani sana ila hakuthubutu kukwambia. kwakua angekuvunja moyo .

Kitu kingine hakupenda kukwambia kwa kuogopa utawambia watu kua nyinyi ni waathrika.

Sidhani kama ni upendo tu, upendo wa agape huo ndugu yangu. cha kufanya usimuache endelea kuishi nae, muombe mkapime wote pia na mtoto

Ili muhakikishe, akiwa mbishi usilazimishe cha muhimu amekubali muendelee. kwa wewe pia niwakati wako wakua karibu na mungu kupita kawaida naku msihi mumeo pia kurudia mungu.

 
pole sana dada kwa wakat mgumu ulionao kwa sasa.
ila kuna vitu me vinanifanya niwe na waswas kidogo....

kwanza hii thread umejaribu kueleza juujuu sana mpaka unaona wachangiaji wanamponda sana mmeo.

pili kuna sehem nimeona umesema huo ugonjwa uliupata labda kutoka kwake au kabla ya ndoa sabab hujawah saliti ndoa. ebu fikiria mmeo ndo angekuwa wa kwanza kukupa hayo maelezo kwamba ni muathirika hivi ungelimuelewa kirahisi kama ulivyoandika, hapo najua ungetokea ugomvi wa ajabu sababu ww unauhakika haujasaliti ndoa sasa yeye kasaliti na sahv ni mgonjwa. apo najua ungedai taraka na kivumbi cha ajabu....check n think then use brain.
wengi wamekushauri vizuri sana, ila ninawaswasi kama utaendelea kuwa nae apo ndani na mambo yakawa safi kama mwanzo kabla hamjapima.
kuhusu jamaa kwa ninavyojua wanaume tulivyo atakuwa keshapima na kakuta anao naye kanyamaza sababu naye ana mchezo mchafu nje ya ndoa na anaamini yeye ndo kakupa so anajaribu kuona upo vip.
 

Oooh brother mungu akubariki sana kwa moyo wako mkuu.
 
Pole sana, we tulia muache yeye achague anachopenda, kwasababu yeye ndo anasema hivi mara vile.
tulia endelea nakazi kama kawaida mpaka atakapojua anataka nini ndo mtaelewana sasa.
 

Dena Amsi kama umesoma mawazo yangu vile. Alikuwa anajua kwamba ameathirika ndiyo maana akawa anajibaraguza na kujidai. Kwa nini amekwenda kupima mwenyewe na hawakufuatana kwenye hilo? Samahani lakini inawezekana anajua sana hali yake ya kiafya alikuwa anakuzuga tu.

Hebu jaribu kufuatilia huyo mama wa mtoto wake bado yuko hai?

Pole sana lakini madamu amekubali mwenyewe wewe endelea nae tu.
 
loliondooooooooooooo!!!!!!!!! Nendeni tu wala msisikilize mameno ya watu ninao ushahidi wa2 wanne na mtoo wa miaka 6 walioenda na wako freshi sasa wanasubiri vipimo vya mara ya pili mwezi wa saba
 
Michelle mambo?
nahisi DA na wengineo wanaompinga mume huyu kwa vile namna ambavyo story imekaa ni vigumu kuamini reaction hii ya mumewe.
1. Kwanza alikuwa anakataa kupima afya yake kwa madai kuwa anaogopa na siku akijua ameathirika atakufa: Ujasiri wa kwenda kupima pasipo kupanick baada ya kuona cheti cha mkewe ameupata wapi? tena kenda pima kimya kimya kisha aja ASEMA (si kuonyesha cheti!!) kuwa hajaathirika???
2. Na kwa uwoga wa kuathirika (kama alivyoonyesha mwanzo) sidhani kama angewezakukubali kuendelea na mkewe unless wifey aseme kuwa makubaliano hayo hayahusishi kushiriki tena tendo la ndoa)
3. Lakini kikubwa nilichonote ni kuwa huyu bwana alizaa nje ya ndoa (huyo bintiye mwenye miaka 10 wakati first born ana miaka 12) ina maana wakati ndoa yake ina miaka 2/3 yeye tayari alishakuwa 'mzoefu wa nje'.....sasa miaka kumi ya mazoea na upungufu wa mapenzi unataka kunambia alitulia na kuwa saint?? Labda!! kama ni kweli nini kilikuwa kinamfanya awe anagoma kwenda kucheck afya??
4. Hii hadithi haijakamilika...........kuna missing/omitted parts nyingi tu
 

Baraka huyo ni mumeo kwa hioli unalolieleza hapa hebu jaribu kumshawishi mwende tena wote mkapime upya kisha baada ya kuhjakikisha nawe umeviona vipimo vyake naye kaona vyako au mmepewa majibu pamoja ndipo uje hapa tujadiliane hayo ya kuuza au kutouza nyumba...........mbona kama kachanganyikiwa sasa??
 

Duh nina wasiwasi na anayoyaeleza kwa hao ndugu zake. Pole sana Baraka but jipe moyo MUNGU atakupigania.

Reaction ninayoiona hapa ni KUCHANGANYIKIWA...........na si kuwa amechanganyikiwa kwa kuwa wewe umeathirika la hasha wanaume wengi hawako hivyo hawako tayari maisha yao yafanywe magumu na mtu mwingine let alone mwanamke (Man's Ego). Yaani ingekuwa hivyo angekwisha kutangazia uchafu ili tu akuondoe kwenye maisha yake. Huyo amechanganyikiwa baada ya kugundua kuwa naye si salama (kama kweli alikwenda kupima na alikuwa hajaathirika tangu zamani) au baada ya kugundua matunda ya 'mambo' yake aliyokuwa akiyafanya gizani.... amechanganyikiwa kwa kile alichokisababisha kwenye familia yake.

Wewe tulia kimya ila vituko vikizidi mama ita wazee liwekeni jambo sawa kisha mkapime wote..........askufrustrate wanao bado wadogo ati
 


Ahasante (Pihu)
Mimi kama sijapata kwake basi nitakuwa nilipata kabla ya kuolewa
Huo ndio ukweli wangu ndugu yangu.


Baraka_41 mpendwa.

Sikiliza kwa makini ushauri wa babu.

Nime quote posts zako zote ili kuunganisha mtiririko wa matukio ya kisanga hiki.

Nazungumza hapa kama mwanaume ambaye nazijua vema tabia zetu wanaume. Nazungumza pia kama mme wa bibi yenu ambaye ni mdau mkubwa katika masuala haya ya HIV/AIDS.. Huwa ananiambiaga visa vya kushangaza na kusikitisha sana.

Kama ulichokiandika hapa na kukiri kwa nafsi na mbele za Mungu kuwa ni ukweli mtupu basi:
1. Mume wako ameathirika na VVU ala anakuficha
2. Ndiye aliyekuambukiza VVU, ila anajaribu kukimbia kivuli chake
3. Anakutafutia sababu akufanyie kitu kibaya

Babu anakushauri, chukua tahadhari. Usikubali kuwa anakupenda kivile. Kwa mtu kama huyu, best option anayoiona babu ni kutengana naye. Kama anadiriki kukuficha ukweli na kukufanyia visa kama hivyo, iko siku atakushangaza kwa kubwa zaidi. ...Unarudi toka kazini unakuta nyumba ina watu wengine kabisaaaaa! Imeshauzwa.

Anywa, pole sana ndugu yangu. Ila maisha lazima yasonge mbele. Ishi kwa matumaini, zingatia masharti ya madaktari, mwombe Mungu akusaidie kuukabili huu mtihani....

Amini amini nakuambia, muda si mrefu dawa itapatikana.

Mungu akubariki sana.

Babu anarudi kitandani.
 

Aksante sana babu.
 
Mungu aendelee kuwalinda na kutunza kwa rehema na baraka zake
pendaneni
 

Babu nashukuru sana kwa ushauri wako , leo tena maekuja na uamuzi mwingine kuwa hatatoa talaka ila tutatengana na yeye takuwa na chumba chake na baadae ataondoka ila pale nyumbani ataacha chumba chake ambapo atakuja wakati wowowte atakapotaka.

Vile vile alisisistiza nikampime mtoto na namshukuru mwenyezi mungu nilikuwa naogopa sana kwenda kumpima mtoto lakini nimeenda kumpima na majibu ni Negative Nilishukuru sana kwa hilo.

Sasa jana anasema amemwambia mtoto kuwa yeye ataondoka pale nyumbani nasikia mtoto alilia sana.
 
inaonyesha anamshaur mbaya sana au jana wakat anaongea na wewe inaonyesha alikuwa anadubai kichwan na alipo amka asubuhi akakumbuka akawa bado anahang over hvyo alikuwa hajijui ila pia na wewe kuwa na msimamo utamuona mwenyewe anarud kwenye mstari usiyumbishwe na tena kama mmezaa na kama mnachangia maisha yan ninamaana wewe unaudumia familia pia acha jifanye hunapesa na hulet pesa uone atasemaje huyo mumeo ni limbuken na anaemshaur itakuwaje
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…