Naomba ushauri wenu wana JF


Nakuombea kwa Mungu wa kuwa........amani yake ipitayo akili zoooote ikuhifadhi, Mungu akuangazie nuru ya uso wake na kukuongoza katika kipindi hiki kigumu unachopitia. Mungu mwenyewe afanyike faraja na tumaini lako binafsi na familia yako pia (utakapo waambia). Nakupenda dia.........take heart.
 

Mpendwa baraka_41,

Bila kung'ata meno wala ulimi babu amegundua hili:

Mme wako amechanganyikiwa! Yuko confused vibaya. Amepima akakuta ameathirika, na amejua kuwa ni yeye ndie aliyeuleta kwako huu ugonjwa. Vinginevyo angeshakutimua siku nyingi sana.... Sijajua ameenda kupima wapi, ila naamini hakupewa counselling ya nguvu.

Ukweli ni kuwa amechanganyikiwa kwa kuwa HAJAIKUBALI HALI HALISI. HAJAYAKUBALI MATOKEO. Bado ana ile mentality kuwa Ukiwa na maambukizi ya VVU ndo umeshalichungulia kaburi..... namwonea huruma sana. Anahitaji counselling ili ayakubali matokeo na kuendelea na maisha.

Kwa muda huu mpendwa chukua tahadhari, watu wa namna hii hawachelewi kuchukua maamuzi ya kijinga sana.

Babu anazidi kukuombea kwa Mungu, akupe nguvu ya kuukabili huu mtihani mgumu. Naamini utashinda.

Mungu na aendelee kukubariki na kukulinda.

Babu anarudi kitandani.
 

Ahsante sana Babu, nashukuru
 
Pole mpendwa. Nafikiri mumeo anakupenda na asingependa kuona unajihisi vibaya au unakosa raha. Ni jambo la kushukuru na kufurahi.
Pia inawezekana na yeye ameathirika ila hajataka kuwa muwazi kwako.
 
Let me analyse your story as follows;
- Duration of marriage.......13 years!
- First born in the marriage.....12 years!
- Father's second born out of the marriage.....10 years!
- Previous HIV test agreements..... Father NO, Wife YES to visit the HIV test center!
- Situation in test...... Individually!
- HIV test results..... Father negative, Wife positive!
- Duration for discovering HIV results......3years!
- Wife's name ....... Baraka_41!
- Opinions after HIV status discovered......Wife; Divorce, Father; Never divorce!

Questions arising in my minds;
- The father's second born is 10years old, and she is originated out of "ndoa"...! and a wife became HIV positive within marriage and she was affected alone...! Je, uaminifu kwenye ndoa uko wapi?
- If a wife proposed for divorce under the marital status, did she forget the negative effects of divorce to their first-born of 12years?
- Kama haukuwepo uaminifu kwenye ndoa, hii kuathirika kwa mama sio adhabu ya kulipiza kisasi kwa mumewe baada ya kugundua baba ana mtoto nje?
- How comes the name of the woman to be "Baraka"?
- Kwanini baba ameamua kwenda kupima mwenyewe sasa? Huo ujasiri kautoa wapi?
- Mbona mama mwenyewe hana uhakika kama ugonjwa huu kaupata wapi? Au vituo vimekuwa vingi?


My stand;
I guess that this story is cooked and not real.....! Otherwise, huenda hata baba ameathirika.....!
 
Pole sana kwa yote yanayokukuta
zidi kumwomba Mungu hatakuacha kipindi hiki kigumu katika maisha yako.
kuna familia moja mke aliugua kwa muda mwisho akaamua kupima majibu yalikuwa Positive
mume akamtia moyo maisha yakaendelea kumbe yule mume alikuwa amepima siku nyingi na aligundua
ni positive akaanza kutumia dawa bila kumshirikisha mkewe matokeo yake yule mama ameshafariki baba
anaendelea kudunda.
inawezekana mumeo alishagundua hilo mapema bila wewe kujua anatumia dawa kwa siri
na kitendo cha wewe kwenda kupima na kujua ukweli ndicho kinachomchanganya.
jipe moyo yatapita unamaisha marefu yakuendelea kulea familia yako



 

Bibi mzuri sana wewe!
 
Nenda mahakamani, huko utapata haki zako zote!
 
Mheshimiwa SharpCorner heshima mbele na salamu

Hapo kwenye red, kuna kosa gani kwa huyu mama aliyeathirika kujiita baraka_41? Tatizo alilo nalo na jina baraka kuna mashaka gani?...Nikuulize wewe ulivyojiita konakali, ulikuwa unamaanisha nini?...Sidhani kama jina lina uhusiano na mada inayozungumziwa hapa.

Hapo kwenye blue, hata mi niliingiwa na mashaka na kuhisi kuna uwezekano huyu mama aliamua kulipiza kisasi baada ya baba kumletea mtoto wa nje. Lakini nilisita kukonkludi hivyo bila kujihakikishia.....(hakuna kitu kibaya maishani mwangu na nachokiogopa kama kuhukumu).... Hatimaye mama akaweka hadharani kama nilivyomnukuu hapa chini.

Ahasante (Pihu)
Mimi kama sijapata kwake basi nitakuwa nilipata kabla ya kuolewa
Huo ndio ukweli wangu ndugu yangu.

Mheshimiwa kona kali, bado una mashaka na huyu binadamu mwenzetu?

Babu anarudi kitandani.
 
Kona kali bwana unataka kusema hakuna wanawake wanaoitwa Baraka?? Ntakushangaa sana ukinibishia maana ni wengi ninaowafahamu.
 

Kona kali bwana unataka kusema hakuna wanawake wanaoitwa Baraka?? Ntakushangaa sana ukinibishia maana ni wengi ninaowafahamu.

Wandugu kwa swala la jina ningeomba tusilishikie bango..... hakuna ubishi....! So, let us go on dealing with the situation....! Kama Babu alivyomnukuu mhusika kuhusu anavyohisi alivyopatia ajali basi binafsi nazidi kuamini kuwa huenda mwanaume ndio kamletea..... na ndio maana nimehoji ujasiri wa huyo mwanaume kwa sasa kwenda kupima tena bila kuhitaji company......!
 

Kweli kabisa huo mtazamo kama wako nadhani unawezakuwa ndio picha halisi. Ila tu hiyo reaction ya shemeji inanitisha ninaomba dada Baraka_41 uwe mwangalifu kwa kila move.......akiwa nicer to you usibweteke na kuamini kuwa amerudi kwenye senses zake inawezekana kuwa ni mtego.anaweza hata kukutilia sumu na yeye kujimaliza .........out of frustration. Just kuwa makini
 
Nawashukuru wote kwa ushauri wenu mzuri, nawashukuru sana na mmenipa moyo sana maana mwanzo nilikuwa nimechanganyikiwa sana, Kwa sasa mimi nipo namsikiliza atakachoamua then nitajua la kufanya kulingana na maamuzi yake.

Mwenyezi mungu awabariki sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…