Naomba ushuhuda kwa watu waliokuza mitaji yao kupitia vikoba

Naomba ushuhuda kwa watu waliokuza mitaji yao kupitia vikoba

Wakuu salama.
Kuna watu wamekuwa wakinishiwashi niingie kwenye vikoba kuwa ntapata mikopo yakukuzia biashara. Nilikuwa naomba watu waliofanikiwa kukuza mitaji kupitia vikoba wanieleze kwa undani, maana hawa wanaonishauri niingie wananiambia faida za vikoba tu ni kiwauliza hasara zake ni nini hawaniambii.

Mimi binafsi ni mwanafunzi chuo wa mwaka wa mwisho, lakini nimebahatika kuajiri watu wanne, wawili kwenye saluni barbershop, mmoja kwenye banda la mpira na mwingine kwenye mchele lakini nilihitaji nikuze mtaji zaidi. Sasa nashawishika kuingia kwenye vikoba ingawa akili yangu pia inasita.

Naombeni ushuhuda kwa waliofanikiwa.

Kiongoz,

kwanza naomba nikupongeze kwa kujitambua..Maana vijana wengi wa chuo huwa wanasubili ajiri ambazo hazipo.

Pili, VICOBA(Village community banking) ni nini,? Ni mkusanyiko wa watu kuanzia 15 mpaka 30 WANAOFAHAMIANA mostly ni wajasiliamali wadogo, wenye lengo la kukuza mitaji kupitia kipato chao wenyewe au vyanzo vingine.

Cha kwanza lazima ufahamu aina ya watu walio kwenye hicho kikoba ilikujua kama mtakopeshana wote mna mna uwezo wa kurejesha mikopo hata ikitokea mmoja wenu ameshindwa basi mjue jinsi ya kumpata aweze kurejesha mkopo wake.

Mwisho lakini sio kwa umuhimu..Kwa upande wako kulingana na maelezo VICOBA is the best place kukuza mtaji wako kama utazingatia tuu hayo mambo muhimi. Mimi nko kwenye vikoba aina tatu tofauti na naona jinsi ambovyo inanisadia zaid hata nilivyokuwa nafikili.

Ni hayo tuuu kwangu mkuu.
 
Asante kiongozi.
 
Raha ya kikoba(nazungumzia kikoba kilichokomaa sio kinachoanza) unaweza kukopa pesa kwa riba ndogo sana ukaongezea kwenye mtaji tofauti na vile ungekopa bank. Mfano kikoba nilichopo Mimi unaweza kukopa hata 5m.wanachama wako vizr kabisa kwenye kuhamasishana juu ya uchakarikaji na usimamizi wa biashara.masharti ya kujiunga hata kama ni mfanyakazi lazima uwe na chanzo kingine cha kipato wanachama wathibitishe ndipo uunngwe.faida nyingine chama kikivunjwa hela inakuwa imeongezeka sababu ya riba ni uwekezaji pia! Hasara zake wanachama wasipokuwa waaminifu unaweza kupoteza hela zako, unaweza kushitakiwa pia kwa kikoba strong ukishindwa kufanya marejesho kwa muda.sababu kuna mkataba lazm ujaze. NB usikurupuke kujiunga kwenye kikoba chochote ni hatari kwa afya yako fanya utafiti kwanza!
Hatari kwa afya kivipi tena ndugu? Nifafanulie hapo tafadhali
 
Hatari kwa afya kivipi tena ndugu? Nifafanulie hapo tafadhali
Hatari kwa afya kivip? Umewahi kupoteza hela wewe? Umewahi kudhurukiwa hela wewe hadi unapungua uzito,ukosa hamu ya kula,unaongea mwenyewe njiani. Kama haujui waulize wale ambao benk zao zmefungwa na waliweka mamilioni ya hela na saiz wanaambiwa watalipwa 1.5 milion na nyiengne until further notes.
Nirudi kwa mtoa mada pia kama kikoba chenu nikichanga na utanziji wa fedha ni wa mkononi kwa maana hela zinakaa kwa mtunza hazina basi badilisheni huo utaratibu na kuhamia benki. Kwani saiz kukaa na hela ni hatar kwenu wanachama hasa usalama wa fedha zenu. Fungueni akaunt benk mfano nmb wanaakanti maalymu kwa vikundi na vikoba pia. Akaunti ambayo haina gharama za uendeshaji,na inaoption ya kupata atm kadi na usalama fedha zenu ni 100%
 
Kuna vikoba hapa kwanza kila wiki unapiteza 4000, hiyo mnachangia afya, ukiumwa, ukifiwa haiwahusu.

Kukopesheka ni baada ya mwaka km una shida ya haraka ni ngumu kupata...!!!

Utafaidika na vikoba kama unatembeza biashara kule ni kuinuana ukikutana na mwana vikoba mwenzio anakuchangia....!!!
Vicoba ni vzuri kama vitakua na katiba nzuri, hvyo ni vicoba vya kina mama mimi nataka kuanzisha support ya wajasiriamali yan lazima kuwe na Kiingilo kama elf 20,000/= maana ntatoa vtambulisho na vidaftari vya kuandika record kwa kila mwanachama na pia kutakua na ada ya kila mwezi kma elf 10 maana kila mwez tutakua tunafanya kikao cha wanachama wote! Watu watawekeza pesa na kukopa maana ni lazima uwe na mtaji wa kuwa unakopesha na kwenye kukopesha pesa lazima uwe na sheria Kali maana pesa ni shetani na me nitakua nakopesha kwa vikundi na marejesho yatarudi kwa vikundi kama mtu akikimbia wanakikundi watabeba mzgo wake! Format ya vicoba ni nzuri ila me nataka kuidadavua kdg nianzishe yangu ambayo ukishatoa kiingilio ukafanyiwa usajili bas utaweza kukopa na kutakua na viwango vya chini vya kuanzia kukopa mtu akilipa anapanda kiwango
 
Yea nipo mwaka wa mwisho wa nne,mchele bado nauza nilifungua frem nauzia kwenye frem ingawa pia nasambaza,banda la Mpira bado lipo pia nimefungua kisaluni cha kiume.

Sasa kuna watu wananishauri niingie kwenye vikoba,nilitaka nifahamu na ubaya wake pia.
chief vp ......naomba unipe mwongozo nataman kufungua banda tiyari nina sumsung 32inc projector nmebakiza kidogo bla shaka
 
Vikoba ni vizuri kwa watu mnaofahamiana wanaweza kua wajasiriamali wenzako au wafanyakazi.hii itarahisisha ifatiliaji wa hisa na ulipaji wa madeni.mimi kuna vikoba nimefaidika navyo na vingine nimepata hasara.nitaeleza hasara niliopata.mwaka jana nilitaka kuanza ujenzi nikaona ni vizuri nianze kiwekeza kwene vikoba nikatafuta ambacho niliona kinafaa sehemu nilipo nikajiunga nikaweka hisa zenye thamani ya 1.3 million kwa muda wa miezi minne ile nataka kukopa nikaambiwa hela hakuna nikasubiri mwezi mwingine nikaambiwa maneno hayo hayo na mhasibu ikabidi nistop kununua hisa nifatilie nikagundua wenzangu hawanunui hisa na madeni walonayo hawalipi.na viongozi wanamadeni makubwa wanashindwa kuyalipa hivo hata ufatiliaji haufanyiki.hapo ndo nikagundua nimewekeza sehemu inayoelekea kufa.
 
Join the Most trustworthy broker!!!
Templerfx!!!!
- Easy to Deposit your investment capital by Mobile Money Transfer (M-Pesa, Airtel Money) Just less than an hour, your account will be funded.
- Easy to withdraw you money(M-Pesa, Airtel Money) less than an hour your money will be in your phone ready to get from WAKALA!!
-Quick and Easy customer services.

Very Easy to join!!!
Click on the link below open account
TemplerFX | Promo

Kwa wale Wa forex templerfx ni broker mzuri sana kwa mazingira yetu ya bongo , ni rahisi kujisajili lakini pia njia za kutuma na kupokea Pesa yako ni rahisi mno!

Minimum deposit ni $1=Tsh2,240 tu
 
Vikoba kujiunga ni very simple sana tatizo malejesho hapo ndo huwa pana noma kama hela yako ni ya.kuunga unga
But vinasaidia sana maana unapata mkopo kwa liba ndogo
 
Kila Vicoba ina sheria zake. Kwa mfano sisi chetu unaweza kukopa miezi mitatu baada ya kununua hisa na unapewa mkopo mara tatu ya hela uliyoweka. Hasara ni kwamba ukiingia vicoba ya watu wasiowaaminifu utalizwa. Zaidi ya hapo Vicoba ina faida sana
Tatizo mi nachukiaga kasiku kamalejesho kakifika halafu sina hela kuzima cm nashindwa ha ha ha.mhasibu na katibu wanapigaga simu.hizo mpaka kero
 
kuna kikoba flani nilikisia ukichangia million 3, unaweza vuta altezer ya milion 9, riba ndogo kweli,, niko mbioni kujiunga,,

pia wanakopesha hadi viwanja, ukimaliza kujenga ndo unapewa hati,,

kima cha chini kuchangia ni elfu 2,

hao wanachukua watu wa hali zote,,
Hao wako wapi
 
lengo lao ni kuchukua watu wa hali zote, za juu na za chini,,

kila wiki wanakutana, kima cha chini elf 2,

mwenye kipato kidogo anatoa elf 2, so kwa mwezi atakuwa ametoa elf 8,,

kama uko poa unaruhusiwa kutoa zaidi,

unaruhusiwa kukopa ×3 cha ulichochangia,, kama kwa mwezi ulichangia laki 3, basi unaweza kukopa laki 9.

hichi hakibagui kipato,
Hiki nmekpenda kwa hali yangu kitanifaa nielekeze kiko wapi
 
Vicoba ni vzuri kama vitakua na katiba nzuri, hvyo ni vicoba vya kina mama mimi nataka kuanzisha support ya wajasiriamali yan lazima kuwe na Kiingilo kama elf 20,000/= maana ntatoa vtambulisho na vidaftari vya kuandika record kwa kila mwanachama na pia kutakua na ada ya kila mwezi kma elf 10 maana kila mwez tutakua tunafanya kikao cha wanachama wote! Watu watawekeza pesa na kukopa maana ni lazima uwe na mtaji wa kuwa unakopesha na kwenye kukopesha pesa lazima uwe na sheria Kali maana pesa ni shetani na me nitakua nakopesha kwa vikundi na marejesho yatarudi kwa vikundi kama mtu akikimbia wanakikundi watabeba mzgo wake! Format ya vicoba ni nzuri ila me nataka kuidadavua kdg nianzishe yangu ambayo ukishatoa kiingilio ukafanyiwa usajili bas utaweza kukopa na kutakua na viwango vya chini vya kuanzia kukopa mtu akilipa anapanda kiwango
Hivi na sisi wanaume vikoba vinatuhusu
 
Wanaume wa dar ktk ubora wenu mpaka vikoba vya kina mama mmevamia.ha ha ha ha ha
 
Wanaume wa dar ktk ubora wenu mpaka vikoba vya kina mama mmevamia.ha ha ha ha ha
Imebidi nicheke kwa sio kwa furaha bali kwa huzuni.ukichukua mkopo kwenye kikoba riba ni asilimia 10 kwa mwaka.wakati kwenye mabenk riba ni 18%/23%.Sasa ukiona kuwa viloba ni vya kina mama hulazimishwi kujiunga.Lakini mie binafsi kikundi nilichopo kuna vijana 20 na wasichana 10.Sasa kwa ratio hio sijui nichakina mama au wakina baba.
 
Vikundi vya VICOBA vipo ambavyo vinafanya vizuri Sana na watu wamenufaika mno hilo Halina ubishi lkn Kunawatu wanaendesha VICOBA kitapeli huko Mitaani jambo ambalo linaumiza wengi. Mfano hicho unachosemaMs Mol hicho Kikundi kinajiita VICOBA lkn Hakina sifa ya VICOBA Kabisa maana kinajiendesha tofauti. Nashauri tutafute watu wenye uelewa wa kutosha watuelimishe
 
Mh mbn kila kitu ulichosema kinafanana Na kikoba nilichopo?
 
Back
Top Bottom