Naomba utushirikishe mbinu wanazoweza kutumia waliojiriwa kumiliki nyumba ya kwanza

Naomba utushirikishe mbinu wanazoweza kutumia waliojiriwa kumiliki nyumba ya kwanza

Aliko Musa

JF-Expert Member
Joined
Aug 25, 2018
Posts
209
Reaction score
315
Habari,

Naitwa Aliko Musa. Ninaishi mkoani Mbeya. Mimi ni mwandishi na mshauri mbobezi kuhusu uwekezaji katika ardhi na majengo.

Mejesho kutoka kwa wasomaji wa makala zangu kwenye mtandao wa UWEKEZAJI MAJENGO BLOG umeonyesha wengi hushindwa kumiliki ya kwanza kutokana na sababu mbalimbali.

Kwa kuwa mafanikio makubwa yana chanagamoto zake. Na kumiliki nyumba ya kwanza ni moja ya hatua kubwa kuifikia maishani.

Hivyo, ninaomba tushirikishane mbinu mbalimbali zinazoweza kuwasaidia watu walioajiriwa serikalini na taasisi binafsi.

Nimepata wazo hili kwa sababu nimeona wengi wa waajiriwa hawawezi kumudu kununua nyumba au kujenga nyumba zao za kwanza kwa wakati.

Wengine wanafikia hatua mpaka kuchukua mkopo wa watumishi kununua au kujenga nyumba yao ya kwanza.

Waajiriwa wengine wamesubiria pensheni yao kama fedha kwa ajili ya kununua au kujenga nyumba yao ya kwanza wanayoipenda.

Ninaamini wewe unayesoma hapa mawazo yako yanaweza kuwa msaada mkubwa kwetu sote.

Tutaweza kumiliki nyumba ya kwanza, ya pili na kuendelea kwa kutumia mbinu utakazotushirikisha hapa.

Ombi; naomba unishirikishe rafiki yangu. Hakika utakuwa umetusaidia sana rafiki yetu.

ZAWADI YA KITABU; Njia 120 Za Kutengeneza Fedha Kwenye Ardhi Na Majengo.

Kwa mchangiaji ambaye ataonyesha ushirikiano mzuri nitampatia zawadi ya kitabu hiki.

Ushirikiano wake utaonekana kwenye maoni chini ya makala hii. Yeyote atakaye kuwa na moyo wa kujali na kutoa mbinu bora atapata kitabu.

Rafiki yako,
Aliko Musa.
WhatsApp/calls: +255 752 413 711
 
Kwa ufupi unahitaji contents za kitabu chako ambacho hakijakamilika.

Kama muandishi na rafiki etu tupe muongozo wa uzoefu wako katika hili ili sisi marafiki zako tuanzie hapo kushauri.
 
kwa ufupi unahitaji contents za kitabu chako ambacho hakijakamilika...

kama muandishi na rafiki etu tupe muongozo wa uzoefu wako katika hili ili sisi marafiki zako tuanzie hapo kushauri.

Rafiki yangu nimeandika zaidi ya njia 30 kwenye mtandao wa UWEKEZAJI MAJENGO BLOG.

Ndio maana leo nimependa kusikia kutoka kwako wewe msomaji wa makala zangu ninazokushirikisha kupitia mtandao huo UWEKEZAJI MAJENGO BLOG.

Kuhusu kitabu sijakuelewa una maana gani?.

Karibu sana rafiki yangu.
 
Mimi nahisi huenda unahitaji hizo njia katika kusaidia umaliziaji wa kitabu chako kama jamaa alivyosema, weka link hapa tuone pia yale usemayo umekwisha yaandika
 
Back
Top Bottom