Habari za asubuhi wakuu??
Kama mwezi mmoja ulopita niliandika kuhusu kuomba uzoefu kuhusu Honda Fit ("UZOEFU KUHUSU HONDA FIT" Hii ndo ilikia title ya thread yangu)
Nashukuru sana wadau walijitokeza na kushare (you can reffer).
Lile gari nili liagiza kupitia SBT Gharama zake zilikua kama ifuatavyo.
Bei ya kununua $ 1,390
Bank Charges $ 60
Total CIF1,450
TRA 3,882,566
Bandarini 640,000
Agent fee 200,000
Approx. Total 7.9 Mill
Mchakato wote ulikua vizuri bila shida yoyote (Nawapongeza SBT kwa huduma yao bora)
Gari nimelichukua jana nikaenda nalo kwa fundi wangu, nikamwambia fundi nimeandaa kama 1.5 mill kwa ajiri ya kurekebisha hili gari, naomba uliendeshe uniambie lina tatizo gani kabla sijaingia nalo mtaani.
Fundi ali test gari akazunguka nayo ile mitaa ya kwa kakobe mwenge, alivyorudi akaniambia kaka, gari halina shida yoyote isipokua kufanya service tu.
Tutamwaga oili na kubadirisha filter na kufanya air cleaner. Akanishauri nibadiri matairi niweke makubwa kidogo au nilipandishe juu kidogo.
Gari linasoma limetembea km 46,000. Kwakweli nime wafurahia honda japo ndo kwanza leo siku ya tatu toka naliendeaha, sijajuta.
Mafuta nimeweka full tank, but bado sijafika katikati na unajua ukiwa na gari jipya unavyo washwa washwa kutembea nalo.
Naomba nimalize kwa kusema hivi
ASANTENI KWA USHAURI WENU NIMEPATA GARI ZURI KWA BUDGET YANGU NDOGO.
ASANTE JF.
Karibuni.
PIA SOMA:
- Naomba uzoefu kuhusu honda fit