Naomba uzoefu kuhusu Honda Fit

Naomba uzoefu kuhusu Honda Fit

Wakuu nimerudi tena baada ya kimya kirefu....
Nimeagiza honda Fit ya mwaka 2004 kupitua SBT Japan sasa n wiki ya pili.... Kila kitu kinaenda sawa
Naomba kuuliza wazoefu wq clearing and forwarding, kama kuna mtu anafanya hii kitu au anamjua anaeweza kunifanyia kwa bei nafuu.
Nimesikia wale wa SBT wana bei kubwa sana, na vyuma vimekaza sana.
Tupe mrejesho kama mkoko umeishafika Dar na uaminifu wa SBT pia
 
Mkuu nipe maujanjaujanja, mbona mie kila nikipita Beforward na SBT Japan naona gharama kwa honda inakita 1900 USD (Plus CIF Inspection) ?
Best Value Used HONDA cars for Sale | BE FORWARD
Ukisha penda gari unafanya negotiation mfano kama hiyo ya 1,900 inaweza kushuka hadi 1,600...
Alafu ukiwa unasearch unaangalia pale kwenye sale, best price, auction, au discount. Ndo utakuta magari ya bei poa, sema hua hayakai ko nikubahatisha.
 
Tupieni hata picha ya Honda Fit
IMG-20171030-WA0074.jpg
IMG-20171030-WA0073.jpg
IMG-20171030-WA0070.jpg
IMG-20171030-WA0071.jpg
 
Kama bado unahitaji, check with Me asap!
Mkuu nahitaji IST nzuri ya kuanzia mwaka 2005 nakuendelea km sio zaidi ya 80,000...
Bajeti yangu n 10 mil vipi ntapata?
 
Habari za asubuhi wakuu??
Kama mwezi mmoja ulopita niliandika kuhusu kuomba uzoefu kuhusu Honda Fit ("UZOEFU KUHUSU HONDA FIT" Hii ndo ilikia title ya thread yangu)

Nashukuru sana wadau walijitokeza na kushare (you can reffer).

Lile gari nili liagiza kupitia SBT Gharama zake zilikua kama ifuatavyo.

Bei ya kununua $ 1,390
Bank Charges $ 60
Total CIF1,450

TRA 3,882,566
Bandarini 640,000
Agent fee 200,000

Approx. Total 7.9 Mill

Mchakato wote ulikua vizuri bila shida yoyote (Nawapongeza SBT kwa huduma yao bora)

Gari nimelichukua jana nikaenda nalo kwa fundi wangu, nikamwambia fundi nimeandaa kama 1.5 mill kwa ajiri ya kurekebisha hili gari, naomba uliendeshe uniambie lina tatizo gani kabla sijaingia nalo mtaani.

Fundi ali test gari akazunguka nayo ile mitaa ya kwa kakobe mwenge, alivyorudi akaniambia kaka, gari halina shida yoyote isipokua kufanya service tu.

Tutamwaga oili na kubadirisha filter na kufanya air cleaner. Akanishauri nibadiri matairi niweke makubwa kidogo au nilipandishe juu kidogo.

Gari linasoma limetembea km 46,000. Kwakweli nime wafurahia honda japo ndo kwanza leo siku ya tatu toka naliendeaha, sijajuta.
Mafuta nimeweka full tank, but bado sijafika katikati na unajua ukiwa na gari jipya unavyo washwa washwa kutembea nalo.

Naomba nimalize kwa kusema hivi
ASANTENI KWA USHAURI WENU NIMEPATA GARI ZURI KWA BUDGET YANGU NDOGO.
ASANTE JF.
Karibuni.

PIA SOMA:
- Naomba uzoefu kuhusu honda fit
 
Honda wana magari Mazuri... Miaka tisa iliyopita nilikuwa na gari ya Honda.. Nilikuwa napepea balaa!
 
Back
Top Bottom