Naomba uzoefu wa kuangalia mechi ya Simba na Yanga

Naomba uzoefu wa kuangalia mechi ya Simba na Yanga

g4cool

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2012
Posts
429
Reaction score
206
Wakuu ni kwa mara ya kwanza nataka kwenda kuangalia mechi ya Simba na Yanga taifa na, sijawahi kabisa kuangalia mechi hapo, so ningeomba kupata experience juu ya

1. Natoka mkoani, jinsi ya kulipia tiketi inakuwaje?
2. Nakuja na watoto, miaka 8, 6 na wa miaka miwili, je VIP itakuwa chaguo zuri?
3. Mechi ni saa moja usiku, angalau muda gani natakiwa niwe nimeshaingia ili kuepusha msongamano? (Kama upo)
4. Nasikia mechi za usiku kunakuwa na tabia za wizi sana je ni kweli?

Na ushauri gan unaweza nipa

Shukrani
 
NUNUA TIKETI MAPEMA KUEPUSHA USUMBUFU WA KIMTANDAO

KAMA HUNA MAMBO MENGI, WAHI NAFASI MAPEMA ANGALAU SAA 9 KUELEKEA SAA 10

TICKET ZINANUNULIWA KIMTANDAO KUPITIA KADI (N CARD)

WIZI UPO NA VIBAKA KUWA MAKINI, KUWA MAKINI

Kama una watoto wengi, wapumzishe kwanza maana sometimes vurugu ikitokea kupoteana kupo
 
Wakuu ni kwa mara ya kwanza nataka kwenda kuangalia mechi ya Simba na Yanga taifa na, sijawahi kabisa kuangalia mechi hapo, so ningeomba kupata experience juu ya

1. Natoka mkoani, jinsi ya kulipia tiketi inakuwaje?
2. Nakuja na watoto, miaka 8, 6 na wa miaka miwili, je VIP itakuwa chaguo zuri?
3. Mechi ni saa moja usiku, angalau muda gani natakiwa niwe nimeshaingia ili kuepusha msongamano? (Kama upo)
4. Nasikia mechi za usiku kunakuwa na tabia za wizi sana je ni kweli?

Na ushauri gan unaweza nipa

Shukrani
Mkuu kwa hiyo familia ulionayo binafsi naona uangalie kwa runinga tu mana varangati la jmosi sio dogo.
 
Wakuu ni kwa mara ya kwanza nataka kwenda kuangalia mechi ya Simba na Yanga taifa na, sijawahi kabisa kuangalia mechi hapo, so ningeomba kupata experience juu ya

1. Natoka mkoani, jinsi ya kulipia tiketi inakuwaje?
2. Nakuja na watoto, miaka 8, 6 na wa miaka miwili, je VIP itakuwa chaguo zuri?
3. Mechi ni saa moja usiku, angalau muda gani natakiwa niwe nimeshaingia ili kuepusha msongamano? (Kama upo)
4. Nasikia mechi za usiku kunakuwa na tabia za wizi sana je ni kweli?

Na ushauri gan unaweza nipa

Shukrani
Usiende kuvunja viti.Nenda Saa tatu asubuhi,paki mbali na uwanja kwenye parking za kulipia.Usiwahi kutoka uwanjani mechi ikiisha au undone kabla mechi haijaisha. Kaa jukwaa la timu unayoshabikia.
 
Angalia tu hom boss mana mpila unachezwa usiku na upo na watoto ungekuwa mwenyewe sawa
 
Ukifika taifa simu uishike mkononi mpaka unaingia ndani halafu kama ww ni yanga lakini una rafiki yako ni simba anakwambia mkakae jukwaa la simba na mmevaa mijezi team yako ikishinda hapo jiandae kisaikolojia maana unaweza kudundwa na mashabiki wenye hasira kali.
 
Mnaosema aangalie home sijui kama mmemuelewa mleta mada.
1. AMETOKA MKOANI (TAYARI YUKO MJINI)
2. DHAMIRA YAKE NI KUINGIA UWANJANI (AMEANGALIA MECHI NYINGI KWENYE TV)

Ushauri wangu.

1. Tambua Jukwaa lako mapema kama ni SIMBA nenda upande ambao wanakaa SIMBA na kama ni YANGA nenda upande wa Yanga.

2. Nunua tiketi yako mapema ili kuondoa usumbufu na kuuziwa tiketi za mchongo.

3. Kaa upande ambao wachezaji hutokea, hili jukwaa ni Salama zaidi maana kuna ulinzi wa kutosha kutokana na wageni waalikwa mbalimbali.

4. Nenda na watoto wawili tu, na hakikisha wanakaa na ww muda wote, kama una mke, ndugu au jamaa nashauri uongozane nae hasa akusaidie kuangalia hao watoto.

5. Uendapo uwanjani hakikisha pesa umeweka mifuko tofauti, ukiweza tenga hata buku 10 kwenye soksi za viatu, likitokea la kutokea usikose nauli ya kurudia home.

6. Kama una gari nenda nalo na tafuta sehemu nzuri ulipark hasa upande ule wa DUCE, ambako hakuna wahuni wengi kama kulivyo uelekeo wa TMK.

7. Jiepushe sana kuisema vibaya timu yako, hata kama inacheza vibaya wewe jitahidi kutoongea vibaya, kuna mashabiki hawana akili uwanjani na ukijaribu kukosoa wanakuona ww sio mwenzao unaweza hatarisha maisha yako bure na hasa watoto wako.

8. Wahi mapema uwanjani, masaa mawili kabla ya game ingia uwanjani na utafute nafasi nzuri zaidi kukaa na watoto wako.

Mwisho nikutakie mchezo mwema, na utambue nchi yetu ni salama na kwa kiasi kikubwa hali inakuwa shwari hadi mitaani.
 
Back
Top Bottom