Naomba uzoefu wa kuangalia mechi ya Simba na Yanga

Naomba uzoefu wa kuangalia mechi ya Simba na Yanga

Nashauri usiende na watoto uwanjani, sehemu za mikusanyiko hivo si nzuri sana hasa ukiwa na watoto.
 
Ukifika taifa simu uishike mkononi mpaka unaingia ndani halafu kama ww ni yanga lakini una rafiki yako ni simba anakwambia mkakae jukwaa la simba na mmevaa mijezi team yako ikishinda hapo jiandae kisaikolojia maana unaweza kudundwa na mashabiki wenye hasira kali.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kwa uzoefu wangu kwa vile ni mara ya kwanza nenda peke yako, kama itabidi fika kuanzia saa sita mchana na nunua tickets za VIP kwa ajili una watoto ,kama ni mzunguko make sura wote mmevaa jezi ya timu moja na kukaa jukwaa la timu yenu ,usivae jezi tofauti na watoto ,si watoto Simba we Yanga au mojawapo Simba huyu Yanga halafu unajichanganya kwenye jukwaa ,mtavuliwa jezi kwa lazima na kipigo juu.

Nenda mwenyewe kwa mara ya kwanza,au angalia kwenye tv mpira ukiisha utashukuru,usiende taifa na watoto kama huna usafiri binafsi maana wakati wa kurudi ni purukushaani balaa
 
Hapana wee naogopa aseeeeh, nilipigwa kofi kule sitaki tena, [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Sasa unapigwa kofi shemeji alikuwa wapi🤔🤔🤔🤔🤔
 
Shukran wakuu, nimecancel, nitawapeleka tu sehemu wakaangalie kwa tv
Usiwanyime hiyo nafasi watoto. Fanya hivi

1. Wahi kuingia uwanjani, hakikisha mida ya saa 9 kamili unakuwa uwanjani sababu una watoto watatu. Mida ya saa 9 kunakuwa hakuna msongamano kabisa, sio pale kuingia getini wala ndani ya uwanjani.

2. Mpira ukiisha tu, subiri watu waondoke, hasa timu iliyofungwa, wakiondoka kabisa na wewe toka na wanao, hapa kunakuwa hakuna msongamano kabisa. Au kama timu unayoshabikia imechukua kombe, usisubiri mpaka ushuhudie kombe. Timu ilofungwa ukiona mashabiki wake woooote wametoka, na wewe unga safar na wanao mrudi.

3. Tiketi kata kwa njia ya Tigopesa au MPESA. Mimi mwenyewe kesho naingia na wife na dogo ana miaka 10. Wife au mimi ningekusaidia kuingia na mtoto mmoja.

Mm na familia yangu sote ni YANGA.

Nipo tayari kukusaidia pale ninapoweza, karibu sana mkuu, tutakaa hata sehemu moja pia.
 
Back
Top Bottom