sometimes nawaza kumchangia lakini moyo unasita kutokana na sababu zifuatazo.
1. Unga kala mwenyewe baada ya kuwa limbukeni wa ela anazopata. Kawa hashauriki na mtu kama kawaida ya watanzania akishapata kila anayemshauri asipotee basi machoni pake uwa ni mwenye wivu au snitch.
2. Kuna watanzania wana matatizo makubwa tena ambayo siyo ya kujitaftia lakini sijaona watu mkijitolea kuwasaidia. Nenda muhimbili kuna watanzania wana magonjwa ya ajabu wanahitaji pesa japo mil 1 wameshindwa kupata matibabu wanateseka lakini hawajasaidiwa na mtu. Nenda mtaani kuna watoto yatima, kuna wajane waliodhurumiwa wanahitaji japo msaada wa kisheria lakini hawajasaidiwa hapo mimi ndipo nashindwa kumsaidia ray c.
3. Akisaidiwa ray c kesho atakuja lord eyes naye teja jamani tumsaidie, atafuata TID ambaye ni wazi naye ni mla unga lakini leo hii ukimsema utaishia kuporomoshewa matusi yasiyo andikika na utaitwa snitch. Hapo huja mtaja Ngwair na wengine wengi ambao bila shaka leo hii wanaona effects na matatizo wanayo pata wenzao lakini wao wamekaa kwa kujiona wajanja.
Si muda mrefu TID atafuata maana ukikaa naye mazungumzo yake ni illusions anaongea vitu kama mtoto mdogo.
Mwisho watakao mchangia mchangieni na Mungu atawalipa kwa wema wenu ila mimi ni afadhali ela yangu nkanunue kiroba cha unga nipeleke kwa watoto yatima kuliko kumchangia mtu ambaye leo hii anaomba mchango kisa alitumia ela nyingi kununua hayo matatizo.