Naombeni elimu juu ya upima wa shinikizo la damu

Naombeni elimu juu ya upima wa shinikizo la damu

kwisha

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2021
Posts
1,779
Reaction score
4,982
Naombeni elimu jinsi ya kupima shinikizo la damu

Nyumbani mzee wangu alinunua kifaa chake cha kupima presha

Siku moja Nikapima na mimi

Cha ajabu nikakuta shinikizo la damu kwangu lipo kwenye 151/77

Nakapima Tena mara ya pili likawa lipo kwenye 133/ 80

Sasa imekuwa tabia yangu ya kupima kila siku asubuhi na jioni

Kinacho ni Shangaza nikipima mara ya kwanza shinikizo la damu linakuwa liko juu nikitulia kama dakika 5 nikipima Tena linakuwa liko chini

Sasa na shindwa kuelewa nikubali lipi apo na je wanapima mara ngapi ili kudhibitisha kama una shinikizo au hauna
 
Hii ni kawaida sana, mala nyingi pressure inakua juu ukiwa hujatulia. Mfano ukiwa umetoka kupanda ngazi za gorofa 4 na ukapima pressure wakati huohuo, lazima itakuwa juu.Lakinj ukipimzika Kwa dakika kadhaa halafu ukapima, utakuta ipo chini.
 
Naombeni elimu jinsi ya kupima shinikizo la damu
Nyumbani mzee wangu alinunua kifaa chake cha kupima presha
Siku moja Nikapima na mimi
Cha ajabu nikakuta shinikizo la damu kwangu lipo kwenye 151/77
Nakapima Tena mara ya pili likawa lipo kwenye 133/ 80
Sasa imekuwa tabia yangu ya kupima kila siku asubuhi na jioni
Kinacho ni Shangaza nikipima mara ya kwanza shinikizo la damu linakuwa liko juu nikitulia kama dakika 5 nikipima Tena linakuwa liko chini
Sasa na shindwa kuelewa nikubali lipi apo na je wanapima mara ngapi ili kudhibitisha kama una shinikizo au hauna
Kwanza unatakiwa ujue kama kifaa unachotumia hakina shida mfano shida ya betri.
Pili unatakiwa ujue hali ya kawaida ya pressure(shinikizo la damu) ni ngapi?
Unatakiwa upime ukiwa umetulia, umerelax na mkono uwe una pa kuegemea.. Mfano, kupima ukiwa umekaa kwenye kiti ni vixuri zaid kuliko ukiwa kwenye kochi,hauna mkojo, haujanywa vinywaji vyenye caffeine.. nk
Pia upime sehemu sahihi juu ya kiwiko cha mkono na cuff ikaze vizuri ili kupata matokeo sahihi.
Usipime juu ya nguo..
Unaweza kurudia baada ya dakika moja kuangalia kama majibu ya mwanzo na ya pili ni sahihi.
Fanya muendelezo wa kupima asubuhi na jioni kwa wiki mbili hadi mwezi, utakuwa na uhakika wa hali yako na kumuona daktari juu ya shida yako, kama ipo. 🤗
 
Kama ni mywa pombe kali lazima presha iwe juu muda wote
 
Back
Top Bottom