Naombeni hekima zenu; Natafuta mtoto na mke wangu hajafanikiwa kubeba ujauzito

Loading failed

JF-Expert Member
Joined
Sep 14, 2023
Posts
2,603
Reaction score
7,501
Ndugu wana Jf natumaini mko salama ndugu zangu.

Ndugu zangu katika vipindi vilivyopita ijulikane nilikua natafuta mke na Mwenyezi Mungu amenijalia nimepata mke na nimeoa.

Ndugu zangu mimi na huyu mke wangu tulikua tunatafuta mtoto katika siku zake tulizo amini ni siku za hatari ila cha ajabu mimba haijatunga na sasa kaona siku zake tena.

Nb; Hapo nyuma . Wakati tupo kwenye mahusiano miezi kadhaa kabla sijaamua kumweka ndani nilinza kufatilia mzunguko wake na ulikua kama ifuatavyo;-

i....Tarehe 28/5 aliingia kwenye siku zake na akamaliza tarehe 2/6

ii....mwingine uliingia tarehe 22/6 akamaliza 26/6

iii...pia aliingia mwingine ulifata tarehe 17/7 akamaliza 21/7 na huu nilikua nimesha muweka ndani ( huu mzunguko wa tarehe 17/7 nilikua teyari nimemuoa)

Hivyo tuliafikiana kutafuta mtoto na yeye aliridhia kwa dhati kubeba ujauzito

Tulianza kukutana kimwili

Tarehe 24-hadi28 , na tare 29-tukapumzika . Tukaendelea tena tarehe 30-31/7 na tarehe 1/ 8 tukakutana tena kimwili na siku zote hizo zilikua tunakutana usiku nikitoka kazini na nilikua na mwagia mbegu zangu ndani ili apate ujauzito tuwe na mtoto wetu

Cha ajabu leo tarehe 11/8 ameingia kwenye siku zake na hii ina ashiria ni kweli mimba haitunga maana pia baada ya week moja nilimpima mimba na akaonekana hana mimba japo alikua anahisi kichefuchefu sana, chuchu kuuma sana ukizishika , maziwa kujaa isivyo kawaida yake na wakati mwingine uchovu kupita kiasi, ila tukajisemea tusiamini vipimo ngoja tuone mzunguko wake kama utaonekana na kweli mzunguko umewadia.

katika kipindi hicho tulipo kua tunatafuta mtoto dawa alizo wahi kutumi ni

*Diclopa
*Amoxilin
*Paracetamol

Ndugu zangu..

Nipo hapa ndugu zangu kuomba hekima zenu na utaalamu kwa wanaojua

a) Najiuliza hii inawezekana vipi wakuu au ni mimi nilizidisha kipimo pale nilipokua nampanda ili abebe ujauzito?

b) Je, au ni hatukujua siku na saa exactly ya kukutana ili yeye atunge mimba , ?

c) kama jibu ni ndiyo katika kipengele (b) je ilipaswa tukutanaje na kwa utaratibu gani/ muda gani ili aweze kutunga mimba?

Natanguliza shukrani za dhati sana
 
Jinga kweli 😂 , fanyeni kazi mimba itakuja tu. Fanya mapenzi zaidi katika siku za hatari siku ya 9-12 kwa kutafuta mtoto wa kike siku 13-16 kutafuta mtoto wa kiume. NB kufanya mapenzi kila siku kunapunguza uwezekano wa kubeba ujauzito. Ikiwa mtapitisha mwaka nendeni mfanyiwe vipimo wawili
 
Mbona ni kwa kipindi kifupi sana jomba tayari umeanza kulialia hashiki mimba?. Kamua hata mwaka ndio uanze kuhangaikia. Halafu mbona unasema hashiki mimba?. Je kama tatizo ni wewe?. Siku hizi wanaume wengi wana matatizo hayo. Usianze kumshushia lawama mtoto wa watu il-hali hamjahakikisha nani mwenye shida.
 
Back
Top Bottom