Naombeni hekima zenu; Natafuta mtoto na mke wangu hajafanikiwa kubeba ujauzito
dogo acha ujinga, yani mwezi mmoja tu unaleta mpaka andiko huku?
mdogo wangu pumzika, tulia na endelea na mishe zao, wewe na mkeo hamtafuti mtoto ila umeamua kukera tu watu hapa,

kikawaida ukimaliza mwaka na mkeo, na bado hajashika mimba inashauriwa uanze kufuatilia tatizo ni nini, pamoja na kwenda kucheki afya na vipimo vingine hospitali,

kuna watu ndoa zina miaka 5+ hawana watoto, wakiona andiko lako hili watashangaa sana
 
Ndugu wana Jf natumaini mko salama ndugu zangu.

Ndugu zangu katika vipindi vilivyopita ijulikane nilikua natafuta mke na Mwenyezi Mungu amenijalia nimepata mke na nimeoa.

Ndugu zangu mimi na huyu mke wangu tulikua tunatafuta mtoto katika siku zake tulizo amini ni siku za hatari ila cha ajabu mimba haijatunga na sasa kaona siku zake tena.

Nb; Hapo nyuma . Wakati tupo kwenye mahusiano miezi kadhaa kabla sijaamua kumweka ndani nilinza kufatilia mzunguko wake na ulikua kama ifuatavyo;-

i....Tarehe 28/5 aliingia kwenye siku zake na akamaliza tarehe 2/6

ii....mwingine uliingia tarehe 22/6 akamaliza 26/6

iii...pia aliingia mwingine ulifata tarehe 17/7 akamaliza 21/7 na huu nilikua nimesha muweka ndani ( huu mzunguko wa tarehe 17/7 nilikua teyari nimemuoa)

Hivyo tuliafikiana kutafuta mtoto na yeye aliridhia kwa dhati kubeba ujauzito

Tulianza kukutana kimwili

Tarehe 24-hadi28 , na tare 29-tukapumzika . Tukaendelea tena tarehe 30-31/7 na tarehe 1/ 8 tukakutana tena kimwili na siku zote hizo zilikua tunakutana usiku nikitoka kazini na nilikua na mwagia mbegu zangu ndani ili apate ujauzito tuwe na mtoto wetu

Cha ajabu leo tarehe 11/8 ameingia kwenye siku zake na hii ina ashiria ni kweli mimba haitunga maana pia baada ya week moja nilimpima mimba na akaonekana hana mimba japo alikua anahisi kichefuchefu sana, chuchu kuuma sana ukizishika , maziwa kujaa isivyo kawaida yake na wakati mwingine uchovu kupita kiasi, ila tukajisemea tusiamini vipimo ngoja tuone mzunguko wake kama utaonekana na kweli mzunguko umewadia.

katika kipindi hicho tulipo kua tunatafuta mtoto dawa alizo wahi kutumi ni

*Diclopa
*Amoxilin
*Paracetamol

Ndugu zangu..

Nipo hapa ndugu zangu kuomba hekima zenu na utaalamu kwa wanaojua

a) Najiuliza hii inawezekana vipi wakuu au ni mimi nilizidisha kipimo pale nilipokua nampanda ili abebe ujauzito?

b) Je, au ni hatukujua siku na saa exactly ya kukutana ili yeye atunge mimba , ?

c) kama jibu ni ndiyo katika kipengele (b) je ilipaswa tukutanaje na kwa utaratibu gani/ muda gani ili aweze kutunga mimba?

Natanguliza shukrani za dhati sana
Mnatafuta mtoto wa nini ?
 
Write your reply...Bila kumung'unya maneno wewe utakuwa umefeli tu ... mpe uhuru mke wako akakumbane na marijali ni suala la muda tu utabembeleza mtoto !
 
Back
Top Bottom