Hiyo ya ku-track namba za simu za watu na Location waliyopo achana nayo, watu wanaweza kuitumia kufanya uhalifu, mwishowe ukaingia mgogoro na polisi.
Mimi cha kukushauri, Tengeneza APP maalumu kwa ajili ya watu wanaotafuta Nyumba za kupanga, Nyumba zinazouzwa na Fremu za maduka. Mimi naona kila siku watu wanatembea kwa miguu kutafuta nyumba za kupanga na Fremu za maduka, na wanaouza nyumba nao uangaika... Sasa Tengeneza APP ambayo itakayokuwa inaonesha ramani kama Google Map location, Picha za nyumba, Bei na kadharika... Kama Uber na Bolt wanavyofanya kwenye kukodi usafiri, lakini wewe unatengeneza za wanaotafuta nyumba za kupanga, fremu za maduka na nyumba zinazouzwa... Wewe unadili na REAL ESTATE