Faana
JF-Expert Member
- Dec 12, 2011
- 38,657
- 44,759
Mwaka 2019 January nilimpangisha mtu kwenye nyumba yangu, akaniahidi kunilipa kodi baada ya wiki, nikamkubalia, lakini wiki ilipokwisha hakulipa akaomba alipe mwisho wa mwezi, nikasema sawa.
Kilichoniumiza, mwisho wa mwezi akaenda kwa wapangaji wenzake akawadanganya kuwa nimemtuma akusanye kodi kwa wote aniletee, alipopewa Tshs 3,000,000 akatoroka nazo! Nilipokwenda kufuatilia kodi nikaambiwa alisema nimemtuma akusanye kodi aniletee kumbe mwongo, wapangaji wenzake wakanambia ana wiki hajaonekana na simu yake haipo hewani.
Leo nipo Mikumi, nimeona jina lake kwenye kitabu cha wageni kwenye lodge niliyofikia, ila kwenye hilo jina ameanza na Mchg.
Je, naweza kuwashirikisha wale jamaa wenye kofia bapa? Nawezaje kulifanya hilo bila kujiathiri mwenyewe, maana rb nilisha missplace sikumbuki ilipo.