Naombeni Msaada Niweze kuacha Kamari ya Aviator, Maisha yangu hayaendi vizuri, Kamari hii Inataka kunitoa Roho

Wadau kila mtu ana siri za maisha yake. Mimi kifupi ni mtu mzima nina maisha nimeenda shule na nina njia zakujipatia kipato.
Kifupi nina rafiki yangu daktari alinionesha kwa simu hii kamari ya hili game - Aviator siku moja tukiwa tumepumzika mahali.

Kuanzia siku ile mwaka 2022 mpaka leo maisha yangu yamebadilika. Yaani ni mimi na aviator tu kila pesa nikipata naweka huko na ninaliwa yaani kuna kipindi kwa wiki naliwa si chini ya 3M...

Imagine, yaani najitahidi kuacha lakini siwezi ile uchungu wakupoteza napata kiu kila ninaposhika pesa a naongeza dau na mpaka moyo wangu umekuwa siku hizi kama hauna hisia tena, naweza eka leo 250K ikaliwa ndani ya dakika kumi, nabaki mtupu kuombaomba.

Imefika hatua nataka kuuza mpaka magari yangu ili nicheze Aviator, thanks kea girlfriend wangu anayenishaurigi nisiuze gari ingawa hajui mimi nacheza kamari, yaani hii siri natoa hapa kwenu sijawahi mwambia mtu yeyote.

Kuna saa nawaza nikate eneo a shamba langu niuze ili niweze kurudisha pesa niliyopigwa na mhindi kwenye Aviator maana kwa mwaka toka 2022 napoteza si chini ya milioni 25-35 kwa hesabu za juu juu nilizofanya.

Nawaza kama Aviator ningeijua kabla sijafanya chochote kwenye maisha leo nisingekuwa na kitu chochote, ila hatari iliyopo ni kuwa sasa yaani kwa siku naweza kupata laki tatu nne ila yote inaisha kwa Aviator,

Hakuna hela inakaa mkononi, mpaka inataka kuharibu mahusiano, girlfriend wangu anajua nina uwezo wa kuwa na hela ila kuna wakati anasema inakuwaje nashindwa kumhudumia pesa napeleka wapi ila kumwambia mimi ni teja wa kamari ya Aviator nashindwa naona aibu nazidi kujichimbia kaburi la umasikini mfarakaniko na self denial...

Naombeni maana imenibidi niandike hili baada ya uchungu nimeweka leo jumla ya 400K na mhindi kala yote yaani asubuhi nilikua na 400K mda huu sina hata mia na kuna saa nilipata mpaka 3.6M ila mhindi akairudisha yoooote.

Mazee nimechoka haya maisha naomba mtu aniambie jamani niachaje kamari hiii!? Sitaki haya maisha....
Kuna saa napata hasira balaa ataka mpaka kujidhuru naniuliza nina pepo gani!?

Naomba msaada wa hali na mawazo niweze kuachana na hii kamari ya mchezo wa Aviator.
Uza smartphone baki na kitochi for a while
 
Doh, pole sana kamari sio nzuri kuna jamaa aliuza mpaka nyumba,

Maamuzi ni yako, Anza kuacha taratebu utaweza
Sakata lako na mumeo umelimalizaje? yule dogo wa nje ya ndoa hajambo?
 
shida mimi naona ni hizi 2.

1. Wewe ni mbishi na haukubali kushindwa.

2. Hizo ndoto za kuwa Billionea kwa kupitia Aviator zitoe. kwa sababu ile ni Kompyuta yenye AI.
inacheza na tamaa zako.

baada ya kujua hayo
hebu anza Leo kuaamua kwa

1. kubali kuwa umeshindwa na Aviator ni mjanja zaid yako. na kushindana nae hauwezi.

alaf Hela zipo zinatafutwa. hivyo sahau hela za nyuma na usonge mbele.

2. futa app unayochezea aviator.
na hamu ya kucheza ikija bas tfuta kitu cha kufanya instead.

nina amini unaweza.
Hakika. Nitafata ushauri
 
Aisee itabidi nifanye hivyo ila duh nimejaribu mara kwa mara nashindwa ...tarehe 25/07 mhindi alinipiga balaa 750K nikajiapiza sichezi tena ila nikarudi...
Yaani sijui nifanyaje itabidi niseme hii siri kwa mtu au girlfriend wangu ili aniseme weee nijisikie vibaya
Ukipata hela tu, mpe zote girlfriend wako akuwekee ukiwa na shida uwe unamuomba.
 
Aisee itabidi nifanye hivyo ila duh nimejaribu mara kwa mara nashindwa ...tarehe 25/07 mhindi alinipiga balaa 750K nikajiapiza sichezi tena ila nikarudi...
Yaani sijui nifanyaje itabidi niseme hii siri kwa mtu au girlfriend wangu ili aniseme weee nijisikie vibaya
Jiulize swali hili .... siku ukiwa Huna pesa TACHEZA?
 
Aiseee so roughly umeshapoteza zaidi ya milioni 100 tokea 2022 todate right? Yaani uitafute pesa yote hiyo kwa jasho na damu halafu umpelekee muhindi aliyeko ofisini kwenye kiyoyozi?? Jifunze kufanya maamuzi magumu na kuyasimamia bila kuyumba...anza na hili uza hiyo simu nunua kitochi...
Kaka nishafanya hivyo tatizo ofisini nyumbani kote kuna wifi access na nina laptops tena napenda kucheza kwa computer kuliko simu...
Yaani hapa nataka niamue moja...NIJINYIME ACCESS YA INTERNET KABISA....MAANA HII ONLINE ACCESS NDO INANIFANYA NIWEZE KUINGIA BETSITES NICHEZE NISHAFUNGA AKAUNTI LAKINI NASAJILI LINE MPYA NAJIUNGA TENA MAPAKA NACHOKA
 
Wewe cheza tu ,,,,,! Kama akili yako unashindwa kuicontroo sisi tukusaiedeje ?

Pesa si zako? Unazitafuta mwenyewe huna uchungu nazo, acha upunwe mpaka ubongo
 
Wadau kila mtu ana siri za maisha yake. Mimi kifupi ni mtu mzima nina maisha nimeenda shule na nina njia zakujipatia kipato.
Kifupi nina rafiki yangu daktari alinionesha kwa simu hii kamari ya hili game - Aviator siku moja tukiwa tumepumzika mahali.

Kuanzia siku ile mwaka 2022 mpaka leo maisha yangu yamebadilika. Yaani ni mimi na aviator tu kila pesa nikipata naweka huko na ninaliwa yaani kuna kipindi kwa wiki naliwa si chini ya 3M...

Imagine, yaani najitahidi kuacha lakini siwezi ile uchungu wakupoteza napata kiu kila ninaposhika pesa a naongeza dau na mpaka moyo wangu umekuwa siku hizi kama hauna hisia tena, naweza eka leo 250K ikaliwa ndani ya dakika kumi, nabaki mtupu kuombaomba.

Imefika hatua nataka kuuza mpaka magari yangu ili nicheze Aviator, thanks kea girlfriend wangu anayenishaurigi nisiuze gari ingawa hajui mimi nacheza kamari, yaani hii siri natoa hapa kwenu sijawahi mwambia mtu yeyote.

Kuna saa nawaza nikate eneo a shamba langu niuze ili niweze kurudisha pesa niliyopigwa na mhindi kwenye Aviator maana kwa mwaka toka 2022 napoteza si chini ya milioni 25-35 kwa hesabu za juu juu nilizofanya.

Nawaza kama Aviator ningeijua kabla sijafanya chochote kwenye maisha leo nisingekuwa na kitu chochote, ila hatari iliyopo ni kuwa sasa yaani kwa siku naweza kupata laki tatu nne ila yote inaisha kwa Aviator,

Hakuna hela inakaa mkononi, mpaka inataka kuharibu mahusiano, girlfriend wangu anajua nina uwezo wa kuwa na hela ila kuna wakati anasema inakuwaje nashindwa kumhudumia pesa napeleka wapi ila kumwambia mimi ni teja wa kamari ya Aviator nashindwa naona aibu nazidi kujichimbia kaburi la umasikini mfarakaniko na self denial...

Naombeni maana imenibidi niandike hili baada ya uchungu nimeweka leo jumla ya 400K na mhindi kala yote yaani asubuhi nilikua na 400K mda huu sina hata mia na kuna saa nilipata mpaka 3.6M ila mhindi akairudisha yoooote.

Mazee nimechoka haya maisha naomba mtu aniambie jamani niachaje kamari hiii!? Sitaki haya maisha....
Kuna saa napata hasira balaa ataka mpaka kujidhuru naniuliza nina pepo gani!?

Naomba msaada wa hali na mawazo niweze kuachana na hii kamari ya mchezo wa Aviator.
Changamsha genge huna uwezo wa kupoteza 3M kwa week kijana punguza illusion
 
Wewe cheza tu ,,,,,! Kama akili yako unashindwa kuicontroo sisi tukusaiedeje ?

Pesa si zako? Unazitafuta mwenyewe huna uchungu nazo, acha upunwe mpaka ubongo
Imagine ni mtoto wako kaingia janga hili usiwe na roho mbaya mimi hata maisha siyafurahii nimejieleza ili kama kuna mtu alishayashinda haya niambie na mimi nitoke hapa shimoni
 
Changamsha genge huna uwezo wa kupoteza 3M kwa week kijana punguza illusion
Braza kama ugumu wako wa maisha ni kupata 3M kwa wiki, kuna watu ugumu wetu ni kupoteza 3M kwa wiki kwenye kamari, maisha yako sio lazima kila mtu ndo awe nayo. We sema nachamsha genge hapa mimi natafuta msaada niweze kubadili maisha haya...
 
Hakika. Nitafata ushauri
Kama sijakosea wewe ni mtu ambae shuleni ulikua na akili, ulifaulu vizuri masomo yako hasa hesabu na masomo ya sayansi. Pia uko vizuri kwenye mambo ya biashara.

Watu kama nyie kinachowasumbuaga ni kudhani kwamba hakuna kitu kinachoweza kukushinda! Sasa mkikutana na changamoto suluhisho lenu hua ni kutaka kupambana mpaka wewe ndio ushinde (kama ambavyo ulikua unapambana na swali darasani mpaka uli solve)

Sasa tambua AI ni system imetengenezwa kuhakikisha kwamba inaingiza hela kuliko inavyopoteza. Ukishindana nayo utaishia kuwa masikini. Kubali kwamba hapa duniani kuna vitu huviwezi, na achana navyo.
 
Tangu niliwe kwenye kamari ya kurusha viringi miaka zaidi ya 30 iliyopita, aisee mimi na kamari hapana.
Ya viringi ndo ipi hiyo!? Au ile kipindi cha utoto niliona watu wanasimama barabarani wameweka vitu wanawapa watu viringi wanarusha waachopata wanakula!?
 
Duuuh inabidi upate mtaalamu wa saikolojia...

Kwanza hapo ulipo unaamini hasara uliyopata siku moja utairudisha.. Kitu ambacho si kweli. Kwanza kubali ushapata hasara. Na ujue unavyoendelea utaendelea kula hasara.
 
Ushauri mzuri, kuna wakati nilikuwa mraibu wa jambo fulani niliuza simu ndani ya mwaka mmoja nilitoka kule.
Kuna kipindi nilikuwa so addicted na social media kwenye simu kiasi kwamba kwa siku nikawa natumia mpaka 6 hrs na kuathiri kazi zangu. Niliuza simu na kubaki na Kiswaswadu na hiyo wiki nikaenda shamba for 2 weeks. Ndani ya miezi 2 nikawa normal na kazi zinaenda plus interactions with family and friends.
 
Braza kama ugumu wako wa maisha ni kupata 3M kwa wiki, kuna watu ugumu wetu ni kupoteza 3M kwa wiki kwenye kamari, maisha yako sio lazima kila mtu ndo awe nayo. We sema nachamsha genge hapa mimi natafuta msaada niweze kubadili maisha haya...
Sibishani na mwongo mm
Hata mm ni mcheza kamari mzuri tu lakini sio muongo muongo kama ww onyesha balance Yako nami nikuoneshe betting ilipo nifikisha
 
Back
Top Bottom