Naombeni msaada wa haraka, NMB wamenikalia kooni

Aishi kama mtu ambaye hana kazi kwa kipindi hicho
Hili ndio la msingi, miezi nane si Mingi. Akubali tu kuishi kwa taabu kipindi hiki ili mradi hadaiwi kodi, taabu nyingine azivumilie, awashirikishe familia vizuri ili kusiwepo masononeko ndani baada ya kuona ni chai na msosi mara moja per day.
 
Hivi mbona unaongelea tu waliofanya kazi miezi mitatu??

Sasa ukae ukijua ukifariki na una mkopo bank, mirathi yako ambayo wangepewa familia inakatwa deni na inayobaki wanapewa familia au wategemezi wako. Usifikiri eti unaweza kufanya kazi 10 yrs alafu ufariki familia isipate chochote.

Hilo fao la mazishi ndio litakatwa deni la bank inayobaki watapewa hao wategemezi..

Wewe unafikiri dhana kwamba mwajiri ndio collateral yako ni ipi? Think!!
 
Wote tunapenda fedha, lakini ulifanya makosa kuchukua fedha isiyokuhusu. Kwa kitendo hicho Benki zote huwa wanachukua hatua hizo, kuchukua chochote kinachoingia Kwa account Hadi wakamilishe hela Yao.
 
Wote tunapenda fedha, lakini ulifanya makosa kuchukua fedha isiyokuhusu. Kwa kitendo hicho Benki zote huwa wanachukua hatua hizo, kuchukua chochote kinachoingia Kwa account Hadi wakamilishe hela Yao.
Mama mkubwa unanisaidiaje
 
Wapeleke mahakamani..
Tumia na media pia kuwapelekesha.
Wataomba makubaliano mapya tu
 
Tafuta email ya CEO wao..
Au nenda ukamuone

Wanachofanya hawa wafanyakazi wa chini ni kukukandamiza kufukia makosa yao..
Mradi Una evidence hadi za simu..
Basi nenda kamuone CEO wao..
Waambie utaenda Kwa media
Bank zinaogopa media kuliko mahakama
 
Mirathi yako inakatwa wanapewa benki? Vipi kama umeacha mashati matatu ??

Sio kila mtu anaacha mirathi inayotosha kukatwa kulipa deni la nyumba bro.

Na hilo fao la mazishi ni hela ya jeneza na nauli ya Coaster moja kwenda kijijini kwenu kuzikwa, inalipaje deni la mortgage ya nyumba ????

Halafu unasema nifikirie watu waliofanya kazi miaka 10, hata miaka 10 haitoshi kupata pensheni. Pensheni inaanzia miaka 15, yani miezi 180 ya uchangiaji.

Huwezi ku kwiti kazi au kufukuzwa au kuvuta kabla ya muda wa kustaafu halafu ukasema una pensheni, inatoka wapi pensheni?
 
Ninachokuambia ni ukweli salary slip bado inaonyesha Bodi wanakata Kama kawaida maana hawajapewa Chao..
Lakini pia Deni ambalo lipo kwenye akaunti yangu,
NI TOFAUTI NA DENI WANALONIDAI HAO LOAN BOARD,
sasa sijui
Kama Mwajiri wako ni serikali basi suala la makato kuendelea kwenda Loan Board hatuwezi ku-conclude kwamba Board hawajapewa chao!! Unaweza kukuta NMB wamesha-prepay Loan Board lakini Hazina bado wanapeleka makato huko huko Loan Board badala ya NMB, matokeo yake pesa inaenda kukaa kwenye suspense account!
 
Kwahiyo huko PSSF yanapelekwa mashati au unakatwa pesa kwenye mshahara wako??

Sasa nikwambie tu kwa kifupi; Serikali iliingia kwenye mgogoro mkubwa sana na Mabenki ya biashara kwa waliofukuzwa kazi kwa vyeti feki. Wengine walikuwa na mikopo bank, kilichofanyika akiba ya pension zao zilitumika kulipa yale madeni.

Ukifariki na unadaiwa na bank, Basi hifadhi yako ya pension italipa deni lako na hiyo ndio dhana ya Mwajiri kuwa mdhamana wako..

Pili, Unaongelea wafanyakazi wa serikali ambao wako involuntary kujitoa na kuchukua pension yao muda wanaotaka, vipi unajua waajiriwa wa private sector dakika yeyote anaweza kuacha kazi na kuchukua pension yake??

Kama unajuana na banker yeyote (Loan Officer) sanasana uliza kama hautaambiwa hichi kitu. Yaani ukope million 40 kabla hata ya marejesho mawili hujamaliza alafu utegemee bank itakuachia?? Hakuna hiyo mkuu, na kama hiyo loophole ingekuwepo maafisa mikopo wangeitumia sana kupiga hela
 
Tafuta email ya CEO wao..
Au nenda ukamuone

Wanachofanya hawa wafanyakazi wa chini ni kukukandamiza kufukia makosa yao..
Mradi Una evidence hadi za simu..
Basi nenda kamuone CEO wao..
Waambie utaenda Kwa media
Bank zinaogopa media kuliko mahakama
Email yake personal au ya kazi?
 
Wewe ni mwizi kwa kuwa kitendo ulichofanya ni wizi, lipa deni la benki, usafishe profile yako. Kwa taarifa yako huwezi kopa benki yoyote wata ku blacklist mpaka urudishe hilo deni.
 
Ni watumishi weeengi mno wanaolia na bank hyo ,kusema ukweli nmb wajitadhimini
 
Tamaa mbaya sana na ndio inakugharimu! Ulikosa uaminifu kula kisicho rizki! Pole na pambana na hali yako sasa!
 
Ni watumishi weeengi mno wanaolia na bank hyo ,kusema ukweli nmb wajitadhimini
Yaani uchukue Mali isiyokuhusu, mwenye Mali ashtuke umlaumu?. Ni kweli situation ya kukosa mshahara ni ngumu na inatesa lakini makosa ni yake.
 
Wewe ni mwizi kwa kuwa kitendo ulichofanya ni wizi, lipa deni la benki, usafishe profile yako. Kwa taarifa yako huwezi kopa benki yoyote wata ku blacklist mpaka urudishe hilo deni.
Hajakataa kulipa ila ni namna ya kulipa kuna muda shida zinaweza kukufanya ufanye jambo la ajabu sana tuendelee kumuomba Mungu atupunguzie ugumu wa maisha kesho yetu iwe njema maana hatuijui na huijui
 
Tugeshea kwenye msafara wa mkuu akipita omba mic utoe malalamiko, kama wanavyofanya wajane waliodhurumiwa nyumba zao skuiz naona anatoa maelekezo. Watakata robo ya mshahara boss.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…