Naombeni msaada wa haraka, NMB wamenikalia kooni

Naombeni msaada wa haraka, NMB wamenikalia kooni

Hupendi kuulizwa kwanini ulitumia pesa zote [emoji15]

Basi na sisi hatutaki kusikiliza hadithi yako

Kamalizane na NMB maana wakati ubakopeshwa hukutushirikisha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii habari mleta mada umeiandika sijui huku unakimbizwa na maofisa mikopo wa NMB wanataka kukunyang'anya na simu kabisa ili wapunguze deni.


Hebu ainisha bila kificho mambo yafuatayo bila kutuchanganyia madawa...

1. Deni la bodi ya mikopo (HELSB) ni kiasi gani?!
2. Ulikuwa unadaiwa na NMB kabla ya kupelekea deni la helsb ama ulimaanishaje?!
3. Hiyo amount ya milioni 5,600,000 inahusiana na nini na hii 17,400,000 ni nini?!
4. Kwa mujibu wa NMB na utaratibu wao wa kukopesha na makato, inakuwaje wanakulamba mshahara wote?!
5. Mshahara wako ni kiasi gani ili tuweze kukusaidia kucalculate makato sahihi?!

Hebu tunyooshee habari maana umeandika kwa kuruka ruka sana...
Niwewe tu Mkuu ndio hujasoma vizuri mbona nimeeleweka kabisa
 
Sheria ya utumishi wa umma inasema lazima mshahara ubaki moja ya tatu.(kila mtu ana ya kwake kulingana na basic salary yake)..lakini pia hakuna mtu mwenye mamlaka ya kukamata mshahara wako bila notification.watu pekee wenye uwezo huo ni MWAJIRI, MAHAKAMA(kwa maandishi ), TAKUKURU(kwa maandishi), benki haina mamlaka ya kushikilia mshahara wako wote bila kupata kibali toka kwa MWAJIRI au MAHAKAMA. walipaswa wafanye negotion na ww namna watakavyokata hiyo hela...nenda kwa MWAJIRI wako mweleze ukweli na ikishindikana nenda kwa wanasheria wakupe msaada wa kuwaita NMB mahakamani.
N.B. watanzania wengi ni waoga kuchukua hatua za kudai haki zao ndo mana wengi huishia maumivu...hizo njia mbili NMB hachomoki...haujashindwa kulipa deni lao watafute njia bora ya we kulipa....
Na kumbuka nimewafuata tufanye negotiation wamegoma,
Nashukuru Mkuu kwasasa nipo naongea na mwanasheria hivi Kuna vielelezo kadhaa nimpe tukutane mahakamani sasa,
Maana Kama Mimi nilifanya makosa kutoa pesa yote na wao wanafanya Yale Yale kushikilia mshahara wote
 
Nisaidieni wakubwa maana nimewaomba walau wakate kidogo kidogo pia wanagoma na sasa wanashikilia mshahara wote mpaka deni liishe ni zaidi ya miezi 8 na wote tunajua maisha ya mfanyakazi bila salary. Nisaidieni nifanyeje.
Wewe si umekula pesa isio yako?unalia Nini?
Jikaze tu litaisha,tatizo mnakimbilia sana kujenga bila kupanga,haya kale hicho kibanda Basi,so umetumia pesa yote kujenga
 
Mshahara ni wako kwanini upate shida nenda CRDB fungua account andika barua kwenda kwa afisa utumishi wako kuwa unaomba kubadilisha account ya mshahara ipige chini hiyo account ya NMB weka ya CRDB ili muonyeshane makali kidogo wakiona pesa haiji watakutafuta mtakaa chini mtaseti ulipaje kwisha habari.
 
Credit bureau ipo Tanzania.
Na inafanya kazi.
Bank zote hawatoi mkopo mpaka wakucheck huko crb ndo process zinaanza.
Sounds good manake dah, zamani ilikuwa uhuni mtupu, na kuna issue moja sijui kama wameshaifanyia kazi! Hii issue ilinifanya niache kazi mahali nikiwa nimefanya chini ya miezi 2... ilikuwa ni Business Consultacy Firm, and I loved the job!

Baada ya jamaa kuanza kuniamini, siku ya siku nikaletewa project ya mteja aliyekuwa anataka mkopo wa 200M. Baada ya mteja kumtaka aniletee docs, akaleta zote including BOQ pamoja na NMB Statement ambayo baada ya kuifanyia valuation, jamaa alistahili kupata mkopo wa around 60M na sio hiyo 200M aliyotaka!

Nikapiga chini!

Heee! Saa chache baadae Bosi wa Kitengo si anakuja na forged bank statement yenye turnover ya kutosha inayompa the same jamaa sifa ya kukopa hata 300M!! Baada ya kuchunguza, nikagundua ndiyo michezo yao, na mbaya zaidi, lending banks zilikuwa wala hazifanyi due dilligence ya kutosha ku-verify bank statements zinazopelekwa kwao kutoka benki nyingine ni credible!!

Yaani walichokuwa wanafanya, wakiona Bank Stamp na "signature", tayari!!

Nikaona hapanifai... nikapiga chini mzigo, nikarudi zangu kijiweni!!
 
Back
Top Bottom