Naombeni msaada wa mawazo mwanangu hapendi Kula

Organic Live Food

Senior Member
Joined
Aug 2, 2013
Posts
127
Reaction score
236
Habari za leo wana Jf. Naombeni msaada wa mawazo ya kumfanya mtoto wangu apende kula.
Mtoto wangu ni wakike anaumri wa miaka 5 sasa. Afya yake sio mbaya ila tatizo lake HAPENDI KULA.
Kila siku lazima nimshikie fimbo wakati wa kula. Nikulazimishana ni vilio mwanzo mwisho mpaka chakula kinaisha.

Na usipomshikia kiboko hicho chakula hakitaisha yuko radhi akae hapo akiangalie tu muda wote.

Na anatabia yakuweka chakula mdomoni halafu hamezi. Kuna wakati najiuliza sijui anashida kwenye koo?

Kwa sasa namuonea huruma mana namchapa sana wakati wakula ila habadiliki ingawa akisikia njaa huwa anasema.

Naomba ushauri nitumie mbinu gani ili nimshawish apende kula ama kama kuna dawa zinazoweza kumpelekea kupata hamu ya kula mara kwa mara ningeomba nizifaham.

Je tatizo hili ni kwa watoto wengine pia ama ni kwa mtoto wangu tu?

Natanguliza shukrani..🙏
 
Sio daktari lakini natumia uzoefu nilioupata baada ya kulea wanangu.
Inawezekana unampa chakula aina moja kinamchosha pia pengine aina ya mapishi inamshinda!!! Badala ya kumchapa kuwa nae karibu muulize Nini anapenda pika vyakula tofauti tofauti mpe uhuru mtoto ujue atakachoweza kula punguza ukali umuelewe mwanao.
Karibu pia hospitali akachekiwe labda ana tatizo
 
Asante nashukuru. Ntazingatia. Vyakula nitofauti tofauti vinapikwa. Labda kwenye mapishi inabidi ujuzi uongezeke. Asante kwa ushauri mzuri
 
Habari za leo wana Jf. Naombeni msaada wa mawazo ya kumfanya mtoto wangu apende kula.
Mtoto wangu ni wakike anaumri wa miaka 5 sasa. Afya yake sio mbaya ila tatizo lake HAPENDI KULA.
Kila siku lazima nimshikie fimbo wakati wa kula. Nikulazimishana ni vilio mwanzo mwisho mpaka chakula kinaisha.

Na usipomshikia kiboko hicho chakula hakitaisha yuko radhi akae hapo akiangalie tu muda wote.

Na anatabia yakuweka chakula mdomoni halafu hamezi. Kuna wakati najiuliza sijui anashida kwenye koo?

Kwa sasa namuonea huruma mana namchapa sana wakati wakula ila habadiliki ingawa akisikia njaa huwa anasema.

Naomba ushauri nitumie mbinu gani ili nimshawish apende kula ama kama kuna dawa zinazoweza kumpelekea kupata hamu ya kula mara kwa mara ningeomba nizifaham.

Je tatizo hili ni kwa watoto wengine pia ama ni kwa mtoto wangu tu?

Natanguliza shukrani..🙏
Hiyo fimbo unayomshikia ndio inampotezea appetite kabisa
 
Umenena Kaka,,Huwezi Kumchampa Mtoto Kisa Kakataa Kula,,Hapo Ndio Anamvuruga Kabisa,Mtoto anahitaji Akili Kubwa Mnoo ili uwezekung'amua Shida Zake
Asante sn ntazingatia. Pia naihitaji hiyo akili ya ziada ambayo nimepungukiwa kwa kupata mawazo ya wadau km nyie. Isitoshe ni ulezi wangu wakwanza
 
Daaah hapa kwenye chips anapenda sn atakula vzr bila shida. Tatizo huwezi pika chips kila siku.
Huyo ana appetite ndogo Kama Mimi tu siwezi kula ugali na mchicha tupu zaidi ya tonge tano.
Chakufanya hapo:
1. Tumia vidonge vya kuongeza hamu ya kula Vitamin B wanaita. AU
2. Mpikie chips yeye peke yake kila siku wengine endeleeni na ugali. AU
3. Kila mlo mpe juice au machungwa yanaongeza sana hamu ya kula. AU
MWISHO LAKINI SIO KWA UMUHIMU
4. Mpeleke kijijini hata miezi miwili akaone wenzake wanavyogonga uji wa chumvi na ugali mchunga. Atabadilika tu.
 
Shida ya wa Tanzania walio wengi vyakula ni vya aina ile ile ugali au wali na ukichanganya na mapishi yenyewe mtoto lazima akinai kula. Jaribu kumbadilishia chakula vyenye radha tamu nadhani unavijua.
Mkuu majimaji vyakula vyenye Radha tamu ni vipi hivyo?

Mtoto azingue kula afu Huku muhindi nae anakula hela za mikeka 😂
 
Back
Top Bottom