Naombeni msaada wa mawazo mwanangu hapendi Kula

Habari za leo wana Jf. Naombeni msaada wa mawazo ya kumfanya mtoto wangu apende kula.
Mtoto wangu ni wakike anaumri wa miaka 5 sasa. Afya yake sio mbaya ila tatizo lake HAPENDI KULA.
Kila siku lazima nimshikie fimbo wakati wa kula. Nikulazimishana ni vilio mwanzo mwisho mpaka chakula kinaisha.

Na usipomshikia kiboko hicho chakula hakitaisha yuko radhi akae hapo akiangalie tu muda wote.

Na anatabia yakuweka chakula mdomoni halafu hamezi. Kuna wakati najiuliza sijui anashida kwenye koo?

Kwa sasa namuonea huruma mana namchapa sana wakati wakula ila habadiliki ingawa akisikia njaa huwa anasema.

Naomba ushauri nitumie mbinu gani ili nimshawish apende kula ama kama kuna dawa zinazoweza kumpelekea kupata hamu ya kula mara kwa mara ningeomba nizifaham.

Je tatizo hili ni kwa watoto wengine pia ama ni kwa mtoto wangu tu?

Natanguliza shukrani..
 
Unamlisha mtoto MAUGALI kila siku unategemea nini?? WE KUWEZA?

Mimi mwenyewe MAUGALI kila siku siwezi, yanakwangua sana koromeo!!

Pika vitu vya kijanja, tumandazi mandazi, visheti, chips, mayai, ufuta, kuku rosti, futari, masotojo nakadhalika!

MAUGALI yaliyokomaa na kudoda utamfanya mtoto azimie.

Hata Mimi ningegoma kula. Halafu UGALI MAHARAGE mweeeehhh!!!!! FAMCHEZO!!!

Cc: Lamomy Labella Extrovert Poor Brain Monetary doctor Mbaga Jr Kijana masikini Dogoli kinyamkela Kalpana Dr. Mariposa Lloyd Munroe secretarybird Mzee wa kupambania
 
Huyo ana appetite ndogo Kama Mimi tu siwezi kula ugali na mchicha tupu zaidi ya tonge tano.
Chakufanya hapo:
1. Tumia vidonge vya kuongeza hamu ya kula Vitamin B wanaita. AU
2. Mpikie chips yeye peke yake kila siku wengine endeleeni na ugali. AU
3. Kila mlo mpe juice au machungwa yanaongeza sana hamu ya kula. AU
MWISHO LAKINI SIO KWA UMUHIMU
4. Mpeleke kijijini hata miezi miwili akaone wenzake wanavyogonga uji wa chumvi na ugali mchunga. Atabadilika tu.
Asante sn. Hili lakumpikia chips kila siku hapana kwakweli ila hili la 4 lakumpeleka kijijini ntaliekea kipaumbele litakuwa la umuhimu sn.
Kusema ukweli vyakula vinapikwa vya tofauti mara nyingi tu tunajitahid kwa hilo
 
1. mpeleke hospitali akachekiwe kama ana tatizo la koo, au minyoo, au vidonda mdomoni.
2. Kama hana ugonjwa wowote. acha kumdekeza. mnalea watoto kimayai mayai, toka asubuhi, mara andazi, mara pipi, mara biskuit, mara asikilimu mara chama, sijui karanga, tena unarudi umemletea piza halafu unategemea mtoto atakula vizuri. kuwe na vipindi vya kula na vipindi vya kusaka njaa sio toto linadokoa dokoa vyakula siku nzima then utegemee ulaji mzuri.
 
Unamlisha mtoto MAUGALI kila siku unategemea nini?? WE KUWEZA?

Mimi mwenyewe maugali kila siku siwezi, yanakwangua sana koromeo!!

Pika vitu vya kijanja, tumandazi mandazi, visheti, chips, mayai, ufuta, masotojo nakadhalika!

MAUGALI yaliyokomaa na kudoda utamfanya mtoto azimie.

Hata Mimi ningegoma kula. Halafu UGALI MAHARAGE mweeeehhh!!!!! FAMCHEZO!!!

Cc: Lamomy Labella Extrovert Poor Brain Monetary doctor Mbaga Jr Kijana masikini Dogoli kinyamkela Kalpana Dr. Mariposa Lloyd Munroe secretarybird Mzee wa kupambania
Najitahidi sn kwangu vyakula vinapikwa vya aina tofauti tofaut. Huo ugali unaosemea umaweza kupikwa mara 2 au 3 kwa wiki
 
Kama hana hamu ya kula kwann unamlazimisha kula?

Tutumie mfano wa ndege kama Tai, Tai akiwa ameshiba hata umuekee mbele yake chakula chochote kile hali, atakula tena endapo tu atakapo sikia njaa na atakula chakula kinachomtosha, hii hali inamfanya asinenepe kupita kiasi na kuwa na mwili mzuri ambao utamsaidia kuwinda chakula.

This applies also to many wild animals.

Sasa sisi binadamu huwa tunafakamia tu, na pia tunalazimisha watoto wetu nao wafakamie.

kwan nani alikwambia lazima ule milo mitatu kwa siku??

Kwani nani alikwambia usipokula milo mitatu kwa siku utakufa?

Tatizo watanzania wengi tunadhani kula milo mitatu kwa siku ni utajiri na kutokula milo mitatu ni sign ya umaskini, ideology ya kipumbavu sana.

Kama mtoto umemlisha asubuhi akashiba sio lazima umlazimishe kula mchana, chakula bado kipo kweny damu ndio maana hasikii njaa, mwache mtoto akisikia njaa atakutafuta tu mwenyew atakwambia njaa inauma.

Tusilamizishe watoto Kula!
 
Kama umeshakapa dawa za minyoo na hakana tatizo kwenye koo,kanadeka hako 5 yrs unamlazimisha Kula! jikaushe kama humuoni siku mbili uone kama hajala ugali tembele Kwa morali, njaa haina rafiki! Kuwa bandidu acha kumbembeleza mkaushie tu!
 
Habari za leo wana Jf. Naombeni msaada wa mawazo ya kumfanya mtoto wangu apende kula.
Mtoto wangu ni wakike anaumri wa miaka 5 sasa. Afya yake sio mbaya ila tatizo lake HAPENDI KULA.
Kila siku lazima nimshikie fimbo wakati wa kula. Nikulazimishana ni vilio mwanzo mwisho mpaka chakula kinaisha.

Na usipomshikia kiboko hicho chakula hakitaisha yuko radhi akae hapo akiangalie tu muda wote.

Na anatabia yakuweka chakula mdomoni halafu hamezi. Kuna wakati najiuliza sijui anashida kwenye koo?

Kwa sasa namuonea huruma mana namchapa sana wakati wakula ila habadiliki ingawa akisikia njaa huwa anasema.

Naomba ushauri nitumie mbinu gani ili nimshawish apende kula ama kama kuna dawa zinazoweza kumpelekea kupata hamu ya kula mara kwa mara ningeomba nizifaham.

Je tatizo hili ni kwa watoto wengine pia ama ni kwa mtoto wangu tu?

Natanguliza shukrani

Nakupa ushauri kama mzazi ambae nimepitia tatizo hilo. Kwanza kabisa shukuru mola kuwa mtoto ni mzima na hana tatizo la kiafya. Mwanangu alikuwa kama hivyo hadi tukafika kwenda kuona madaktari na ushauri wao wote ulikuwa ni kuwa usiwe na wasi wasi iko siku atakuja badilika. Na kweli hivi sasa anakaribia miaka tisa na ndio anaanza kula kama hakuna kesho!

Ushauri wangu wa kwanza kabisa ni kuwa wacha mara moja kumpiga kwa kukataa kula, kumpiga hakutamfanya ale bali atazidi kuchukia kula na kuchukia time za kula. Pili usimpe chakula kingi katika sahani yake na hakikisha anakaa chini kula na haondoki hadi ale angalau nusu ya chakula ulompa. Jaribu sana kuwa mnakula wakati mmoja kifamilia. Hakikisha mnapokula hakuna distraction ya tv, mobile au games zozote zile ili awe concentrate na kula tu. Jaribu kujua ni aina gani ya chakula anapenda kula na uwe uanampa hicho mara nyingi. La muhimu sana ni kuwa kumbuka akiwa na njaa mtoto atakula tu kwa hiyo usimlazimishe, sio lazima mtoto ale breakfast, lunch na dinner.
 
1. mpeleke hospitali akachekiwe kama ana tatizo la koo, au minyoo, au vidonda mdomoni.
2. Kama hana ugonjwa wowote. acha kumdekeza. mnalea watoto kimayai mayai, toka asubuhi, mara andazi, mara pipi, mara biskuit, mara asikilimu mara chama, sijui karanga, tena unarudi umemletea piza halafu unategemea mtoto atakula vizuri. kuwe na vipindi vya kula na vipindi vya kusaka njaa sio toto linadokoa dokoa vyakula siku nzima then utegemee ulaji mzuri.
Asante sn. Nalichukua hili
 
Kama umeshakapa dawa za minyoo na hakana tatizo kwenye koo,kanadeka hako 5 yrs unamlazimisha Kula! jikaushe kama humuoni siku mbili uone kama hajala ugali tembele Kwa morali, njaa haina rafiki! Kuwa bandidu acha kumbembeleza mkaushie tu!
Itabidi nimpeleke hosp akachunguzwe koo then km hana shida huu ushauri utatumika tu
 
Nakupa ushauri kama mzazi ambae nimepitia tatizo hilo. Kwanza kabisa shukuru mola kuwa mtoto ni mzima na hana tatizo la kiafya. Mwanangu alikuwa kama hivyo hadi tukafika kwenda kuona madaktari na ushauri wao wote ulikuwa ni kuwa usiwe na wasi wasi iko siku atakuja badilika. Na kweli hivi sasa anakaribia miaka tisa na ndio anaanza kula kama hakuna kesho!

Ushauri wangu wa kwanza kabisa ni kuwa wacha mara moja kumpiga kwa kukataa kula, kumpiga hakutamfanya ale bali atazidi kuchukia kula na kuchukia time za kula. Pili usimpe chakula kingi katika sahani yake na hakikisha anakaa chini kula na haondoki hadi ale angalau nusu ya chakula ulompa. Jaribu sana kuwa mnakula wakati mmoja kifamilia. Hakikisha mnapokula hakuna distraction ya tv, mobile au games zozote zile ili awe concentrate na kula tu. Jaribu kujua ni aina gani ya chakula anapenda kula na uwe uanampa hicho mara nyingi. La muhimu sana ni kuwa kumbuka akiwa na njaa mtoto atakula tu kwa hiyo usimlazimishe, sio lazima mtoto ale breakfast, lunch na dinner.
Asante sn nmekuelewa sn
 
Chips kila siku hapana😁
Mimi nina familia nyumbani wanangu toka wakiwa aged three wanapewa vyakula tunavyokula wakubwa so a’cally wanavizoea ukifika umri wa kuchagua sana wakiona wamedeka na hawadekezwi wanaendelea kula maisha yanaenda.

Huyo hajashikwa na njaa tu,labda kama mgonjwa but kama mzima akiwa na njaa chochote atakula.
 
Back
Top Bottom