Pyaar
JF-Expert Member
- Feb 11, 2018
- 16,078
- 77,186
Pole sana.
Mpeleke hosp. wamchunguze kama ana shida kooni, apatiwe na dawa za minyoo.
Pia, zingatia kwenye upishi wa chakula chake (Apikiwe chakula chake), kwa kuanzia mpikie vyakula rojorojo, asile chakula kikavu (Kama ni wali, ufanye rojo) Unaweza kumuongezea tui la nazi, maziwa ama karanga.
Jitahidi pia kumkorogea uji awe anakunywa asubuhi na jioni (katika kuandaa unga wa uji zingatia nafaka za makundi mawili/matatu). Katika ukorogaji wa uji unaweza pia kuongeza tui la nazi maziwa ama karanga.
Ukishaona anaanza kula vizuri sasa ndo utaanza kuvifanya vyakula vyake kuwa milo ya kati kabla ya milo mikuu mnayokula wote kama familia.