Naombeni msaada wa mawazo mwanangu hapendi Kula

Naombeni msaada wa mawazo mwanangu hapendi Kula

Hakikisha unapika chakula anachokipenda. Mimi kwangu watoto ndo wanapanga menu. Muulize unataka kula nini.. Then pika chakula anachokitaka.

Asipokula au akila kidogo usimlazimishe muache hadi njaa imkung'ute kisawa sawa ataomba mwenyewe chakula.

Unajua hii mambo ya kula asububi mchana na jioni ni mazoea tu. Ila mtu anatakiwa ale pale anaposikia njaa.

Swala lingine, Je mtoto yuko active? Anacheza michezo ya kutumia nguvu.

Hakikisha mtoto anacheza michezo ya kutumia nguvu, lazima atasikia njaa tu. Lakini kama anakaa ndani siku nzima ni changamoto.

Summary

Usimlazimishe, akisikia njaa ataomba chakula mwenyewe
Nimekusoma mtaalam. Kwenye swala lakucheza yupo active nimtundu sn hadi kero
 
Akipata chakula apendacho atakula bila shuruti.. Unajua huwa tunawapangia vyakula kwa ladha na mitazamo yetu
Nikweli ila chakula kikuu ni chips ukimtajia anapenda ale ninj anakutajia chips. Sasa chips kila siku😁
 
Pole aisee, nakuelewa sana jinsi unaumia kwa unachopitia. Yani hakuna mtoto anaumiza kichwa kama hasiyependa kula, ukute kajaza chakula tu mdomoni.
Nilipata hiyo shida kwa mwanangu, ikanilazimu niwe napika chakula kingi ili nichukue na rafiki zake wale pamoja. Vile alivyokuwa akiona wenzake wanakula nae anakula, ikamjenga baada ya muda mfupi akawa OK.
Mwanao haumwi, ni changamoto za kawaida, tafuta mbinu taratibu mpaka utaipata,
 
Kutokula kunaweza kusababishwa na mambo kama vile
1: uchache wa watoto. Mtoto ambae hali mpeleke changanyikeni akakutane na rika wenzake wakagombee chakula.
2: Nature. Kuna watu kwa asili yao sio walaji sana wanakulatu kidogo wanaachwa
3: Vyakula vya aina Moja mfululizo
4: Hali ya hewa ambayo sio rafiki kwa mtoto
5: Mtoto kutopewa maji mengi
6: Mtoto kunyonyeshwa marakwamara hivyo kua muda mwingi ameshiba
 
Mi wa kwangu Ana miaka 3 najua Nini anakula Nini hataki anamwacha..mfano samaki na nyama anaita panya. Hali kabisa...ngano mchele chai magarage ndio Mambo yake...more kila siku...kuku Bata anakula.ila nyama mbuzi ngombe kitimoto hagusi sijui anaionaje hata ubadilishe mapizshi vip..
 
Pole aisee, nakuelewa sana jinsi unaumia kwa unachopitia. Yani hakuna mtoto anaumiza kichwa kama hasiyependa kula, ukute kajaza chakula tu mdomoni.
Nilipata hiyo shida kwa mwanangu, ikanilazimu niwe napika chakula kingi ili nichukue na rafiki zake wale pamoja. Vile alivyokuwa akiona wenzake wanakula nae anakula, ikamjenga baada ya muda mfupi akawa OK.
Mwanao haumwi, ni changamoto za kawaida, tafuta mbinu taratibu mpaka utaipata,
Asante sana mdau
 
Organic Live Food tukijaji kitabu kwa kuangalia kava lake... kama hii ID inasadifu yaliyomo basi shida unaweza ikawa inaanzia hapa.
😁😁Hapana kaka hii ni hobby yangu tu najihusisha na kilimo kisichotumia kemikali ila kwenye upande wakula nawaachia familia wale wanachokitaka. Mim wakati meingi nakula vitu vyakuchemsha ila siwakataz wapike vyakula vyao vya mafuta. Inshot wako na uhuru wakula chochote
 
Kutokula kunaweza kusababishwa na mambo kama vile
1: uchache wa watoto. Mtoto ambae hali mpeleke changanyikeni akakutane na rika wenzake wakagombee chakula.
2: Nature. Kuna watu kwa asili yao sio walaji sana wanakulatu kidogo wanaachwa
3: Vyakula vya aina Moja mfululizo
4: Hali ya hewa ambayo sio rafiki kwa mtoto
5: Mtoto kutopewa maji mengi
6: Mtoto kunyonyeshwa marakwamara hivyo kua muda mwingi ameshiba
Sawa sawa mdau hyo namba 3 najitahidi sn kuwe na vyakula tofauti home
 
Jaribu njia hii itakusaidia, tafuta watoto wenzie wenye rika kama lake wawe watano au wanne then waekee chakula kwenye sahani moja kisha waache we kakae sehemu umwangalie mwanao atakavyokula
 
Jaribu njia hii itakusaidia, tafuta watoto wenzie wenye rika kama lake wawe watano au wanne then waekee chakula kwenye sahani moja kisha waache we kakae sehemu umwangalie mwanao atakavyokula
Hii ntaitengea siku maalum. Kila wiki itakuwa na siku yakula na watoto wa jirani
 
Hiyo tabia alikuwa nayo mdogo wangu yani uji unamlisha anaweka mdomoni dakika kumi na anaweza kumeza ukimfurahisha au ukimtishia sana,Dada wa kazi alikuwa anambana pua ili ameze ila maza alivyomstukia alimgombeza kinoma,unakuta uji wa kunywa Dakika 10,yanatumika masaa hadi matano kumaliza,ila sahizi ni mbaba na anapeleka msosi kinoma,la msingi mvumilie tu please,na usimchape unamuumiza hisia kwa kiasi kikubwa.
 
Back
Top Bottom