Dadakidoti
JF-Expert Member
- Jul 26, 2024
- 399
- 1,409
- Thread starter
- #21
likizo yangu kazini ni mwezi wa tatu mwishoni na ndio nimepanga kwenda lakini naona hali inazidi kuwa mbaya.Kama Hutojali Nitafute Nikupe Kumbato La Faraja Ya Huba Kipenzi
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
likizo yangu kazini ni mwezi wa tatu mwishoni na ndio nimepanga kwenda lakini naona hali inazidi kuwa mbaya.Kama Hutojali Nitafute Nikupe Kumbato La Faraja Ya Huba Kipenzi
MkuuMkuu kwa Padre tena, mbona wakatoliki wanatoka kwa hao Mapadre na wanakuja kwa mwamposa.
Hata waislam wanaenda kwa mwamposa lakini haina maana ya kuwa hakuna shehe anayeweza kukuombea ukapona. Wapo mapadri wanatoa hadi mapepoMkuu kwa Padre tena, mbona wakatoliki wanatoka kwa hao Mapadre na wanakuja kwa mwamposa.
Unaota vile unavyivipatia nafasi kuuuuubwa kuviwaza mchana.Bila shaka wote mko poa kabisa.
Kidoti wenu nimerudi maji ya shingo nashindwa hata pa kuanzia. Kama familia yangu ya JF naombeni ushauri wenu wenda nikapata hata msaada.
Kama mnakumbuka nilileta uzi huu Kuna wengine hatujui tulipokosea
Sikuweza kuandika kila kitu. wengi mlisoma historia yangu na mnajua wapi nimepitia mpaka nilipo.
niwawachoshe moja kwa moja kwenye mada.
Katika maisha yangu watu ambao ndo walikuwa familia yangu ni babu na bibi zangu sababu wao ndio walikuwa wanasimama kama wazazi ninapopitia changamoto. Hasa hasa babu mzaa baba na bibi mzaa mama. kwa ufupi mwaka jana mwezi wa tatu mwishoni babu yangu alikufa. Kipindi msiba unatokea nilikuwa na wakati mgumu sana sababu sikuwa na kazi ya kueleweka na nilikuwa na mtoto mdogo. Hivyo sikuweza kwenda kanda ya ziwa msibani. wakati huo huo bibi yangu mzaa mama alikuwa Arusha kwa ajili ya matibabu alikuwa anaumwa baada ya kupata taarifa alinipigia simu kunipa pole na kunitia moyo sababu alijua jinsi nilivyokuwa nampenda babu yangu. akanisisitiza nimwangalie mtoto alijua nilivyokuwa nimeumia kutoweza kwenda kumzika babu yangu. alikuwa anasisitiza nisiangalie kitu kingine zaidi ya kumwangalia mtoto. nilitaka kuuza kibanda changu ili nipate nauli lakini bibi alikataa akaniahidi kuwa akirudi nyumbani atanitumia nauli nitaenda kuzuru kaburi.nikaona ni sawa nikamkubalia.
Ilikuwa ni ijumaa bibi alinipigia simu tliongea sana karibia masaa mawili. akinisisitiza akili yangu yote iwe kwa mtoto. Kesho yake ajabu napigiwa simu kuwa bibi yangu nae hayupo tena duniani ndani ya wiki mbili tu nilipoteza watu muhimu sana kwangu. walisafirisha mwili pia sikuweza hata kwenda kuzika. hakuna kipindi kigumu niliwahi kupitia kama kipindi hicho. sina kazi ya kueleweka nilikuwa nafanya kazi kwa mama ntilie nalipwa elfu tano angalau nipate kula na mtoto. Mama angu alikuja kumzika bibi lakini hakunipigia hata simu kujua angalau mimi na mtoto tunaendeleaje. kwa ufupi bibi ndo alikuwa kama mama yangu.
Mungu ni mwema nilifanikiwa kupata kazi ambayo naendelea nayo mpaka sasa namshukuru Mungu nipo vizuri japo si sana nina dhiki za kawaida kama za watu wengine. hatulali njaa na mtoto naweza kulipa ada kodi na kujikimu mahitaji yangu na mtoto. naweza kula nachokitamani. namshukuru sana Mungu kwa hilo.
ila kinachoniumiza toka itokee hiyo misiba sina amani nikiwakumbuka babu na bibi yangu naanza kulia. usiku silali nimekonda nimepungu kutoka 63kg mpaka 55kg.
usiku nikilala naweza kuota nipo kanda ya ziwa yaani naota makaburi naweza ota nimeenda kwa bibi lakini nyumba imejengwa makaburini. naweza kuota nipo mochwari yaani kwa ujumla sioti ndoto za kawaida. najikuta wakati mwingine natamani kufa labda naweza kupumzika lakini akili inaniambia ukifa huwezi kupumzika kwa amani kwa sababu mtoto wako hutakuwa umemuacha katika mazingira magumu sana. nimedhoofika sana kichwa kinaniuma kila siku nameza pain killer lakini kuna muda zinadunda.
samahani naombeni msaada wenu nipo njia panda.
Iko nalo neno
Mungu Akitujalia Afya ya Mifupa, Damu Na Nyama Kama Hutojali Twende Wote Huo Mwezi 3 Kwenu.likizo yangu kazini ni mwezi wa tatu mwishoni na ndio nimepanga kwenda lakini naona hali inazidi kuwa mbaya.
Mungu Akitujalia Afya ya Mifupa, Damu Na Nyama Kama Hutojali Twende Wote Huo Mwezi 3 Kwenu.
nilisema kila kitu kwenye uzi huu Kuna wengine hatujui tulipokoseaKuna kitu bado hujakisema ambacho ndicho kiini cha changamoto unazopitia. Pata mtu sahihi wa kumueleza kila kitu kuhusu wewe na njia ulizopita mpaka kufikia hapo. Utasaidika vizuri sana na huo mzigo mabegani mwako utautua, utajiskia amani sana. Imani hufanya kazi na Ukweli na uwazi.
Omba bila kukoma,pitia uzoefu wa Ayubu!Hata Mimi ninayekushauri nimepitia hayo uliyoyaeleza na kuzidi,maana niliwazika baby na Bibi na mke na watoto,hadi nikawa kama nimechanganyikiwa,Wadau hawakuwa nyumba kuniambia Nina Ukimwi.Hivi Sasa Nina watoto warembo na Wana akili darasani,na maisha yangu ni mazuri kama Niko peponi Hata vikwazo vya Trump naona ni upepo tuu wa asubuhi.Mungu ni Mwema hutupitisha kwenye tanuri la moto na hutupa milango ya kumtokea,milango sio mlango.yaani hata nguvu za kuomba niwe mweli sina. kabla ya vifo hivi kutokea hakuna siku niliacha kuwataja babu na bibi yangu kwenye maombi walivyokufa tu. Ndio nikaona Mungu ameniadhibu vibaya. sitamani tena kuomba
amenDaah pole sana dada💔, nitakuweka kwenye maombi 🙏
nitajaribu tena japo nguvu sina tenaOmba bila kukoma,pitia uzoefu wa Ayubu!Hata Mimi ninayekushauri nimepitia hayo uliyoyaeleza na kuzidi,maana niliwazika baby na Bibi na mke na watoto,hadi nikawa kama nimechanganyikiwa,Wadau hawakuwa nyumba kuniambia Nina Ukimwi.Hivi Sasa Nina watoto warembo na Wana akili darasani,na maisha yangu ni mazuri kama Niko peponi Hata vikwazo vya Trump naona ni upepo tuu wa asubuhi.Mungu ni Mwema hutupitisha kwenye tanuri la moto na hutupa milango ya kumtokea,milango sio mlango.
Nakuhakikishia hutakuja kujuta, Mungu anatuwazia mema,ndio maana hao Babu na Bibi walikuwa wema kwako,Ibilisi ni mchonganishi na ndie anayekukatisha tamaa,jipe matumaini,simama kama Wewe bila kujali hao manabii wa mchongo!nitajaribu tena japo nguvu sina tena
thamani yangu hipi labda? hiko wapi mdogo wangu tumbo moja baba mmoja na mama mmoja yupo hapa Dar lkn nina miaka saba sasa tangu nimuone, nikimpigia huwa hapokei msg hajibu. nimejifungua mwanangu ana miaka 2.5 sasa lkn hajawahi hata kuja kumuona. kama ndugu yako mwenyewe hakuoni wa thamani nani ataiona thamani yako. mama alikuja Tz kumzka mama yake alipitia Dar lkn hakunipigia hata simu. angalau kumwona mjukuu wake. nisipo mgia mimi hata siku moja hawezi hata kukosea namba akanipigia nina miaka 8 sasa tangu niione sura ya mama yangu. babu na bibi waliokuwa wananipa thamani Mungu akawachukua kudhihirisha kuwa mimi si chochote. kinachoniuma ni hiki kiumbe kisicho na hatia. thamani hipi unaongelea labda.Pole nakushauri pata rafiki,rafiki ambae ataweza kuwasiliana na wewe muda wowote,atakutoa kwa mawazo na ukajiona uko wa thamani
You need some body…
thamani yangu hipi labda? hiko wapi mdogo wangu tumbo moja baba mmoja na mama mmoja yupo haha Dar lkn nina miaka saba sasa tangu nimuone, nikimpigia huwa hapokei msg hajibu. nimejifungua mwanangu ana miaka 2.5 sasa lkn hajawahi hata kuja kumuona. kama ndugu yako mwenyewe hakuoni wa thamani nani ataiona thamani yako. mama alikuja Tz kumzka mama yake alipitia Dar lkn hakunipigia hata simu. angalau kumwona mjukuu wake. nisipo mgia mimi hata siku moja hawezi hata kukosea namba akanipigia nina miaka 8 sasa tangu niione sura ya mama yangu. babu na bibi waliokuwa wananipa thamani Mungu akawachukua kudhihirisha kuwa mimi si chochote. kinachoniuma ni hiki kiumbe kisicho na hatia. thamani hipi unaongelea labda.