Naombeni msaada wenu

Naombeni msaada wenu

Bila shaka wote mko poa kabisa.
Kidoti wenu nimerudi maji ya shingo nashindwa hata pa kuanzia. Kama familia yangu ya JF naombeni ushauri wenu wenda nikapata hata msaada.

Kama mnakumbuka nilileta uzi huu Kuna wengine hatujui tulipokosea
Sikuweza kuandika kila kitu. wengi mlisoma historia yangu na mnajua wapi nimepitia mpaka nilipo.
niwawachoshe moja kwa moja kwenye mada.

Katika maisha yangu watu ambao ndo walikuwa familia yangu ni babu na bibi zangu sababu wao ndio walikuwa wanasimama kama wazazi ninapopitia changamoto. Hasa hasa babu mzaa baba na bibi mzaa mama. kwa ufupi mwaka jana mwezi wa tatu mwishoni babu yangu alikufa. Kipindi msiba unatokea nilikuwa na wakati mgumu sana sababu sikuwa na kazi ya kueleweka na nilikuwa na mtoto mdogo. Hivyo sikuweza kwenda kanda ya ziwa msibani. wakati huo huo bibi yangu mzaa mama alikuwa Arusha kwa ajili ya matibabu alikuwa anaumwa baada ya kupata taarifa alinipigia simu kunipa pole na kunitia moyo sababu alijua jinsi nilivyokuwa nampenda babu yangu. akanisisitiza nimwangalie mtoto alijua nilivyokuwa nimeumia kutoweza kwenda kumzika babu yangu. alikuwa anasisitiza nisiangalie kitu kingine zaidi ya kumwangalia mtoto. nilitaka kuuza kibanda changu ili nipate nauli lakini bibi alikataa akaniahidi kuwa akirudi nyumbani atanitumia nauli nitaenda kuzuru kaburi.nikaona ni sawa nikamkubalia.

Ilikuwa ni ijumaa bibi alinipigia simu tliongea sana karibia masaa mawili. akinisisitiza akili yangu yote iwe kwa mtoto. Kesho yake ajabu napigiwa simu kuwa bibi yangu nae hayupo tena duniani ndani ya wiki mbili tu nilipoteza watu muhimu sana kwangu. walisafirisha mwili pia sikuweza hata kwenda kuzika. hakuna kipindi kigumu niliwahi kupitia kama kipindi hicho. sina kazi ya kueleweka nilikuwa nafanya kazi kwa mama ntilie nalipwa elfu tano angalau nipate kula na mtoto. Mama angu alikuja kumzika bibi lakini hakunipigia hata simu kujua angalau mimi na mtoto tunaendeleaje. kwa ufupi bibi ndo alikuwa kama mama yangu.

Mungu ni mwema nilifanikiwa kupata kazi ambayo naendelea nayo mpaka sasa namshukuru Mungu nipo vizuri japo si sana nina dhiki za kawaida kama za watu wengine. hatulali njaa na mtoto naweza kulipa ada kodi na kujikimu mahitaji yangu na mtoto. naweza kula nachokitamani. namshukuru sana Mungu kwa hilo.
ila kinachoniumiza toka itokee hiyo misiba sina amani nikiwakumbuka babu na bibi yangu naanza kulia. usiku silali nimekonda nimepungu kutoka 63kg mpaka 55kg.

usiku nikilala naweza kuota nipo kanda ya ziwa yaani naota makaburi naweza ota nimeenda kwa bibi lakini nyumba imejengwa makaburini. naweza kuota nipo mochwari yaani kwa ujumla sioti ndoto za kawaida. najikuta wakati mwingine natamani kufa labda naweza kupumzika lakini akili inaniambia ukifa huwezi kupumzika kwa amani kwa sababu mtoto wako hutakuwa umemuacha katika mazingira magumu sana. nimedhoofika sana kichwa kinaniuma kila siku nameza pain killer lakini kuna muda zinadunda.
samahani naombeni msaada wenu nipo njia panda.
Unaota vile unavyivipatia nafasi kuuuuubwa kuviwaza mchana.
Hakuna kibaya hapo,tulia endelea kutafuta nauli ukiipata nenda.
 
Kuna kitu bado hujakisema ambacho ndicho kiini cha changamoto unazopitia. Pata mtu sahihi wa kumueleza kila kitu kuhusu wewe na njia ulizopita mpaka kufikia hapo. Utasaidika vizuri sana na huo mzigo mabegani mwako utautua, utajiskia amani sana. Imani hufanya kazi na Ukweli na uwazi.
nilisema kila kitu kwenye uzi huu Kuna wengine hatujui tulipokosea
 
yaani hata nguvu za kuomba niwe mweli sina. kabla ya vifo hivi kutokea hakuna siku niliacha kuwataja babu na bibi yangu kwenye maombi walivyokufa tu. Ndio nikaona Mungu ameniadhibu vibaya. sitamani tena kuomba
Omba bila kukoma,pitia uzoefu wa Ayubu!Hata Mimi ninayekushauri nimepitia hayo uliyoyaeleza na kuzidi,maana niliwazika baby na Bibi na mke na watoto,hadi nikawa kama nimechanganyikiwa,Wadau hawakuwa nyumba kuniambia Nina Ukimwi.Hivi Sasa Nina watoto warembo na Wana akili darasani,na maisha yangu ni mazuri kama Niko peponi Hata vikwazo vya Trump naona ni upepo tuu wa asubuhi.Mungu ni Mwema hutupitisha kwenye tanuri la moto na hutupa milango ya kumtokea,milango sio mlango.
 
Omba bila kukoma,pitia uzoefu wa Ayubu!Hata Mimi ninayekushauri nimepitia hayo uliyoyaeleza na kuzidi,maana niliwazika baby na Bibi na mke na watoto,hadi nikawa kama nimechanganyikiwa,Wadau hawakuwa nyumba kuniambia Nina Ukimwi.Hivi Sasa Nina watoto warembo na Wana akili darasani,na maisha yangu ni mazuri kama Niko peponi Hata vikwazo vya Trump naona ni upepo tuu wa asubuhi.Mungu ni Mwema hutupitisha kwenye tanuri la moto na hutupa milango ya kumtokea,milango sio mlango.
nitajaribu tena japo nguvu sina tena
 
Pole nakushauri pata rafiki,rafiki ambae ataweza kuwasiliana na wewe muda wowote,atakutoa kwa mawazo na ukajiona uko wa thamani

You need some body…
 
Pole nakushauri pata rafiki,rafiki ambae ataweza kuwasiliana na wewe muda wowote,atakutoa kwa mawazo na ukajiona uko wa thamani

You need some body…
thamani yangu hipi labda? hiko wapi mdogo wangu tumbo moja baba mmoja na mama mmoja yupo hapa Dar lkn nina miaka saba sasa tangu nimuone, nikimpigia huwa hapokei msg hajibu. nimejifungua mwanangu ana miaka 2.5 sasa lkn hajawahi hata kuja kumuona. kama ndugu yako mwenyewe hakuoni wa thamani nani ataiona thamani yako. mama alikuja Tz kumzka mama yake alipitia Dar lkn hakunipigia hata simu. angalau kumwona mjukuu wake. nisipo mgia mimi hata siku moja hawezi hata kukosea namba akanipigia nina miaka 8 sasa tangu niione sura ya mama yangu. babu na bibi waliokuwa wananipa thamani Mungu akawachukua kudhihirisha kuwa mimi si chochote. kinachoniuma ni hiki kiumbe kisicho na hatia. thamani hipi unaongelea labda.
 
thamani yangu hipi labda? hiko wapi mdogo wangu tumbo moja baba mmoja na mama mmoja yupo haha Dar lkn nina miaka saba sasa tangu nimuone, nikimpigia huwa hapokei msg hajibu. nimejifungua mwanangu ana miaka 2.5 sasa lkn hajawahi hata kuja kumuona. kama ndugu yako mwenyewe hakuoni wa thamani nani ataiona thamani yako. mama alikuja Tz kumzka mama yake alipitia Dar lkn hakunipigia hata simu. angalau kumwona mjukuu wake. nisipo mgia mimi hata siku moja hawezi hata kukosea namba akanipigia nina miaka 8 sasa tangu niione sura ya mama yangu. babu na bibi waliokuwa wananipa thamani Mungu akawachukua kudhihirisha kuwa mimi si chochote. kinachoniuma ni hiki kiumbe kisicho na hatia. thamani hipi unaongelea labda.

Wewe ni wa thamani sana Kidoti nasisitiza
 
Usikasikirike au kuchukia kwa kitu usichoweza kukizuia hakuna kosa hata moja hapo linalokuhusu moja kwa moja makosa yote yalikuwa nje ya uwezo wako.

Kila kitu kinatokea kwasababu ukipata mda na pesa nenda katembelee makaburi yao na ufanye maombi au dua maalum kwa ajili yao hyo hali ni kawaida katika maisha.

Mimi mwenyewe mwaka jana nilimpoteza mzee wangu ni hali ambayo itachukua mda kuizoea kwasababu nakumbuka vitu vingi na naona kama life is not fair.

Nashukuru nina kazi but nahisi ni kama kuna kitu kimepungua kwenye maisha yangu vitu hvyo ni kufiwa na baba yangu mzazi na kuumwa kwa mama yangu mkubwa ambaye alinisomesha na kunilea na haoni kabisa ukifika mpaka ujitambulishe wewe ni nani.


Kwenye maisha hvyo ni vitu vya kawaida mimi I'm not happy 100% kwasababu watu wanaotakiwa kula matunda yangu mmoja hayupo duniani mwingine ni mgonjwa na kuona haoni ambayo yupo ni bi mkubwa maisha yanaenda hivyo japokuwa sio kama zamani nimeamini mungu akikupa kimoja anakunyima kingine kikubwa uzima tu.

Alamsik.
 
Back
Top Bottom