Naombeni msaada wenu

Unaota vile unavyivipatia nafasi kuuuuubwa kuviwaza mchana.
Hakuna kibaya hapo,tulia endelea kutafuta nauli ukiipata nenda.
 
nilisema kila kitu kwenye uzi huu Kuna wengine hatujui tulipokosea
 
yaani hata nguvu za kuomba niwe mweli sina. kabla ya vifo hivi kutokea hakuna siku niliacha kuwataja babu na bibi yangu kwenye maombi walivyokufa tu. Ndio nikaona Mungu ameniadhibu vibaya. sitamani tena kuomba
Omba bila kukoma,pitia uzoefu wa Ayubu!Hata Mimi ninayekushauri nimepitia hayo uliyoyaeleza na kuzidi,maana niliwazika baby na Bibi na mke na watoto,hadi nikawa kama nimechanganyikiwa,Wadau hawakuwa nyumba kuniambia Nina Ukimwi.Hivi Sasa Nina watoto warembo na Wana akili darasani,na maisha yangu ni mazuri kama Niko peponi Hata vikwazo vya Trump naona ni upepo tuu wa asubuhi.Mungu ni Mwema hutupitisha kwenye tanuri la moto na hutupa milango ya kumtokea,milango sio mlango.
 
nitajaribu tena japo nguvu sina tena
 
Pole nakushauri pata rafiki,rafiki ambae ataweza kuwasiliana na wewe muda wowote,atakutoa kwa mawazo na ukajiona uko wa thamani

You need some body…
 
Pole nakushauri pata rafiki,rafiki ambae ataweza kuwasiliana na wewe muda wowote,atakutoa kwa mawazo na ukajiona uko wa thamani

You need some body…
thamani yangu hipi labda? hiko wapi mdogo wangu tumbo moja baba mmoja na mama mmoja yupo hapa Dar lkn nina miaka saba sasa tangu nimuone, nikimpigia huwa hapokei msg hajibu. nimejifungua mwanangu ana miaka 2.5 sasa lkn hajawahi hata kuja kumuona. kama ndugu yako mwenyewe hakuoni wa thamani nani ataiona thamani yako. mama alikuja Tz kumzka mama yake alipitia Dar lkn hakunipigia hata simu. angalau kumwona mjukuu wake. nisipo mgia mimi hata siku moja hawezi hata kukosea namba akanipigia nina miaka 8 sasa tangu niione sura ya mama yangu. babu na bibi waliokuwa wananipa thamani Mungu akawachukua kudhihirisha kuwa mimi si chochote. kinachoniuma ni hiki kiumbe kisicho na hatia. thamani hipi unaongelea labda.
 

Wewe ni wa thamani sana Kidoti nasisitiza
 
Usikasikirike au kuchukia kwa kitu usichoweza kukizuia hakuna kosa hata moja hapo linalokuhusu moja kwa moja makosa yote yalikuwa nje ya uwezo wako.

Kila kitu kinatokea kwasababu ukipata mda na pesa nenda katembelee makaburi yao na ufanye maombi au dua maalum kwa ajili yao hyo hali ni kawaida katika maisha.

Mimi mwenyewe mwaka jana nilimpoteza mzee wangu ni hali ambayo itachukua mda kuizoea kwasababu nakumbuka vitu vingi na naona kama life is not fair.

Nashukuru nina kazi but nahisi ni kama kuna kitu kimepungua kwenye maisha yangu vitu hvyo ni kufiwa na baba yangu mzazi na kuumwa kwa mama yangu mkubwa ambaye alinisomesha na kunilea na haoni kabisa ukifika mpaka ujitambulishe wewe ni nani.


Kwenye maisha hvyo ni vitu vya kawaida mimi I'm not happy 100% kwasababu watu wanaotakiwa kula matunda yangu mmoja hayupo duniani mwingine ni mgonjwa na kuona haoni ambayo yupo ni bi mkubwa maisha yanaenda hivyo japokuwa sio kama zamani nimeamini mungu akikupa kimoja anakunyima kingine kikubwa uzima tu.

Alamsik.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…